TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,087
- 3,156
UTANGULIZI
Idadi ya wahitimu wa vyuo katika ngazi mbalimbali hapa nchini ni kubwa sana ikilinganishwa na idadi ya nafasi za ajira na serikali zinatangazwa katika mwaka husika,sambamba na hilo kuna mlundikano wa wahitimu wa miaka ya nyuma jambo linalofanya kuongeza ushindani katika soko la ajira.
Wahitimu wa miaka ya nyuma wananafasi kubwa yakuajiriwa katika kila ajira zinazotolewa ikilinganishwa na wahitimu wapya, sambamba na hilo Serikali haiwezi kuajiri angalau theluthi ya wahitimu wote kila mwaka,na mashirika binafsi yakiungana na serikali bado hayawezi kuajiri hata robo ya wahitimu wote kwa mwaka,na hapo hapo kuna mlundikano wa wahitimu miaka ya nyuma.
Sambamba na hilo elimu ya Tanzania haimuandai mhitimu kujiajiri,kadhalika serikali pia,wahitimu pia wana ugonjwa wa kufikiria kuajiriwa,hawana mshipa wa kufikiria kujiajiri kabisa,nawanajisahau kabisa pindi wawapo masomoni kuwa kuna maisha baada ya chuo,na kuna balaa la kutafuta ajira baada ya masomo wanakuja kushituka mwishoni wakati ubao unasoma tofauti na matarajio yao.
SERIKALI IPUNGUZE MANENO.
Viongozi wa kiserikali wamekuwa wakitoa kauli kedekede kwamaba vijana wasitegemee kuajiriwa wajiajili,maneno laini laini tu,nahakuna namna yeyote ambayo inaonesha vijana hawa wajiajiri vipi,hakuna mfumo sahihi wakuwafanya hawa vijana wajiajiri,ba ukisogea ba kutazama kwa ukaribu ni kama hawana mpango kabisa wakukabiliana na janga hili.
MAMBO YANAYOKWAMISHA WAHITIMU KUJIAJIRI.
Vipo vitu vingi ambavyo vinawakwamisha wahitimu kujiajiri,yakiwemo mambo kama upeo mdogo wa kufikiri,
tama ya maisha ya haraka,maisha ya ushindani na kujionesha,wivu au choyo na ubinafsi,hofu yakufirisika,kukosa mtaji,elimu isiyo na maarifa,uvivu,kukata tama,kuishi kwa matamanio,Mikakati na sera mbovu za kiserikali Na mengine mengi kama haya.
Yamkini wapo wenye mawazo ya kutaka kujiajiri lakini vingi vina wakwamisha kutoka hayo tajwa hapo juu,mazingira mabovu ya nafasi za kujiajiri na sera mbovu za ajira ni chanzo cha haya yote kwa viwango zaidi.
SERIKALI ITENGENEZENI MAZINGIRA YA WAHITIMU WENGI KUJIAJIRI ILI WAAJIRI KWA MFUMO HUU.
Kwa kuwa changamoto kubwa katika suala zima la kujiajiri ni mitaji,lakini pia kunachangamoto kubwa zaidi ya kustahimili mikiki ya biashara hasa wakati wakipindi cha mpito hivyo kusababisha wengi kukata tamaa.
Serikali inatakiwa kuanzisha utaratibu wa wahitimu watarajiwa kujiaajiri baada ya kuhitimu,serikali ianzishe mfumo wakuwadhamini wahitimu watarajiwa ambao wataonesha sababu yakinifu ya kujiajiri kupitia mawazo ya biashara ya tofauti,na kipaumbele kiwe kwenye mawazo ambayo yatakuwa na uhitaji mkubwa wa kuajiri hapo baadae.
Serikali kupitia wizara ya elimu,wizara ya fedha na wizara ya ajira,itafute wadhamini kila mwaka au makampuni makubwa ya mikopo ambayo itawakopesha wahitimu hao kupitia serikali,ambapo angalau kila mwaka yatoke makundi kadhaa kulinga na idadi ya wahitimu watarajiwa katika mwaka husika na lengo liwe kuwafanya angalau robo ya wahitimu wote kujiajiri kwa kila mwaka.
