Hili ndio wazo langu la biashara nahitaji mchango wa mawazo zaidi

Hili ndio wazo langu la biashara nahitaji mchango wa mawazo zaidi

Ni wazo zuri sana lakini mboga za majani zilizokatwa katwa na containers bila shaka bei itapanda. Anyway itategemea umelenga jamii ipi na aina zipi za mboga.
Kama ukiongeza matunda ukayaweka vizuri bei ikawa reasonable it can also pay. Ukianza utapata maoni pia. Hebu zungumza pia na wauza njegere.
Thanks mkuu
 
Hapo sawa ila anyway ni wazo zuri nilikuwa na ku challenge tu ila vipi hutojisikia vibaya classmates wako wakikuona unafanya biashara hiyo?
Awali nilishtuka kidogo nilizani umekunywa VIROBA nikajiuliza lakini umevipata wapi mbona vimefungiwa haha hah hah hah kumbe ulikuwa unamchallange.
 
Mawazo ya kijinga sana hayo ila kuna mijitu ya ajabu ajabu itaiba idea yako.

Una dhalilisha elimu yako yani mimi ningekuwa rafiki yako halafu nakukuta unauza mboga aisee nakukataa mchana kweupe na siku hiyo hiyo urafiki unaisha
ww ni maskini wa mawazo
 
Vicontainer vinapatikana k.koo kuanzia 200,300 na kuendelea kwa size na shape tofauti tofauti. Kwa mboga za majani sikushauri uweke tangawizi instead tumia karoti na kitunguu tu. Its awesome kama vile kabichi ndio unaweza kuweka hoho,kitunguu maji na karoti. Kila la kheri
 
good idea ukifanikiwa kuianza tafadhali hakikisha unazingatia usafi na ubora wa bidhaa zako kumfanya mteja kwanini asinunue kwa akina mama wanaotembeza anunue kwako (hadi aweke oda )japo sijajua kama hizo mbogmboa utazilima mwenyewe au unanunua kwa watu, na mfumo wa biashara yako utakuwa special kwa kiasi gani... maana kila mtu ana strategies zake mf.mwingine anapita anaimba kwa style ya aina yake................yote kwa yote wazo zuri ila kama nakuona vile unaimba alaf unapita nyumba flaniu pale mikochen unakutana montress wa wa std V (natania)
 
If you dont know that you dont know, you are foolishh
If you know that you dont know, you are clever.

Rafiki, wewe uko kwenye hiyo ya kwanza. Fanya mpango ujitoe hapo, wakati ukuta.
Mawazo ya kijinga sana hayo ila kuna mijitu ya ajabu ajabu itaiba idea yako.

Una dhalilisha elimu yako yani mimi ningekuwa rafiki yako halafu nakukuta unauza mboga aisee nakukataa mchana kweupe na siku hiyo hiyo urafiki unaisha
 
Usitumie mifuko myeusi ile, kwanza haivutii kuwekwa mboga ambayo ni tayari kupika kwa sababu wakati mwingine unatoa rangi.

Zungumza na huyu jamaa (078) 430-3478, ni mhindi ana kiwanda cha mifuko ya nailoni. Anaweza kukuuzia ama kudesign mifuko yako transparent kwa ajili ya kuweka mboga. Ukiongea nae idea nzima atakupa pa kuanzia.

Achana na label kwanza kwa sababu inahitaji mtaji kiasi japo huyo huyo jamaa anaweza kukupa idea.

Kuna kiwanda wanatengeneza plastic containers kipo mbezi beach, kituo cha samaki. Ukiwa unatokea mwenge upande wa kushoto behind some demolished building. Uliza hapo, ukiwapata ongea nao uone kwa bei ya jumla unaweza kupata kwa sh ngapi. Ili kumaintain wateja wako unaweza encourage warudishe containers ili wapate discount, japo kuwahakikishia usafi unaweza kuwaambia wachukue mpya kila siku.

Onyo tu, nadhani containers ni ghali kuliko mfuko.

Mboga zikishakatwa kwa uzoefu wangu hazifai kuhifadhi kwa muda mrefu. Ni muhimu ukasikilizia wateja wako na kamwe usimuuzie mteja kitu kilichoharibika. Kila mteja utakaemhudumia hakikisha unachukua namba yake na kumtumia SMS mara kwa mara kuuliza kama ana order maalum.

