Hili ni MUHIMU kulifahamu wakati wa kudate kabla ya kuingia katika ndoa.

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
8,323
Reaction score
18,051
Ni ajabu sana ya miaka hii vijana wanahisi wapo tayari kwa commitment kubwa ya ndoa kirahisi rahisi wakijua ndoa ni plug and play game kumbe bila kujua ni plug and not play until you do overhaul and rewiring then try to play.

Wakati wa kudate sio tu wakati wa kufanya ngono tu, kuigiziana character za kuwa romantic yaani unajifanya Alfonzo na yeye anakuwa Barborita au Romeo and Juliet. Then paap pete zikishavikwa mkiingia ndoani mnaanza kuona ndoa ni vita kwasababu hakuna aliyejiandaa na majukumu ya departments za Ndoani. Kinachofuata ni kusukumiana majukumu na kutegeana na kuegemeana as if mlilazimishwa kuishi pamoja kumbe tamaa zenu za kimwili na mihemuko ndivyo viliwaleta pamoja na sio work plan ya kuishi pamoja kama mke na mume kitaasisi.

Kufanya mapenzi ni sehemu ndogo sana ila muhimu ya ndoa kama uliingie ukitegemea kufanya mapenzi ndio itakuwa tiba ya migogoro na sababu ya kuelewana au kumshika mwenzako ili mambo yaende then utakausha sana maji mwilini na bado matokeo usiyaone.

Waliopo ndoani wanakiri kuwa kuna kipindi hawagusani hata miezi miwili na wanalala kitanda kimoja. Sasa wewe unayejiandaa na ndoa, kama ni binti unawazia utamshika mwanaume kwa kumpa mchezo mtamu kuna muda hatakuwa akisisimka hata kidogo tena hapo bado haujapata watoto na mwili haujakongoroka. Imagine mwili ukikongoroka itakuwaje?

Mwanaume kama unaamini show za kibabe zitakuweka salama then tafakari upya. Utapeleka moto style zote ila ukimaliza maisha ya ndoa kwa maana ya gharama zote zinakuhusu na wewe ndie CEO. Huyo unaemkaza, ukimaliza anakuwekea list ya mahitaji ukamletee na wewe ulijua ukishamkaza mtaamka nyote kutafuta ukasahau kuwa yeye anajua wewe ndie kichwa na ndio provider wa kila kitu.

So ushauri wangu kwenu, ule wakati wa kudate (vikao vya kimahusiano mkiwa wawili tu bila mtu yoyote) kaeni mkijua pale ndio muda pekee wa kuwa serious kupanga mustakabali wenu wa maisha na kuwekeana terms zote ambazo hakuna mtu mwingine atawaamulia nje yenu.

Mzungumze yanayowasibu kisaikolojia na huko mnapotoka makwenu kuna changamoto gani zimewaganda ambazo zinaweza kuwa changamoto katika kuishi pamoja.

Mjadili mpango wa mali kwa maana ya mahitaji yenu binafsi na sio binti unakuwa na mipango yako kichwani kwamba mwanaume apambane kupata mali wewe ukasomeshee wadogo zako na kuhudumia wazazi wako ambao wanaendekeza uvivu kwa kisingizio cha umri kwenda. Au unaplan kuweka mali kando wakati mwenzako anaweka mali zote mezani, huo ndio u$eng* unaowaponza mabinti wa kileo kwasababu ya kuendekeza ubinafsi na umimi kwanza mafala ninyi.

Mjadili vyanzo vingapi vya mapato mtahitaji ili kuweza kukidhi mahitaji yenu binafsi kila m'moja wenu separate, then mahitaji ya jumla, na yepi muhimu kuanza na yepi yafuate baadae.

Yapo mengi ya kupanga na hapa uzi utazidi kuwa mrefu nikiendelea kuyalist.

Niwakumbushe tu kuwa ndoa sio lelemama kwa maana ya kitu kinachojiendesha chenyewe bila msaada. Ndoa ni kama baiskeli ukiacha kunyonga inaancha kwenda.

