Hili ndilo Lengo la Maisha

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,323
Reaction score
10,813
Habari Wakuu.

Jukwaa hili ni kwa watu wenye fikara yakinifu na wenye kufikiri sana. Basi ikiwa ni hivyo natumaini mada hii itakuwa sehemu ya kufikirisha na kutoa maarifa kwa wale waliotayari kupata maarifa hayo.

Pengine umekuwa mmoja wa watu wenye kujiuliza kwa nini unaishi, Nini lengo la maisha, kwa nini uzaliwe hapa na si pale, kwa nini uzaliwe na huyu na si yule, Kwa nini umzae huyu na si yule, Kwa nini, kwa nini isiyoisha. Ikiwa umewahi kujiuliza hayo basi jua nawe upo katika listi ya watu wenye akili nyingi.

Maswali haya ili yajibiwe sharti Imani ijumuishwe. Lazima majibu yatolewe kwa minajili ya kidini hasa kwa waamini na waaminio. Kinachofurahisha ni kuwa kila mwanadamu amepewa namna ya kuamini. Hii ni kusema hakuna mtu asiyeamini yaani asiye na imani.

lengo la maisha ni moja tuu. Ukishalifahamu lengo hili basi maisha hayatakusumbua abadan. Utakachokifanya ni kuhakikisha unafuata njia ya kufikia lengo kuu. Utahakikishaje unafuata njia itakayokufikisha katika lengo kuu la maisha ni kwa kusoma maandiko mbalimbali matakatifu yenye dalili zote ya Mungu. Bila kujali yanamrengo wa Kikristo, Kiislamu, Kihindu au Kimila(kiafrika).

Ikiwa maandiko/mafundisho hayo hayaudhuru mwili wako wala mwili wa jirani yako basi hayo ndio maandishi bora kabisa.

Lengo la maisha ni kuishi kwa furaha yenye kiasi:
Binadamu upo kwa lengo la kufurahia maisha ya hapa duniani. Mtu mmoja anaweza kujiuliza "nitawezaje kuishi kwa furaha" Hilo ndilo swali muhimu sana.

Zipo njia kadha wa kadha ambazo kwazo lazima uishe kwa furaha. Mungu alipomuumba Binadamu alikusudia mambo kadhaa. Lakini lengo kubwa la maisha likiwa ni furaha.

Akili yangu inanituma kusema Mungu aliona njia pekee ya mwanadamu(wewe) kuwa na furaha ambalo ndilo lengo la maisha ni kutawala(uhuru).

Kutawala ndio njia ya kwanza ya kuishi kwa furaha ndio maana watu wengi na mataifa mengi hupigana ili yaweze kujitawala. Kupitia kutawala dunia, bahari na anga ndipo chanzo cha furaha hujitokeza. Ndio maana wenzetu wazungu huhangaika usiku na mchana baharini na kwenye anga za mbali ili kukamilisha jambo hili yaani kuitawala dunia. Huwezi ishi kwa furaha na amani ikiwa utawala haupo mikononi mwako. Hata vita ya kiroho huhusu utawala.

Ndipo nikafikiri kuwa; Mungu alipohitaji mwanadamu kutawala ili aishi kwa furaha aliona si kazi nyepesi bila kumpa njia na namna mbalimbali za kufanya ili aweze kuitawala dunia.

Zifuatazo ndizo njia pekee alizoziona Mungu kuwa ndizo zitakazo msaidia Binadamu kuishi kwa furaha:

