KERO Hili tatizo la mtandao hapa NSSF Ilala Boma ninaloambiwa lipo kwa zaidi ya wiki mbili sasa, ni kweli?

KERO Hili tatizo la mtandao hapa NSSF Ilala Boma ninaloambiwa lipo kwa zaidi ya wiki mbili sasa, ni kweli?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ninasubiri mafao yangu kwa mwezi mmoja na wiki mbili hadi leo bila kuyapokea.

Tarehe 5 Agosti 2026, nilifika NSSF Ilala Boma kufuatilia suala hilo, lakini nikaelezwa kuwa kuna tatizo la mtandao na nikaombwa kuendelea kusubiri. Leo, tarehe 17 Agosti 2026, nimekwenda tena kufuatilia, lakini nimepewa jibu lilelile kwamba tatizo ni mtandao.

Naomba JamiiForums mnisaidie kupata ufafanuzi kutoka kwa mamlaka husika. Je, kweli tatizo la mtandao limechukua muda wote huu? Na linatarajiwa kutatuliwa lini?
 
Back
Top Bottom