Hima wabunge mtakaorudi 2020 himizeni FAO la kujitoa

Hima wabunge mtakaorudi 2020 himizeni FAO la kujitoa

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,784
Reaction score
6,183
Mtakubaliana na Mimi kwasasa Kuna wimbi kubwa la wafanyakazi wanaoacha kazi kutokana na maisha magumu, Miaka 6 hii itabaki kwenye kumbu umbu ya vizazi na vizazi kwa watumishi wa Umma.

Hakuna asiyejua "kichapo" kwa watumishi wa Umma na kupelekea kupoteza points zote tatu kwa miaka mitano mfululizo...

Niombe wabunge watakaochaguliwa haraka Sana warudishe mswada huo mfanyakazi aruhusiwe kuacha kazi kwa hiari yake na apewe pesa zake alizochangia kwa miaka hiyo katika mfuko wa hifadhi ya jamii.

Hoja hii ikipita ndipo tutakaposhuhudia idadi kubwa ya watu watakaoacha kazi na kwenda kufanya mishe zingine!
 
Tatizo Hawa wabunge ndo wanayapitisha hizi Sheria bungeni, wakitoka bungeni wanakuja kupinga huku nje. Hapo huwa siwaelewi kabisaaa.
 
Daah ingekua poa sana ili wengine waache kazi wakafanye yao na wanaotaka kuajiriwa waingie mzigoni, itasaidia kupunguza tatizo la ajira. Naona maisha yatakua poa sana sema tu tunalazimishana vitu ambavyo havina tija kwa maendeleo ya watu na taifa.
Wapunguze basi hata mda mfano miaka 10 au 15 hiyari mtu kuacha kazi na alipwe mafao yake mara moja.
 
Back
Top Bottom