Kwanza pole kwa hayo yote dada angu,
Sina familia lakini kwa hali ya kawaida sidhani kama hio ni sahihi kwa baba kuwa wa staili hio.
Najua hapa utapata ushauri mzuri tu, lakini na mbaya pia.
Sasa ili uweze kuchanganya ushauri utakaoupata hapa na akili zako mwenyewe hebu, jaribu kumshirikisha Mungu.
Ingia chumba chako cha ndani, moyoni mwako I mean, muombe Mungu, akuongeze katika kupata majibu ya hili tatizo lako.
Halafu omba utulivu wa moyoni, hakikisha moyoni una utulivu, usiwe na hasira, chuki wala lawama juu ya baba huyo.
Imagine hivi, Angekuwa ametangulia mbele ya haki (si ombei) usingeweza kuhudumia watoto wako na wewe mwenyewe?
Jitengenezee confidence ndani yako, kwamba you can without him.
Ukifanikiwa hapo, andaa safari na mpango mzuri tu, wenye hekima na unyekekevu ndani yake.
Ukae na huyo baba/mume wako mpendwa, uzungumze nae, msikilize, mueleze vile unavyojisikia, hapo nadhani na Mungu akiwa upande wako,
Utamuelewa tu nia yake ni nini hasa.
Kumbuka hekima ya pekee inatakiwa hapa dada, zingatia utulivu moyoni, utaipata tu nia yake.
Ukisha fahamu nia yake hata kama haitakuwa nzuri kwako, still usikate tamaa,
utaumia lakini usikate tamaa kamwe, kumbuka unaweza, Yes you can even without him. Maana hata sasa umeweza.