Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
Mwaka 2000 wakati Wajerumani wakipitia kipindi kigumu kwenye mashindano ya EURO-2000 ndicho kipindi walimuita Lother Mathius aje kuokoa jahazi. Kipindi England walipokuwa na wakati mgumu 2011 waliwaita kina Alan Shearer waje kuwapa motisha wachezaji. Kipindi Cameroon walipotaka matokeo waliwatumia kina Nkono, Roger Milla na Biyik kuwapa motisha wachezaji. Hata Crotia waliwapeleka kambini kina Boban na Davor Suker kuwapa mbinu wachezaji. Kesho Tanzania wanatafuta matokeo kwa kuwatumia Shilole na Wema Sepetu. Kuna vitu vinafurahisha sana yaani Shilole amekuwa muhimu kwenye soka kuliko Lunyamila na Chambua Sekilojo. Wema anakuwa na mchango wa ushindi kuliko Pawasa na Matola? Nahisi wanafananisha soka na Bar, Casino ama Club za music na pombe. Wamesahau kuwa mpira ni science inayoitaji taaluma, weledi na ustarabu wa hali ya juu. Mpira hautaji picha za uchi kama mziki wala skendo za ngono bongo movie. Naacha akiba ya maneno hadi baadae baada mechi nitaeleweka tu.
'When you’ve been an Arsenal fan as a kid, you will be one your whole life in some way.” David Alaba
'When you’ve been an Arsenal fan as a kid, you will be one your whole life in some way.” David Alaba