Sasa kama mwanamke unadhania kufanya mapenzi ndio mtaji au mchango wako kwenye ndoa then jiulize kwann masingle mothers wanaongezeka kila uchao.

Na kama mwanaume unadhani ukishamkojoza demu basi unakuwa umeshamaliza majukumu yako kama kidume na mengine utamshirikisha mwanamke ili mfanye nusu kwa nusu trust me utakuja kufungua nyuzi nyingi sana za lawama kwa wanawake hapa. Mwenzako hapo anasubiria hata chupi zikiisha wewe ndie uwajibike na yupo sahihi sababu yupo chini ya himaya yako na anatakiwa kufuata lolote utakalo mwambia kama mume na kiongozi wake.

Young couples huwa mnatumia muda mwingi sana kujadili mambo ambayo kwenye ndoa ni 20% important, mnaacha 80% ambayo ndio yanakuwa ndio msingi na nguzo ya Ndoa.
 
Hongera mtoa mada, umekuja na very best analysis.

Swali moja! wewe uko ndoani?

Nilichogundua huwezi kujadili mambo ya ndoa ukiwa nje ya ndoa.

Muhimu ni kupick mambo machache ambayo unahisi yanaweza kuwork out huko mbeleni.

Najiuliza tu what kind of discussion utafanya na mchumba wako kipindi cha uchumba ili yafanye kazi ukiwa ndoani.
 
Ndoa katika kizazi hiki cha nyoka, zimekuwa ni majaribio.. watu wanaingia kwenye ndoa asubuhi mwaka mmoja wanaachana.. ndoa zimeisha kuwa upuuzi mtupu
Wanatest mitambo ila hawajui mitambo ikiwaka joto linaongezeka.
 
K

Kweli ? Je hao wazee wakiugua uzeeni nani atawaangalia kwa ridhaa zao bila malipo na mara nyingi watu kama sie wakoloni ndio tunakufa vibaya japo kubwa tunakuwa tunafamilia
Pesa jawabu la mambo yote. Kuna wazee wanafamilia wanaishi vibaya kuliko wasio na familia. Namna gani utamaliza uzeeni ni fumbo sana
 
Sawa Mzee wa Busara, ila tambua kuwa sisi vijana tunaojielewa tumeshakataa kuoa.

HATUOI ABADANI ASILANI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Ukipata mwanamke anae eleweka usichukulie poa kumuweka ndani na kudeal nae vizuri. Wanawake wanaojitambua ni hazina na wanajua nafasi yao na hatakupa headache.

Ila hawa wajuaji, unakuwa wewe ndie mwanamke sasa yeye anataka akucontroll. Si ufala huo.
 
Ndio nipo ndani.

Mambo ya msingi yatategemea mahitaji yenu binafsi na ya jumla.

Vipaumbele lazima viwekwe wazi na ubishi uwe kando. Kinacho waharibia mabinti na vijana ni ule ubishi na ulazima wa kujiamini kuwa yeye ndie sahihi kumliko mwenzake.

Unaweza kutana na mwanamke ambaye akili yake imeshikwa na mama yake ambaye anataka mtumia binti yake kama chanzo cha mapato na mdoli wa kuegemea kihisia. Binti wa hivi ukiingia nae ndoani utakuwa na mtihani wa kudeal na kivuli cha mama yake ambacho kitamfuata kila mtapokwenda.

Inabidi mkae na kukubaliana kuwa mama yake ameshakuwa mtu mzima na ni muda muafaka sasa apate mwenzake wa kumtegemea na kumpa emotional support na amuachie binti sasa afate maisha yake mapya bila kuzongwa na uwepo wake abakie tu kuwa mama mzazi sio mama shosti.

Kijana kama umezoea kupelekeana moto na mademu wapya kila siku kaa chini mzungumze hiyo changamoto na mwenzako usije mpa mitihani ya maumivu baadae.

Kwa kifupi mjadili mahitaji yenu kwa kina na namna za kuyafinance hayo mahitaji bila kutetereka na namna kama couple mtagawana vipi majukumu ys usimamizi wa vitengo mtakavyounda kwenye familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…