Sikuwa najua kumbe huyu mlinzi wa hii Kampuni kubwa ya Ulinzi hapa DSM usiku ana mwalika mwenzie aje alale kibarazani pangu apigwe na AC.
Unajua mimi kwenye hii apartment ninayoishi ina vyumba 4. Kila chumba,korido,jikoni,washrooms zote vyumbani kuna AC. nikaamua na kuweka AC kibarazani pia ili napokaa pale nje nijisikie kama nipo home kule Ulaya au Marekani.
Mimi ukija kwangu njoo na jacket au sweater.na hizi AC ni heavy duty zinawaka 24x7 yaani unaweza sema umeingia kwenye friji.
Ila sasa usije ukadhani ni friji.no...lile friji ndo kuna mtu mmoja nlimkaribisha siku moja akaingia ndani ni kama chumba kabisa unaweka kitanda cha 6x5 na sofa mbili.
Ni friji ambalo nlitoka nalo Israel.kubwa sana. Ukiliacha mlango wazi unaweza kuta kila maji kwenye nyumba yameganda.
So kumbe usiku walinzi wengine wanakimbia malindo yao wanakuja kulala kibarazani pangu.wapate ubaridi na faraja moyoni.nmejisikia huzuni sana.
Siku naweka ile AC pale kibarazani fundi akanambia eti ngeweka fan.nlimwambia fan zinasambaza vumbi.lakini sasa nmegundua kumbe nimesaidia watu kupata faraja.
Basi angalau kwa hali hii sipati joto kabisa la dar.na pia inanisaidia kukumbuka hali ya majira ya baridi ulaya na marekani.
Nipo hapa naangalia CCTV cameras ndo nawaona walinzi wawili wamelala usingizi mzito huku wanatabasamu.bunduki wameweka chini mmoja mkono mmoja kaingiza kwenye suruali.wamelala huku wametabasamu kwa furaha.
Nimetokwa na machozi kwa furaha na huzuni.