Makundi haya yatakuwa yakiendeshwa katika mfumo wa makampuni,Sherti liwe kundi lililoundwa na watu wasiopungua 20 ambao ni wahitimu watarajiwa,wanafunzi hawa wataandaa mpango kazi wa biashara yao ambayo wanataka kuanzisha kisha kuiwasilisha katika sekretarieti ya ajira ama vyovyote itakavyo undwa ila nilazima isimamiwe na serikali kuu.
Mawazo hayo ya biashara yatafanyiwa mchujo wa awali na chombo cha uchambuzi ambacho kitakuwa kimeundwa na wataalamu wa masuala ya biashara,usimamizi wa fedha,ujasiriamali nakazalika.
Makundi yatakayopita yatatangazwa na baada ya hapo kutakuwa na tukio la makundi husika kutetea mawazo yao ya biashara kwa kuzingatia mpango kazi waliouwasilisha. Mbele yawachambuzi.
Wataalamu wa biashara katika Nyanja tofauti watakuwepo kuuliza maswali ili kuishawishi sekretarieti,,na kundi zuri liwe lile ambalo limeundwa na mchanganyiko wa wahitimu kutoka katika fani tofauti tofauti kama vile biashara,usimamizi wa fedha nk.
Serikali itatakiwa kutafuta wadhamini kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwa lengo la kupata fedha na kutafuta mikopo kwa ajili ya kuwezesha wahitimu kujiajiri,kisha serikali itayakopesha makundi ambayo yatakuwa yametetea mawazo yao kwa uyakinifu na kushinda.
Serikali itakopesha makundi hayo ambayo yatakuwa yameshasajiriwa kama makampuni na ambapo kila mwanakundi atatambulika kwa hisa ambazo zitagawanywa sawa kulingana na thamani ya biashara yao na pesa waliyokopeshwa na serikali.
Serikali kupitia wizara husika itakuwa mlezi wa makampuni hayo katika kipindi cha mpito kwa ajili yakuhakikisha biashara zinasimamiwa vizuri,na mikopo hiyo itaanza kurejeshwa baada ya kipindi cha mpito,kwamba kampuni zitakuwa zimeanza kutengeneza faida,hii itasaidia kampuni kutokwama mapema kutokana na marejesho ya mapema wakati kampuni ipo kipindi cha mpito.
Itakuwa ni jukumu la serikali pia kuhakikisha kwamba kampuni hiyo inafuata mpango kazi wa biashara kama ilivyowasilishwa hapo awali na kupewa nafasi,baada ya kampuni hizo kuonekana kwamba zimeimarika basi wataziacha zijisimamie zenyewe,na kuendelea kulipa deni lao.
Makampuni hayo baada ya kuwa yamepevuka yatakuwa na uwezo wa kuajiri wahitimu wapya,masalani chukulia serikali ikadhamini makundi tufanye mia moja (100) kila mwaka maana yake tutakuwa tumewafanya vijana elfu mbili (2,000) wajiajiri kila mwaka,na tutakuwa na makampuni mia moja (100) kila mwaka,ambayo makampuni hayo kila moja likiwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi tufanye mia mbili (200) tu kwa mwaka maana yake tutakuwa tumeajiri wahitimu elfu ishirini (20,000).
Maana yake serikali ikiweka mkatata wa utekelezaji kwa muda wa miaka kumi (10) nakulifikia lengo,basi katika kipindi hicho tutakuwa na ajira 220,000 kwa makampuni mia moja (100) yaliyotengenezwa katika mwaka mmoja tu,sasa kama serikali itakuwa imefanya kazi hiyo kwa muda wa miaka yote kumi(10) maana yake itakuwa imetengeneza makampuni elfu moja (1,000) .
HITIMISHO.
Suala hili ni suala Zito linalohitaji umakini na usimamizi yakinifu,ni lazima lisimiamiwe na serikali kuu ili kuepusha kukwama kutokana na sababu za weledi wa watakaoteuliwa kusimamia.
Serikali ioneshe kwa vitendo kuwa inata vijana wajiajiri kwa MFUMO upi nasio kuongea tu.
Ahsante

Upvote
1