Hili suala la uhamisho kwa watumishi linashangaza sana!

Umenena, hili suala sijawahi kulielewa kabisa ...Tena ni gharama mtu hana maamuzi ya kujenga , inafika hatua familia yake iko mbali akienda kuitembelea anaingia gharama tena ...

Sijawahi kufikiria kufanya kazi nje ya mkoa wa nyumbani labda biashara ...Huu ujinga wa kutumia gharama .

Wengi walichagua mbali wakanidharau eti wanataka kuishi mbali na kwao ...Mda huu wanataka kurudi kwao uhamisho ni mtihani .
 
Mkuu, hivi utaratibu wa kuandika barua ukoje..
Halafu kama mtu anataka kumfuata mkewe ambae anafanya biashara bila kusahau watoto inakuwaje hapa
We andika tu kwenda kuungana na familia yako ...Sasa hivi watumishi kila mkoa wapo...Kila mtu apangiwe mkoani kwake sio kusumbua watu ,unapeleka watu maeneo ambayo hata wanyeji wamekimbia .
 
Binafsi nina ndugu yangu nimemjazia kwenye mfumo anavigezo vyote vilivyoainishwa kwenye hili Tangazo jipya. Kwa sasa anasubiri Approval kutoka kwa Katibu Mkuu Tamisemi.
Yaani hapo kwenye approval ndo kuna changamoto kama hujui mkuu wangu, KATIBU MKUU anaweza kukaa nayo kwenye mfumo hata kwa mwaka mzima au zaidi bado uwajibikaji kwa viongozi wetu ni 0% kabisa hawajali watu wengine bali wao wenyewe hata tangazo hili usije kushangaa limekuja kimkakati kwani hawakujua kama kuna watu wenye wenza? Tena wengine wanaomba uhamisho na vithibitisho wanavyo lakini wanasumbuliwa kila kukicha.
 
Hawajafafanua ni wenza wa namna gani....
Je, ikiwa mimi ni mtumishi nipo Dodoma na mwenza wangu ni Mkulima wa parachichi kule Mbeya, naruhusiwa kuomba kufuata?
 
Hawajafafanua ni wenza wa namna gani....
Je, ikiwa mimi ni mtumishi nipo Dodoma na mwenza wangu ni Mkulima wa parachichi kule Mbeya, naruhusiwa kuomba kufuata?
Mwenza = Spouse

Bangi addiction is real
😀
 
Kuna kitu nimekiona nimecheka sana,kuna barua zilishasainiwa na katibu mkuu tangu desemba mwaka jana ila cha ajabu zimefika mwezi wa tisa,vichekesho sasa zikifika halmashauri wanazificha,kuna mambo yanachekesha.
 
nchi ya kusadikika poleni sana lakini
 
H
Kuna kitu nimekiona nimecheka sana,kuna barua zilishasainiwa na katibu mkuu tangu desemba mwaka jana ila cha ajabu zimefika mwezi wa tisa,vichekesho sasa zikifika halmashauri wanazificha,kuna mambo yanachekesha.
Hiyo ni huzuni kiongozi wangu wala sio kichekesho, ifike mahali tuwe wakali na kila uchao tupaze sauti juu hili suala, mbona wao wakihama wanahama na familia zao? Ujue ulioa uwe na familia bora sio vinginevyo. Binafsi mke wangu uhamisho wake unasomeka kwa katibu mkuu tangu June mwanzoni! Unaweza kunambia kwamba huyu kiongozi hajawahi kuingia kwenye ankaunti yake miezi yote hiyo? Maana tulitegemea huu ni mfumo wa kidijitali mambo yawe rahisi zaidi tofauti na ilivyokuwa kwenye makaratasi lakini ndo imekuwa kinyume, inatia hasira sana. Tunajua anashughulikia mambo mengi lakini mbona tunahamisha wanafunzi kwa mfumo kirahisi sana why shubiri kwa watumishi? Kuna nia ambayo sio njema kabisa, wajirekebishe bhana.
 
Binafsi nina ndugu yangu nimemjazia kwenye mfumo anavigezo vyote vilivyoainishwa kwenye hili Tangazo jipya. Kwa sasa anasubiri Approval kutoka kwa Katibu Mkuu Tamisemi.
Nakushauri aandike upya aende kwa maboss zake watamshauri kulingana na tangazo, asibweteke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…