Mwisho nikupongeze kwa kujiongeza. Ukienda Nigeria, SA na hata Kenya tu, watu wana masters zao na wanajipatia vipato kwa kujishusha na kupiga kazi.
1. Tumia mtandao kusaka wateja wako. Weka namba ya simu, weka picha. Post kwa siku mara 10 kuzidi wauza sura

2. Nunua mboga kwa wauzaji, kuna mshamba mengi tu wanalima mboga mjini. Tafuta wanaouza sokoni wanaponunulia. Uzia wateja wako bei ya sokoni ila weka chaji ya delivery ya kama tshs 1000 tu

3. Toa huduma ya mboga ngumu kuandaa. Mfano kisamvu, ukiweka na vitunguu swaumu nadhani vijana wengi wadada watafurahi kuletewa ofisini jioni

4. Mengi utajifunza kutokana na makosa. Listen to your customers. Waulize wanataka nini kila wakati utafanikiwa hadi ushangae

Mw

Mkuu nimekuelewa vizuri ila ningependa kuijuwa hiyo mifuko japo hata kwa picha na inapouzwa lakini lengo langu ni kuuza japo 100 parcked vegetables per day mkuu
 
Hahaaa kuna mahali nilisoma kwamba ukianza kueleza watu idea yako ya biashara bai ni uoga usha kuingia na kuitekeleza ni vigumu sana.
Implement Idea yako kimya kimya na acha mafanikio ndo yapige kelele na kushitua watu
 
Mawazo ya kijinga sana hayo ila kuna mijitu ya ajabu ajabu itaiba idea yako.

Una dhalilisha elimu yako yani mimi ningekuwa rafiki yako halafu nakukuta unauza mboga aisee nakukataa mchana kweupe na siku hiyo hiyo urafiki unaisha
We fala na mjinga sana so unaona kuuza mchicha sio biashara? Mawazo ua kishoga haya. Nyie ndo mnakalianawaza biashara ni kuagiza magari yakuuza au kuanza biashara ya magari.
Je angekuja na wazo la biashara ya mahari ungeponda? au hapo ndo ungeona ndo biashara?

Kuna watu ni wa kublokiwa moja wapo wewe na coment za kishoga shoga tu humu.
.Sio lazima kuchangia some time kaa kimya.
 
Habari wana jF,

Mimi ni kijana baada ya kukaa sana mtaani bila kazi ya kueleweka japokuwa nina kijielimu kangu kutoka college moja hapa mjini nimeamua kuja na wazo langu la biashara kwa ajili ya kulifanyia kazi?

Lengo la kuweka uzi huu hapa ni kwa ajili ya michango ya kimawazo katika kuliboresha wazo hilo ambalo mimi au hata mtu mwingine anaweza akalitumia na likamtowa sehemu moja na kumpeleka sehemu nyingine.

Wazo lenyewe:

Kuuza Mboga za majani.
Ukiliangalia kwa haraka inaweza likaonekana ni wazo flani hivi la kipuuzi sana. Pia inaweza isikuingie akili kama kweli muhitimu wa chuo anaweza kufanya hiyo biashara. Lakini ndio wazo ambalo mimi nimekaa na kuja nalo.

Mchakato utakavyokuwa:
Jinsi nitakavyokuwa nafanya ni rahisi sana nitakuwa na nunua mboga za majani then nazikatakata halafu nazipaki kwenye vikontena. Ndani ya kikontena kimoja kutakuwa na mboga ya majani iliyooshwa taya na kukatwa katwa pia kutakuwa na kitunguu ambacho tayari kimeshakatwakatwa na pia kutakuwa na tangawizi ambayo tayari imeshasagwa.

Nb: Kitunguu na tangawizi kila kimoja kitakuwa kimehifadhiwa peke yake then vinawekwa ndani ya kikontena cha mboga ya majani. Bei nita idetermine kwa kutumia method inayoitwa Cost based price.

Usambazaji:
Njia ya usambazi nitakuwa nasambaza mimi mwenyewe kwa njia ya kutembea nyumba hadi nyumba. Yaani kwa kifupi nitakuwa nachagua mtaa wa kudeal nao kwa siku hiyo. Kama itakuwa ni Mikocheni maana yake nitachaguwa kimtaa cha ndani ya Mikocheni na kuuza biashara yangu. Then kwenye kila sehemu ninayouza biashara yangu nitaacha mawasiliano kwa ajili ya kumpelekea bidhaa kama ikitokea siku akiihitaji.

Changamoto nizionazo mpaka sasa ni kutokujuwa gharama halisi za package za plastiki ni shillingi ngapi itakuwa vizuri kama ukiweka na picha pamoja na bei zake kama unazifahamu.

