Huyu ni rappa Ol' Dirty Bastard aka ODB akiwa amepanda stejini wakati wa tuzo za Grammy mwaka 98, ODB alivamia steji baada ya kutangazwa Puff Daddy ndio amechukua album of the year na album ya No way out wakati dunia nzima ilitegemea album bora ya hiphop wangechukua Wu Tang Clan na album yao hatari Wu Tang Forever. Alichosema ODB ni kuwa amepanda kuiambia dunia kwamba Wu wanafanya muziki kwa ajili ya watoto wanataka watoto wajifunze kupitia muziki wao.
"Please calm down, the music and everything. It's nice that I went and bought me an outfit today that costed a lot of money, you know what I mean? 'Cause I figured that Wu-Tang was gonna win. I don't know how you all see it, but when it comes to the children, Wu-Tang is for the children. We teach the children. You know what I mean? Puffy is good, but Wu-Tang is the best. Okay? I want you all to know that this is ODB, and I love you all. Peace!"
Kilichofata baada ya hapo ni bifu kati ya Bad boys na Wu tang...Wu wakapata bonge ya kiki na album yao ika double mauzo