Hili lililomkuta Bashe liwe fundisho kwa Mawaziri

Viongozi wa kiafrika,hawana utamaduni wa kujiuzulu.
Hata ingekuwa mimi sijiuzuru kwani nisipojiuzuru kuna hasara gani?

1. Gari VXR unapewa bure
2. Bima
3. Malupulupu kibao
4. Mshahara mnono
5. Nyumba unapewa na serikali
6. Mafuta ya gari serikali inakuhudumia


Halafu nijiuzuru nijipeleke kwenye shida!
 
Watu huwa ni kama hawamuelewi mpina.....this guy is so logical,wabunge wengi hudhani mpina ana ghubu ya kuvuliwa uwaziri.
Napenda sana michango yake, anaona tatizo na kulitolea ufumbuzi.
Bashe kujifanya kujibu hoja konki ya Mpina na ka kingereza uchwara amelamba matapishi.

Ety'' is very danger''... Bure kabisa.
 
Naomba kujuzwa huo Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea BPS unavyofanya kazi?
BPS ni ufupisho wa nini?
 
Liwe fundisho kweli hasa kwa wale mawaziri wanaopenda kupandisha mabega na kujifanya wanajua kila kitu badala ya kusikiliza hoja za wabunge ambao kimsingi ndio waliopewa jukumu la kuisimamia Serikali.
 
Liwe fundisho kweli hasa kwa wale mawaziri wanaopenda kupandisha mabega na kujifanya wanajua kila kitu badala ya kusikiliza hoja za wabunge ambao kimsingi ndio waliopewa jukumu la kuisimamia Serikali.
bashe ni kiongozi mzuri ila hapa alipotoka sana lakini nimeona akiwa kilosa alitangaza kurejesha mambo yote yaliyoshauriwa na Mpina ikiwemo BPS, BEI ELEKEZI NA USIMAMIZI MZURI WA RUZUKU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…