Imenilazimu nilete mada fupi hapa, kuhusu hili swali ambalo limenitatiza, tokea nilipoona limeandikwa magazetini.
Mimi siyo mtaalam wa haya mambo, kwa hiyo nategemea kupata mchango mahsusi toka kwa walio na upeo juu ya mambo haya.
Nchi jirani imepata matatizo ya kupungukiwa na pesa ya kigeni, (U.S. Dollar). Habari zinasema kuna baadhi ya wahitaji wa pesa hiyo imewabidi waje huku kwetu kutafuta pesa ili wakidhi mahitaji yao.
Sasa ninajiuliza, itakuwaje hilo? Hii biashara ya pesa ya kigeni inawezekana ikafanyika holela huko mitaani, na hata kuruhusu biashara hiyo nje ya mipaka?
Je, hili nalo linaweza likawa ni sehemu ya "Kuifungua Nchi"?
Ngoja nisiendelee zaidi ya hapa na kuwachosha wasomaji wa mada.