unajua Watanzania tulio wengi kama sio wote ikijumulisha na wewe na mimi tumekuwa confused. Utakataa au utakubali lakini haitabadidilisha hilo mkuu, wengi wetu ni dhaifu kama ilivyowekwa na Mh Myika siku moja Bungeni.
Angalia wanaoendesha mpira wa Tanzania (hasa katika capital city) ni akina nani ...zaidi ya 96% ni watu ambao ni hopeless na upeo wa malengo yao ni mdogo mno. Mtu anaweza kuzuia jambo la maana lisifanyike just kwa ahadi ya sahani ya pilau na sod tu, aibu.
Kuna jamaa mmoja yuko Simba SS pia na huwa anaongea sana kwenye kipindi cha TV cha Sport Kizaazaa, jamaa ni mbishi na mwenye jazba sana lakini nilipokuja kushtuka ni pale nilipogundua kuwa ndiye katibu mwenezi wa ccm wa mkoa wa Dar es Salaa (nafasi ya Nape kitaifa). Na nadhani uliona hata julio alitaka kugombea nafasi nyingine ccm.
naeleza hayo yote hili angalau kutoa picha ya hali halisi ilivyo.
Katika mpira wa Tanzania ikichochewa na dar es Salaam, bila kujua fitina na unafiki huwezi kufanya lolote na huo ndio msingi wa viongozi wa Simba na Yanga. Lakini kama tunavyojua unafiki na fitina ndio msingi mkubwa wa umasikini wa mtu/jamii/jumuia/chama/timu/taifa lolote hapa duniani.
Hiyo hoja ya Vodacom ni muendelezo huo huo wa watu ambao ni hopeless na wasiowaza mbali zaidi ya matumbo yao. Tuliiga mambo ya mpira kutoka Ulaya lakini huko japo wana mambo yao ya rangi za jezi (identity) likija suala la biashara na pesa hawaangalii hilo, wanaangalia pesa na maendeleo.
Well stated mkuu lakini hili jambo yapaswa tuliangalie kwa mapana yake, maana linanikumbusha kitabu fulani nilichokisoma (nafikiri ni beautiful ones are not yet born) kilikuwa na ndege aitwaye chichidodo ndege huyu alikuwa ana chukia kinyesi lakini anapenda mafunza yanayotoka kwenye hicho kinyesi, so hili la Yanga huu ndo mfano wake kwasababu anachukua kila kitu kwa mdhamini halafu anakataa nembo yake kisa ni nyekundu na nyeupe, tatizo lingine ni uongozi wa TFF umejaa usimba na Uyanga, just imagine badala ya Rais wa TFF kushughulika na hili swala maana ni wao walioingia mkataba na Vodacom anasema kuwa Vodacom wakutane na Yanga kujadili swala hili.