Mama Salma alisema, ujenzi wa shule za sekondari umeongezeka kutoka 1,745 hadi 4,102 katika kipindi cha miaka mitano, jambo ambalo ni mafanikio makubwa, lakini kuna watu wanaojifanya kutoyaona.
Kutokana na kuongezeka kwa shule hizo, alisema idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka ambapo uandikishaji wa kidato cha kwanza hadi cha nne ulitoka kuwa wanafunzi 401,598, mwaka 2005, hadi 1,401,559 mwaka 2009.
Mimi naona angesema MAGEREZA YA WATOTO WA WAKULIMA. Nasema hivyo kwa kuwa kwa sasa mtoto wa hohehahe mkulima wa Tanzania hana namna ya kutoka tena pale kijijini kwao! Ameanza darasa la kwanza pale, sekondari pale na sasa wana high school za kata na baadhi ya kata na tarafa kama pale Kibosho wanajenga Chuo cha ufundi. Kijana anafika umri wa miaka 25 hajui kuna kabila fulani wanaishi hivi (sorry sipendi kutumia neno KABILA). Unategemea nini kama sio umemweka gerezani. Hawa vijana hawana waalimu na kama wapo ni walimu 2 au 3 na zaidi hawana ujuzi. Nilikuwa shule moja ya kata nikakuta mwalimu analia eti mwanafunzi kamkorofisha. Nilirudi pale baada ya siku 5 nikaambiwa hataki tena kufundisha na anataka uhamisho. waalimu wenyewe ni watoto ambao hata hawajui mbinu sahihi za kukabiliana na watoto (wanafunzi). Sasa hivi watoto wa wa hawa wakulima hawajui hata kuandika, wacha kusoma. tumeshuhudia kwenye TV leo eti mwalimu anawaonyesha mtihani watoto wa darasa la saba, watoto wote wanafaulu kwenda Sekondari ya kata, hajui kusoma wala kuandika unategemea nini. Hapa tunajali ELIMU BORA au BORA ELIMU? Huyu mama wala asishabikie hilo! Wala asijivunie hilo kwa sababu mzazi mwenye mwamko akijua kama tunavyojua sisi basi mumewe anaweza asiende IKULU ambacho ndicho anachoombea dua usiku na mchana. Mimi pamoja na kubanwa sana enzi za Mwalimu, watoto walikuwa wanafaulu wale kweli ambao walikuwa na uwezo na hawa walikuwa wanapelekwa shule shule mbalimbali Tanzania. Mtoto anaondoka na umri wa miaka 14 ama 15 wakati huo anakutana na msukuma, mmsai, mzigua, mdigo, mpare mzaramo nk. Anatoka Moshi baada ya kumaliza O level anajua nikienda Morogoro kuna jamaa nilikuwa naye pale KIBAHA, chain inaanzia hapo. Hawa wa sasa ukimtuma Moshi mjini anakuuliza ndo wapi huko?. SHULE ZA KATA MWALIMU SALMA SIO ZA KUJIVUNIA! CHEZA KARATA NYINGINE