Hili ni jambo la kijinga na dhambi niliyowahi fanya ambayo naijutia sana

Matongee

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
1,056
Reaction score
2,729
Mwaka 2002 nikiwa kijana mdogo wa sekondari nilifanya jambo la kipuuzi sana na ilikuwa dhambi. Nakumbuka ilikuwa ni kipindi cha likizo ya mwezi wa 6. Kwa miaka yote 6 ya sekondari sikuwahi kusoma tuition kabisa na ilikuwa kila likizo lazima tukutane na program za kazi baba kashaziandaa. Likizo nzima ilikua kazikazi hakuna tuition. Bahati nzuri form IV na VI sikufeli.

Kwenye likizo hiyo nilipangiwa kwenda Karatu kwenye shamba la ngano kupambana na ndege aina ya kwelea kwelea. Ilikuwa sio kazi ngumu ila ni ya kushinda shamba siku nzima kufukuza kwelea kwelea. Na shamba lilikuwa na umbali mrefu toka nilipokuwa nakaa. Sasa siku moja mida kama ya saa 10 kasoro jioni nikiwa narudi maskani ndo njiani nikakuta nyumba ya mwanakijiji mmoja kuna sherehe ya harusi ya binti yao. Ikumbukwe sherehe za kijijini hasa kwa miaka ile haikuwa na mambo ya mialiko wala kadi. Wanakijiji wote ruksa kujichanganya na kusherehekea. Mimi pia kutokana na njaa plus kiu nikaona hii ni fursa adhimu sana. Na hapo nilikuwa kwenye umri wa balehe njaa kama zote halafu NO AIBU.

Bahati nzuri nilifika ndo wanataka kuanza kula. Kulikuwa hakuna ishu za bufee. Ni vijana walikuwa wanabeba sahani na kuwagawia watu waliokuwa wamekaa sehemu mbalimbali hasa chini ya miti. Mimi nilipopewa sahani yangu nikagundua wameweka kidogo sana kwa nia ya kila mtu apate japo kidogo. Akili ikanijia ya kujiunga na wale vijana wagawaji wa msosi kwa nia ambayo ilikua ovu. Nakumbuka ni sahani moja tu niligawa. Zingine kama 3 nilijigawia mwenyewe. Nikatoka hapo nimeshiba kupindukia.

Kiukweli lile lilikuwa jambo baya sana lisilokuwa tofauti na ufisadi serikalini. Mtu anajigawia pesa za umma bila aibu na kuzitafuna mwenyewe. Kwa vyovyote nilichokifanya kitakuwa kilisababisha baadhi ya wanakijiji wasipate chakula kwenye ile sherehe. Mimi natubu kila mara kwa hiyo dhambi niliyofanya miaka 22 iliyopita.
 
Mkuu badaye ulienda chuo gani na olisome kozi gani?
 
1721757912087.jpg
 
Ila wabongo tumezoea tabu na dhambi hadi tukizisoma za wazungu zinatuchekesha 😁

Mbaya zaidi uzikute za wazungu anazisimulia mbongo mwenzetu, tunaona kama anatania..

Pole mkuu Ila ulizaliwa in a wrong country. Huku kwetu watu wanajutia kuzini na ndugu, kuua, kubaka, kumchoma mtu kisu etc
 
Pika chakula ukagawe kwenye hicho kijiji, hakikisha kila mtu anapata hapo utapata amani ya nafsi.
 
Back
Top Bottom