Hili Ndilo Taifa La Tanzania!!!!!

Manyi

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Posts
3,253
Reaction score
605
[h=5]Kichwa kimeanza choka, ebu niwaze Taifa...

1. Taifa ambalo binti zake wakimwona Mzungu wanadhani ana hela.

2. Taifa ambalo ukiongea kiingereza unaonekana umesoma.

3. Taifa ambalo bank haikutafuti we ndo unaihonga ikukopeshe.

4. Taifa ambalo ukifeli unakuwa mtangazaji wa kipindi maalumu kabisa.

5. Taifa mbalo simu kali ni dili hata kama vocha waweka za jero jero.

6. Taifa ambalo unazaliwa umeme shida, unafika miaka 30 hata huna bajeti ya Jenereta/Solar, unailaumu tu TANESCO.

7. Taifa ambalo warembo washajiona wao ni waomba kusaidiwa daima.

8. Taifa ambalo kila mtu anataka ajue bei ya kitu ulichonunua!

9. Taifa ambalo usipoiba unaonekana ----!

10. Taifa ambalo kila mtu analalamika hana ela, mpe dili sasa, anaanza longolongo.

11. Taifa ambalo sanne lina foleni ya watu wanaenda makazini.

12. Taifa ambalo ukisema upo ofisini satatu usiku unashangawa ila upo club sanane usiku unasifiwa.

13. Taifa ambalo kusema jana nlikuwa bata sana ile mbayaaaa ni dili na waonekana mjanja.

14. Taifa ambalo bila kuigana siku haijapita.

15. Taifa ambalo kila anayehojiwa anasema "Naiomba Serikali iliangalie suala hili"

16. Taifa ambalo ukiwa na gari hutongozi unatoa tu lift kitu shaa.

17. Taifa ambalo kulipa bili yako pekeako ukaruka za wengine ni vita.

18. Taifa ambalo ikinyesha dakika 5 tu foleni masaa.

19. Taifa ambalo viongozi wanajua "hawa watazoea tu" washazoea umeme, washazoea "haijajulikana", watazoea na hii.

20. Taifa ambalo kijiMC kidonyo tu kinaweza kufariki Taifa zima likageukia Msiba.

21. Taifa ambalo kuteswa ni kunyofolewa Meno na Kucha.

22. Taifa ambalo viongozi wake wana mipasho ka taarabu.

23. Taifa ambalo vijana wameombwa wasipondee bali wasifie nchi.

24. Taifa ambalo hata bomu likilipuka Arusha, wa Mbagala anajichagulia jina la Mlipuaji.

25. Taifa ambalo, dah, nmechoka, endeleeni nyie....[/h]
 
26. Taifa ambalo Raisi wake anaishi uwanja wa ndege.
27. Taifa ambalo kijana anamalizda darasa la saba hajui kusoma na kuandika na anaenda kidato cha kwanza.
28 Taifa ambalo viongozi wake wanaamini vijana kujiunga JKT ni kudumisha uzarendo wakati waliopita JKT enzi za Nyerere ndio wanaoifisadi hii nchi.
29. Tafa ambalo kila siku yanatoka matamko lakini utekelezaji wake.
30. Taifa ambalo kila mtu anajiita mwanaharakati.
 
Taifa ambalo linaandaliwa serikai tatu.
 
Taifa ambalo kila mwaka mikoa zinaongezeka.
 

No 12 nmeipenda!
 

31.Taifa ambalo lina waziri mkuu mpumbavu
32.Taifa ambalo mgonjwa mwenye maradhi ya kichwa anafanyiwa oparesheni ya mguu na mwenye maradhi ya mguu anafanyiwa oparesheni ya kichwa
33.Taifa ambalo raisi wake hajui ni kwa nini raia wake ni masikini
34.Taifa ambalo raia wake wanakufa kwa kupigwa na vitu vya nchakali/vizito kutoka kusikojulikana
35.Taifa ambalo mwandishi wa habari akijipendeka kwa chama tawala anateuliwa kuwa DC
36.Taifa ambalo wezi wanaiba pesa benki kuu raisi anawaomba wezi wazirudishe
37.Taifa ambalo halina mtaala wa elimu
38.Taifa ambalo lina naibu wazi wa elimu asiyejua nchi yake ni muungano wa nchi zipi
39.Taifa ambalo linaviwanja vya ndege vingi lakini lina ndege mbili mbovu
40.Taifa ambalo linauza samaki wote na wananchi wake wanakula mapanki
 

Ha ha haa mkuu we acha tu, "Taifa ambalo Waziri Mkuu Mpumbavu anatoa hukumu wakati yeye si Mahakama"
 

41. Taifa ambalo kila kitu ni Liwalo na liwe.
42. Taifa ambalo mtu aliyeishia darasa la saba anafanyiwa mpango akasome Chuo Kikuu.
43. Taifa ambalo lina viongozi aina ya Lukuvi na Mwigulu.
 
44. Taifa ambalo wananchi wameahidiwa maisha bora wote, bila ya kuhimizwa, kuwezeshwa kujitegemea na kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
 
Taifa ambalo rasilimali zake kubwa akiwemo rasilimali_watu ni mali ya wawekezaji wakigeni
 
47. Taifa ambalo walimu wamekuwa mbumbu hawajui kudai haki zao,mishahara midogo,
hata kile kidogo wanachopaswa kulipwa kama haki yao mf; posho ya likizo,masomo, madaraja,madai mbalmbal hawapewi,
 
Taifa ambalo rais hajui kwa nini ni masikini na yuko bize kucheza michiriku
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1372269289.688565.jpg
    38.5 KB · Views: 337
Taifa ambalo wananchi wake hawaishi kuilamu serikali
Taifa ambalo kila mtu anataka kuwa mwanasiasa
Taifa ambalo wabunge wake ni waigizaji/wanafiki
Taifa ambalo lina baa karibu kila mtaa halafu kila siku zinajaa bado walalamika hawana hela
Taifa ambalo hata asiyesoma anataka awe na kazi ya ofisini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…