Udhalishaji.
Nimepanga kama ikiwezekana kwa kila ninapoingia sokoni kuuza biashara yangu natakiwa kwenda sokoni na vikontena mia moja na kumake sure vikontena vyote vinaisha ndani ya siku moja.

Nakaribisha mawazo ya kujenga na hata wale wa kukejeli pia nawakaribisha maana naamini yule anayekukejeli au kukusema ndio anakujenga.

Karibuni sana wakuu
Go on na Idea yako. nice idea ila kosa kubwa sana ulilo fanya ni kuleya Idea yako humu, utakatishwa tamaa make humu kuna fullu wafanyakazi yaani wao mambo kama haya ni wanaona ni ujinga na huawaambii chochote kuhusu kuajiriwa.
Unatakiwa kusonga mbele na Idea yako, na kikubwa ni commitment ukisosa commitment basi sahau kabisa kuimplement.

Time is now mkuu go on
 
Idea nzuri! Kuongezea tafuta sehemu ya permanent(sio lazima ukodi fremu) ambayo watu wengi wakitoka makazini ile jioni wanapita. Iwe open, unabandika tangazo lako fresh na mboga zilizokwisha katwa na kupakiwa kwenye vifungashio zinaonekana kwa wateja. Hakikisha mboga umezikata mchana/jioni hiyo ili zisiwe zimenyauka sana. Wateja wakishazoea kijiwe chako trust me lzm utoke!! Kuna mtu hapo juu ametolea mfano kisamvu, yes ni idea nzuri pia coz kuna mboga zina usumbufu sana kuziandaa kama kisamvu so mtu akikikuta tayar kimeandaliwa bado kupikwa tu basi chance ya kununua ni kubwa.
Kila la kheri!!
 
hongera san mkuu kuna mwanafunzi wa chuo kikuu cha mkwawa iringa anafanya hii kitu ,ananunua mboga sokoni anaikata vizuri then anaweka nyanya 1,kitunguu 1 ,karoti 1 na hoho 1 ndani ya mfuko wa mboga na anatembea kuwauzia wenzie magetoni .Niliwahi kuongea nae per day analaza faida ya buku 30 to 50 na akawa na mpango wa kuikuza zaidi biashara yake kwa kununua usafiri wa Bodaboda na kuanza kudeliver katika makazi ya watu wengine katika mitaa tofauti
 
Aisee hongera sana kwa ideal hii,anza leo ,mawazo kama haya ndo mtu huwa anapiga hela mpaka watu wanashangaa,mchangamoto zipo na utazishinda ukikomaa
 
Mboga mboga usiweke tangawizi utaongeza gharama tu.
Mboga rahisi kuuza kwenye vibobo ni kisamvu.
Wengi huwa na changamoto ya kutwanga.
Pia kama Upo Dar unaweza pia kwenda feri unanunua wale samaki wakubwa kabisa kama Kole kole, nguru jodari unawasafisha vizuri, unaenda kukatiwa vipande vingi unawagawa kwenye vikontena idadi sawa unagandisha unauza. Ila jitangaze sana.
Wale faida ipo na bei yao ni nafuu kwa sababu sio kila mteja anaweza kununua bei ya buchani
 
good idea ukifanikiwa kuianza tafadhali hakikisha unazingatia usafi na ubora wa bidhaa zako kumfanya mteja kwanini asinunue kwa akina mama wanaotembeza anunue kwako (hadi aweke oda )japo sijajua kama hizo mbogmboa utazilima mwenyewe au unanunua kwa watu, na mfumo wa biashara yako utakuwa special kwa kiasi gani... maana kila mtu ana strategies zake mf.mwingine anapita anaimba kwa style ya aina yake................yote kwa yote wazo zuri ila kama nakuona vile unaimba alaf unapita nyumba flaniu pale mikochen unakutana montress wa wa std V (natania)
hahahaha kazi nyingine ni kuweka aibu pembeni
 
Fanya kijana, tena ni safi sana. Nimeshaona nchi za nje wanafanya hivyo.

Ngoja baadae ntakuwekea picha.

Packaging unaweza kwenda Kariakoo zipo kila namna na rahisi.

Hakikisha tu mboga zako zinakuwa fresh na zinavutia unapozi-pack.

Hongera sana, ni wazo zuri sana, anza tu hata na pack mbili tatu si lazima ifikie 100 mwanzoni.
 
Back
Top Bottom