Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 899
- 1,231
Huuo mpira wa bongo sio poa ni vyema TFF ihamishiwe TAMISEMI rais ateue mwenyewe maana kila anayeteuliwa madudu kuliko ya mwanzo
Anaandika shaffih Dauda;
Goodmorning!Nimefuatilia kwenye vyanzo vyangu vyote kutaka kufahamu kwanini Simba SC na Stand UTD walivaa jezi zinazofanana,kwenye pre match meeting iliyohudhuliwa na viongozi wa vilabu vyote pamoja na kamisaa (Jovin Bagenda) na mwamuzi wa mchezo huo (Kinungani Selemani )
Kanuni zinasemaje? (i) Kamishna atahakikisha timu zinatumia sare kwa mujibu wa rangi za
nyumbani na ugenini kama zilivyoandikishwa na klabu zenyewe kwa TFF. (j) Timu zitaheshimu uchaguzi wao wa rangi za sare zao kwa michezo ya nyumbani na ugenini, na endapo itatokea timu ya nyumbani kukosa uzingativu wa kuwasilisha rangi sahihi kwa sare zake kwa mechi za
nyumbani katika kikao kitangulizi cha mchezo (pre match meeting) timu ngeni itakuwa na haki ya kwanza ya kuchagua rangi ya sare katika mchezo husika.
Baada ya utafiti wangu nimejiridhisha ya kwamba Simba hawakuwa tayari kuvaa jezi za ugenini kutokana na maagizo ya 'KAMATI' ikabidi kamishna wa mchezo akubali kwasababu jezi za Stand zilikuwa ni za rangi ya machungwa na Simba rangi nyekundu kwaiyo zisingewasumbua waamuzi.