  • Alimpatia miongozo, amri na sheria mbalimbali ambazo kupitia hizo basi mtu (hapa ni wewe na mimi) ataweza kuitawala dunia na maisha yake.
Sheria zilizotolewa ambazo sharti mtu azishike ili afikie lengo la maisha ni hizi zifuatazo;
  1. Sheria za mahusiano
  • Mahusiano ya mtu na Mungu
  • Mahusiaono ya Mtu na Mtu
    • Waheshimu wazazi wako
    • Usiibe, Usiue, usizini, Usiseme uongo, Usitamani.
2. Sheria za kazi, mapumziko
  • Sheria za kazi
    • Fanya kazi kwa siku sita
    • Toa zaka sehemu ya kumi ya mapato au mazao yako
    • Toa sadaka kwa wenye mahitaji na shughuli za kijamii ikiwepo Kodi, ushuru n.k
  • Sheria za Mapumziko
    • Siku ya sabato pumzika ukimtukuza Mungu kwa kutambua nawe uliumbwa
    • Adhimisha sikukuu zilizoamriwa za kidini, kitaifa na binafsi. Binafsi ni kama sherehe za siku ya kuzaliwa rejea kitabu cha ayubu na watoto wake walioenda kufurahia kwa kaka yao mkubwa.
3. Sheria za Vyakula na Vinywaji
  • Kula vyakula vilivyoagizwa kuepuka magonjwa yatakayokupotezea furaha yako. Pendelea nafaka, matunda, mboga za majani kwa wingi
  • Kunywa vinywaji safi hasa hasa maji kwa wingi na Juisi za matunda.
4.Sheria za Mavazi na mapambo ya mwili
  • Mwanaume avae mavazi na mapambo yampasayo
  • Mwanamke avae mavazi mapambo yampasayo
  • Mtu asiuchore mwili wake iwe kwa chale au kwa Tattoo.
  • Mtu asinyoe kipara, kiduku, au mitindo yoyote ya nywele
  • Mwanaume asisuke
5. Sheria za ndoa, talaka, Mirathi na maziko
  • Oa mwanamke/wanawake bikra safi umpendae/uwapendao
  • Toa mahari kwap mwanamwali umuoae
  • Zaa watoto idadi uipendayo
  • Mpe talaka mwanamke mzinzi na muasherati
  • Mpe Talaka Mwanamke mchawi, na mshirikina
  • Mzaliwa wa kwanza apewe kipaombele cha urithi kwa kiwango kikubwa tofauti na wengine. Bila kujali ni wa mke wa kwanza au wa pili, Umpendaye au usiyempenda hapa kigezo ni Uzaliwa wa kwanza.
  • Kila familia(wake zako) ijitegemee kwa mali na miradi ya vipato
  • Mtoto wakike hana haki sawa na kijana katika suala la urithi.
  • Chukua mahari umwozapo binti yako
  • Zikwa katika ardhi ya Baba na babu zako. Usizikwe uhamishoni au utumwani.
6. Sheria za Mamlaka
  • Baba ndiye kichwa cha Familia
  • Mke ndiye msaidizi
  • Mtoto wa kwanza wakiume ndiye kiongozi namba tatu katika familia.
  • Heshimu mamlaka inayoheshimu na kusimamia sheria za Mungu katika Jamii au taifa lako.
Ukishika mambo hayo hapo basi utakuwa na maisha yenye furaha pasipo kujali unaelimu au hauna elimu, una dini au hauna dini. Kuishi kwa furaha ndilo lengo la maisha.

Karibuni kwa mjadala.
 
hapo penye kuoa wanawake bikra hapo....unaweza tafuta hata kwa tochi na maana nzima ya maisha ama hata ukazeeka usimpate huyo bikra, labda ubake mwanafunzi
 
hapo penye kuoa wanawake bikra hapo....unaweza tafuta hata kwa tochi na maana nzima ya maisha ama hata ukazeeka usimpate huyo bikra, labda ubake mwanafunzi


Wanawake bikra wapo mkuu, tena wengi tuu.

kuoa mwanamke asiye bikra ni kuupa nguvu uzinzi.
 
Leo acha nichangie tu ntasoma siku nyingine. Ahsante.
 
bikra nyingi za kutengeneza........

yupo binamu....sihitaji kuzungumzia mambo gani hupita kwa mabinamu ila, ilikuwa hv, kabinamu kalikuwa kakibrashiwa tangu la saba, na kidato cha pili ka njia kakawa wazi, binamu akalipenda rungu, akanogewa, akawa mwalimu, sasa kuna mambo yakawepo hawa watu ukiangalia ni ndugu hawawez oana, ikabidi huyu aolewe mashariki, mwingine aoe magharibi...wiki mbili kabla huyo msichana hajaolewa akampelekea ndugu yake amtambikie, jamaa akatunukiwa siku tatu non stop kisha yule bi dada akaingia kijiji flani, akapewa vya kupewa kitumbua kikasinyaa...akaolewa....sasa ajabu siku ya harusi bwana harus na wapambe wanafurah mchiz wao kapata mtoto bikra...wakati kama sijakosea yule bi harus kisha uonja ududu si chini ya mara 40 hivi....ngoja niishie hapo
 


Mpaka sasa hujui bikra feki na OG
 
Nimependa tu sheria ya Kazi na Mapumziko... Ikumbuke siku ya SABATO uitakase, siku sita Fanya kazi na utende mambo yako yote, Lakini siku ya Saba ni SABATO ya BWANA MUNGU WAKO.
 
Nimependa tu sheria ya Kazi na Mapumziko... Ikumbuke siku ya SABATO uitakase, siku sita Fanya kazi na utende mambo yako yote, Lakini siku ya Saba ni SABATO ya BWANA MUNGU WAKO.

Sheria zina tegemeana mkuu
 
nitakuuliza swali moja..
kuishi kwa furaha yenye kiasi kunamfaidisha nini huyo Mungu..?
 
nitakuuliza swali moja..
kuishi kwa furaha yenye kiasi kunamfaidisha nini huyo Mungu..?
 
nitakuuliza swali moja..
kuishi kwa furaha yenye kiasi kunamfaidisha nini huyo Mungu..?


Kuishi kwa furaha hakuna athari chanya wala hasi kwa Mungu bali kwako wewe au binadamu yeyote.
Mungu hafaidiki na chochote kutoka kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…