BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Ukifuatilia siasa za Tanzania kuna mambo mengi sana yanachukuliwa poa lakini kiuhalisia yanaweza kuwa kikwazo cha Tanzania kutofanikiwa kwenye mambo mengi.
Kuna jambo ambalo najua mimi sitakuwa wa kwanza kulizungumza, hili suala la Wabunge wetu kuwa sheria au niite kigezo cha kwanza lazima ajue kusoma na kuandika, sawa ni kitu kizuri lakini tumeshawahi kujiuliza uzito wa mambo ambayo yanapita Bungeni na levo ya elimu ya baadhi ya Wabunge wetu?
Sio kwamba nawakosea heshima, nikutolee mfano wakati Job Ndugai akiwa Spika kuna kipindi aliwahi kunukuliwa akiizungumzia Sheria fulani ndani ya Bunge na kusema hajui ilipitajepitaje hadi kuwa Sheria.
Inawezekana ilipitishwa kisiasa ndio maana hakujali hilo lakini pia inawezekana ilipitishwa kwa kuwa Wabunge kadhaa kutokana na levo yao ya elimu inawezekana kuna baadhi ya mambo yanakuwa mazito kwao kuyachanganua.
Simaanishi kuwa Wabunge lazima wawe na elimu kubwa sana, HAPANA, wapo wenye elimu kubwa hadi ngazi ya Profesa lakini mambo wanayoyafanya hata wale wa darasa la 7 wanawazidi kwa kiwango kikubwa tu.
Ushauri wangu hiki kipengele kibadilike kuhusu kigezo cha elimu ya kujua kusoma na kuandika kwa kuwa Bungeni kuna hoja nyingi nzito, zipo za kisheria, zipo za kiuchumi na nyingine nyingi, ambazo uelewa wake angalau ukiwa na elimu ya kidado cha nne au sita.
Basi kama itashindikana wale walioingia kwa kupitia mgongo wa darasa la saba wanaweza kujiendeleza kielimu ili wawakilishiwetu hao wawe angalau na upana wa uelewa katika kuchambua mambo, huu ni mwaka 2022 mambo ya kuishia elimu ya msingi kisha ukapewa nafasi ya kuongoza mamilioni ya watu si sawa.