Hints za January Makamba kuhusu mafuta na Gesi Tanzania

Twambie kwanza, mradi wa umeme wa Mwl. Nyerere utakamilika lini. Hatutaki maswala ya gesi kwani Rais Magufuli aliishatwambia kuwa huko tushapigwa.
 
Kuna wapuuzi wata like hii comment ya mchawi mwenye chuki Sana
 
Majadiliano ya mkataba wa biashara sio sawa na majadiliano ya katiba
 
Wewe una shida kichwani,ulifuatilia majadiliano ya mradi wa Bomba la mafuta la Uganda? Yameshuhudiwa na Marais mara ngapi?

Ilivyokuwa kule ndivyo na huku itakuwa.
 
Nafaham ya kwamba imekuwa ikitumika kwa matumizi ya nyumbani lkn kwa njia ya mabomba,hoja yangu ni kama imeweza kusindikwa kwenye mitungi na kutumika kwenye magari,je inashindakana nini kujazwa kwenye mitugi hii tunayotumia majumbani?
Gesi asilia ya kwenye mitungi inayouzwa Tanzania kwasasa inaitwa compressed natural gas (CNG) kwa kiswahili ges asilia iliyoshindiliwa. Huwezi pikia gesi asilia ikiwa kwenye mtungi wa CNG, pressure yake inakua kubwa mno.

Gesi asilia tunachotumia kupikia inaitwa gesi asilia ya bomba (PNG).

Huna haja ya kukandamiza gesi asilia ili uweze kuitumia kwenye jiko kwa kupikia kwasababu pressure itakua kubwa. Kama pressure yake ni kubwa Utalazimika kupunguza ili uweze kupika.

Kwa kupikia chakula kwenye majiko ya kawaida ya nyumbani, tunahitaji pressure ya 21 mbar. Na hii ndogo sana kuliko hata atmospheric pressure. Kwa hiyo utalazimika kutumia pressure regulator ili kupunguza pressure hadi 21 mbar ndipo uweze kupika.

CNG inatumika zaidi katika magari, ambayo yana pressure kati ya 200 na 250 bar.

Hivyo ikiwa utapunguza pressure ya gesi asilia kwenye silinda mpaka 21 mbar, utajaza kiasi kidogo sana cha gesi. Hivyo nishati itakayopatikana itakua ndogo sana.

Lakini kwa hiyo, kwa pressure hiyo ya 21 mbar, unaweza kupata kiasi kingi zaidi na nishati iliyohifadhiwa kwenye silinda yenye LPG.

Hivyo ili kupata nishati ya CNG ya kutosha ya kupikia, utahitaji kubadilisha silinda mara nyingi zaidi, na zitakua nzito zaidi kwa sababu ya mahitaji ya juu ya pressure.
 
Majadiliano ya mkataba wa biashara sio sawa na majadiliano ya katiba
Wewe ata nikikwambia ‘unitisation agreement’ ya mafuta na gas ni kitu gani. Hiyo terminology ndio utakuwa umeisikia hapa kwa mara ya kwanza.

Kwa ivyo sitarajii uweze ku analyse limitations za Makamba kwenye maswala ya mikataba ya mafuta kwa kumsikiliza na wala uwezi kuona mantiki ya kuanzisha mijadala ikibidi tofauti kuzungumzia different aspects za contract negotiations ya oil and gas wahusika kupata ideas.

Stick na ushambenga wa mambo ya katiba hayo yanahitaji makelele yasiyo na kichwa wala miguu ndio unayoyaweza, huku kwenye mafuta kunataka uwe na foundation ya mambo kadhaa.
 
Wewe una shida kichwani,ulifuatilia majadiliano ya mradi wa Bomba la gas? Yameshuhudiwa na Marais mara ngapi?

Ilivyokuwa kule ndivyo na huku itakuwa.
Asante dadangu ila sasa hilo bomba la gesi limetupa faida ipi wabongo kwenye upatikanaji wa Umeme wa bei Nafuu?
 
Hata ningekuwa ndio naisikia saizi,google ipo kwa Kazi gani Kwa mfano?

Narudia kukwambia majadiliano ya biashara sio sawa na majadiliano ya katiba kwamba ni public,kule msingi ni nipe nokupe..

Kama unaona timu ya majadiliano haijui wewe ndio unajua Sana omba Kazi wakuweke huko..
 
mkuu tofautisha COMPRESSION na LIQUIFICATION, ya kwenye magari ni compressed natural gas aka CNG na ya kwenye mitungi ni liquified natural gas aka LNG sasa hii LNG mchakato wake ndio complex sana.
 
Ni jambo jema,waharakishe kujenga Ili tuwapige BAO Msumbiji.
Yaani mbulukenge kama hizi zimejazwa JF kwa ajili ya kusifu na kuabudu. Hana hoja, hana knowledge wala hana skills. Rasilimali kama gesi sio ishu za kukimbiza ili umshinde Jirani yako, ukimshinda then what's next?

Mikataba ya rasilimali inatakiwa iwe shirikishi, ya kizalendo kweli kweli, ikihusisha utaalamu wa ndani kwanza, majadiliano ya kina nk. Tusirudie makosa yaliofanyika kwenye uwekezaji wa madini na nchi kupigwa mchana kweupe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…