Ninasubiri mafao yangu kwa mwezi mmoja na wiki mbili hadi leo bila kuyapokea.
Tarehe 5 Agosti 2026, nilifika NSSF Ilala Boma kufuatilia suala hilo, lakini nikaelezwa kuwa kuna tatizo la mtandao na nikaombwa kuendelea kusubiri. Leo, tarehe 17 Agosti 2026, nimekwenda tena kufuatilia, lakini nimepewa jibu lilelile kwamba tatizo ni mtandao.
Naomba JamiiForums mnisaidie kupata ufafanuzi kutoka kwa mamlaka husika. Je, kweli tatizo la mtandao limechukua muda wote huu? Na linatarajiwa kutatuliwa lini?