Ww acha ujinga sasa mbona kiba kawa kimya zaid ya mwaka mzima hajatoa wimbo wowote unaanzaje kusema anashindana na mond , afu hata kiba sio wa bei Poa acha umbea.
Mwambie tu diamond kinacho mcost sasa hiv ni dharau zake ( rejea kauli zake za kuhusu tunzo za EATV ) na hizo redio sasa hiv zinasambaa sana mikoan East Africa redio wanasikilizwa mikoa mingi sasa, hivyo hivyo Efm na zingine kama ana wadharau hao lazima coverage ya nyimbo zake iwe kidogo
Japo nimependa ushauri wako 1 awe balanced kwenye media
Kiba anafanya mzik wake na huyo mond Ndiyo anaonesha ni mwenye roho mbaya na uswahili mwingi ( jiulize kwanin alitaka kumharibia kiba kwa kutoa ngoma siku moja na kiba kama ilikuwa ni kupima nani atafanya vizur majibu yamepatikana)
Ishu nyingine ukubal ukatae kuingia bifu na watoto wa kike lazima upoteee tu hao Ndiyo Mara nyingi wanasikiliza sana nyimbo zao hao wasaani na hata kwenye show Ndiyo wadau wazuri ( wanaume huwaga hatuna sana time kufuatilia nyimbo kutokana na majukumu ya kimaisha muda mwingi tupo bize ) sasa bwana mdogo tabia zake za kuwadharau hao wadada Ndiyo shida inaanzia hapo ( hao nasikia wana team zao ambazo zina nguvu sana na kwa umoja wao ni rahis kujenga ushawishi au kuharibu )
Namkubal diamond kama real fighter wa kusaka maisha lakin ukifanikiwa sio uwe jeuri na kuanza kudharau au kejeli kwa wale unaohis umewazidi na ishu ya mwisho inabid amkanyee mkewe apunguzee drama za kipuuz na majibu ya ovyo nazan wengi wanaweza kuwa wanamchukia kisa yule demu kwa kuonesha ana nyodo
Ishu ya muhimu arudi njia alizopita kujenga ushawishi mwanzon ( ishu ya bei ni haki yake kuweka bei kubwa ana team kubwa sasa akiweka bei kidogo atawezaje kuwalipa watu)
Kiufupi hawa wote ni vijana wa kitanzania mafanikio yao ni faida kwetu ila sio ubaya kuona kiba anaendelea kufanya vizur na kusema anamtegemea diamond hiyo ni kumvunjia heshima kiba ameanza kutoa hit song tokea enzi za 2005 had Leo ( rejea, cindelela, my everything n.k) kila mtu ana style yake
Sent using
Jamii Forums mobile app