Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,323
- 10,813
Habari Wakuu.
Jukwaa hili ni kwa watu wenye fikara yakinifu na wenye kufikiri sana. Basi ikiwa ni hivyo natumaini mada hii itakuwa sehemu ya kufikirisha na kutoa maarifa kwa wale waliotayari kupata maarifa hayo.
Pengine umekuwa mmoja wa watu wenye kujiuliza kwa nini unaishi, Nini lengo la maisha, kwa nini uzaliwe hapa na si pale, kwa nini uzaliwe na huyu na si yule, Kwa nini umzae huyu na si yule, Kwa nini, kwa nini isiyoisha. Ikiwa umewahi kujiuliza hayo basi jua nawe upo katika listi ya watu wenye akili nyingi.
Maswali haya ili yajibiwe sharti Imani ijumuishwe. Lazima majibu yatolewe kwa minajili ya kidini hasa kwa waamini na waaminio. Kinachofurahisha ni kuwa kila mwanadamu amepewa namna ya kuamini. Hii ni kusema hakuna mtu asiyeamini yaani asiye na imani.
lengo la maisha ni moja tuu. Ukishalifahamu lengo hili basi maisha hayatakusumbua abadan. Utakachokifanya ni kuhakikisha unafuata njia ya kufikia lengo kuu. Utahakikishaje unafuata njia itakayokufikisha katika lengo kuu la maisha ni kwa kusoma maandiko mbalimbali matakatifu yenye dalili zote ya Mungu. Bila kujali yanamrengo wa Kikristo, Kiislamu, Kihindu au Kimila(kiafrika).
Ikiwa maandiko/mafundisho hayo hayaudhuru mwili wako wala mwili wa jirani yako basi hayo ndio maandishi bora kabisa.
Lengo la maisha ni kuishi kwa furaha yenye kiasi:
Binadamu upo kwa lengo la kufurahia maisha ya hapa duniani. Mtu mmoja anaweza kujiuliza "nitawezaje kuishi kwa furaha" Hilo ndilo swali muhimu sana.
Zipo njia kadha wa kadha ambazo kwazo lazima uishe kwa furaha. Mungu alipomuumba Binadamu alikusudia mambo kadhaa. Lakini lengo kubwa la maisha likiwa ni furaha.
Akili yangu inanituma kusema Mungu aliona njia pekee ya mwanadamu(wewe) kuwa na furaha ambalo ndilo lengo la maisha ni kutawala(uhuru).
Kutawala ndio njia ya kwanza ya kuishi kwa furaha ndio maana watu wengi na mataifa mengi hupigana ili yaweze kujitawala. Kupitia kutawala dunia, bahari na anga ndipo chanzo cha furaha hujitokeza. Ndio maana wenzetu wazungu huhangaika usiku na mchana baharini na kwenye anga za mbali ili kukamilisha jambo hili yaani kuitawala dunia. Huwezi ishi kwa furaha na amani ikiwa utawala haupo mikononi mwako. Hata vita ya kiroho huhusu utawala.
Ndipo nikafikiri kuwa; Mungu alipohitaji mwanadamu kutawala ili aishi kwa furaha aliona si kazi nyepesi bila kumpa njia na namna mbalimbali za kufanya ili aweze kuitawala dunia.
Zifuatazo ndizo njia pekee alizoziona Mungu kuwa ndizo zitakazo msaidia Binadamu kuishi kwa furaha:
Karibuni kwa mjadala.

- Alimpatia miongozo, amri na sheria mbalimbali ambazo kupitia hizo basi mtu (hapa ni wewe na mimi) ataweza kuitawala dunia na maisha yake.
- Sheria za mahusiano
- Mahusiano ya mtu na Mungu
- Mahusiaono ya Mtu na Mtu
- Waheshimu wazazi wako
- Usiibe, Usiue, usizini, Usiseme uongo, Usitamani.
- Sheria za kazi
- Fanya kazi kwa siku sita
- Toa zaka sehemu ya kumi ya mapato au mazao yako
- Toa sadaka kwa wenye mahitaji na shughuli za kijamii ikiwepo Kodi, ushuru n.k
- Sheria za Mapumziko
- Siku ya sabato pumzika ukimtukuza Mungu kwa kutambua nawe uliumbwa
- Adhimisha sikukuu zilizoamriwa za kidini, kitaifa na binafsi. Binafsi ni kama sherehe za siku ya kuzaliwa rejea kitabu cha ayubu na watoto wake walioenda kufurahia kwa kaka yao mkubwa.
- Kula vyakula vilivyoagizwa kuepuka magonjwa yatakayokupotezea furaha yako. Pendelea nafaka, matunda, mboga za majani kwa wingi
- Kunywa vinywaji safi hasa hasa maji kwa wingi na Juisi za matunda.
- Mwanaume avae mavazi na mapambo yampasayo
- Mwanamke avae mavazi mapambo yampasayo
- Mtu asiuchore mwili wake iwe kwa chale au kwa Tattoo.
- Mtu asinyoe kipara, kiduku, au mitindo yoyote ya nywele
- Mwanaume asisuke
- Oa mwanamke/wanawake bikra safi umpendae/uwapendao
- Toa mahari kwap mwanamwali umuoae
- Zaa watoto idadi uipendayo
- Mpe talaka mwanamke mzinzi na muasherati
- Mpe Talaka Mwanamke mchawi, na mshirikina
- Mzaliwa wa kwanza apewe kipaombele cha urithi kwa kiwango kikubwa tofauti na wengine. Bila kujali ni wa mke wa kwanza au wa pili, Umpendaye au usiyempenda hapa kigezo ni Uzaliwa wa kwanza.
- Kila familia(wake zako) ijitegemee kwa mali na miradi ya vipato
- Mtoto wakike hana haki sawa na kijana katika suala la urithi.
- Chukua mahari umwozapo binti yako
- Zikwa katika ardhi ya Baba na babu zako. Usizikwe uhamishoni au utumwani.
- Baba ndiye kichwa cha Familia
- Mke ndiye msaidizi
- Mtoto wa kwanza wakiume ndiye kiongozi namba tatu katika familia.
- Heshimu mamlaka inayoheshimu na kusimamia sheria za Mungu katika Jamii au taifa lako.
Karibuni kwa mjadala.