Hili swali huwa linanikera mno unapokutana na mtu ambaye hujaonana naye muda mrefu

Hili swali huwa linanikera mno unapokutana na mtu ambaye hujaonana naye muda mrefu

Cytochrome p450

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2019
Posts
5,638
Reaction score
15,044
Naomba nishee nanyi kuhusu hili wakuu.

Leo nilipata nafasi na kukutana na mshkaji wangu sana tuliesoma pamoja elimu ya shule ya msingi kitambo hicho.

Tukasalimiana pale kwa kuwa ni muda sana hatujaonana tangu tumalize.

Ofcoarse, kwa mshkaji ambae hamjaonana muda mrefu kuna mabadiliko ambayo kila mmoja anayaona kwa mwenzie.

Hilo likampelekea kuja kwenye swali, ama sijui niite statement ambayo mara nyingi nikiulizwa nashindwa nitoe jibu la aina gani. Nabaki nashangaa na kuchekacheka nisijue la kujibu.

Eti ananiambia:

" Kaka naona umekonda sana.. hhm! 😊 sema kitambo mzee.."

Em tushirikiane wanajamvi, viumbe wa namna hii tunawajibu vipi?!
 
Hapo kwenye akili yake anakuona wee ni beggar maskini,huna dili,umekosa connection

Wabongo wengi hasa waliofanikiwa kupata hela,kazi au mafanikio Fulani kwenye maisha huwa ni watu wanaojiona wamefanikiwa kiakili,kimwili hivyo kujiona wao ni watu wazito wanene

So huyo msela kakuona umekonda kwa sababu yeye tayari ana mafanikio Fulani,ila kihualisia kuwa na mwili mwembamba tena unajitegemea kwa kulipa kodi,hela ya kuhonga,kuhudumia familia, na unaishi maisha yako pasipo kumtegemea mtu basi wee ni mnene sana kifikra suala la mifupa na nyama lisikupe presha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nishee nanyi kuhusu hili wakuu.

Leo nilipata nafasi na kukutana na mshkaji wangu sana tuliesoma pamoja elimu ya shule ya msingi kitambo hicho.

Tukasalimiana pale kwa kuwa ni muda sana hatujaonana tangu tumalize.

Ofcoarse, kwa mshkaji ambae hamjaonana muda mrefu kuna mabadiliko ambayo kila mmoja anayaona kwa mwenzie.

Hilo likampelekea kuja kwenye swali, ama sijui niite statement ambayo mara nyingi nikiulizwa nashindwa nitoe jibu la aina gani. Nabaki nashangaa na kuchekacheka nisijue la kujibu.

Eti ananiambia:

" Kaka naona umekonda sana.. hhm! [emoji4] sema kitambo mzee.."

Em tushirikiane wanajamvi, viumbe wa namna hii tunawajibu vipi?!
We mwambie nchi nzima tunakula chakula cha taifa tangu December ni wali maharage vs ugali dagaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom