Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi mziki hua napenda kuchana just for fun sijawahi kuwa na kipaji cha kunifikirisha niende studio
Lakini kipaji hakifi unaweza ukaendelea kutwanga japo hakuna mpunga kwenye kinu
Daaah zote hizo zilikua ni connection mkuu kwanini ulizi kacha?Mkuu wewe mkali. Ingia studio for fun. Utauza for fun. Pale Morogoro nilisoma na SQUEEZER, Getto niliishi na GODFREY TUMAINI! Baadae DSM nikaishi Camp 1 na Kali P kabla baadae kukutana na MwanaFa A level! Nafanya Hip Hop upande wa usikilizaji tu
Legend never die.. Talent never fade..Mkuu wewe mkali. Ingia studio for fun. Utauza for fun. Pale Morogoro nilisoma na SQUEEZER, Getto niliishi na GODFREY TUMAINI! Baadae DSM nikaishi Camp 1 na Kali P kabla baadae kukutana na MwanaFa A level! Nafanya Hip Hop upande wa usikilizaji tu
Hivi mnajua siku hiyo ntaziskia sauti, japo nitakua ndani ya jeneza nimenyuti/On my death bed, I see my presence on this earth get fade
I'm suprised, I was smiling, instead of being sad,
Does that make me strong and not a coward?
Remembering when I was at twenties, I had plenty,
I thought, that energy I had forever will stay
Everything was okay, never thought one day I'm gonna turn to ninety
Magonjwa ya uzee yamenishika mazee, kama yotee
Pembeni kuna kijana amevaa koti jeupe
Ananicheki kwa jicho la huruma kibabu cheupe,
Nimejichokea, namwomba Mola niache nisepe
Daktari anasema you have got 24 hours left
Say your last words before your name changed into the late
Dear God forgive me for the sins I have done,
I have done my part in this world, its Mc Cane
Hivi mnajua siku hiyo ntaziskia sauti, japo nitakua ndani ya jeneza nimenyuti/
Ntawaskia walio wema hadi mamluki, sauti ya vilio vya fitina vilivyojaa chuki/
Scars kafa kwa ngoma alipenda sana wasichana, eti ndio sababu iliyomfanya afe huyu mwana/
Tulimwambia ashike dini amkubuke bwana, akasema mnipishe acheni nile ujana/
NomaaaKwa mbali nasikia, Rika zoote wanalia
Wanajihoji huyu mshua, ni kweli amekuwa is no more
Maneno mengi mengi, kama ilivyokuwa kwa mwamba Mengi
Nikasikia sauti ya Mangi inauliza jeneza limeshapakwa rangi
Parapanda italia Parapanda, mara sijui nini we Pinda umeandaa Sanda?
Sijisikii kitu, nasikia watu, wanachangishana bukubuku
Katika kujiuliza za nini, Nikasikia rambirambia za kununua kuku
Baada ya kitambo, Nikasikia shusha taratibu
Mara michanga inarushwa juu, sauti zikasizi, nikaona kiza kikuu
Maneno yako ya mwisho yatakuwaje endapo akatokea mtu akakuwekea bastola kichwani kisha akakupa nafasi uongee maneno yako ya mwisho kabla hajakuua??
Naanza na mimi
Je nitatamani niwaombe msamaha wale wote niliowakosea kabla sijafa?, ili nikifa niende pepo yenye furaha isiyo na maafa/
Je nitajutia maamuzi yangu niliyoyafanya kipindi ambacho nina afya, au nitasizi na kukomaa kimafia?/
Au nitapiga kelele kuomba msaada kwa watu niepukane na kifo, Au kupiga dua kushirikisha malaika wamshushe kristo/
Ugekua wewe ungeweza kumsamehe hadi muuaji ambaye atayateketeza maisha yako, au roho yako itakua ngumu kufunguka kama lango la gereza la keko/
Utaweza kuyafanya hayo ili kuipata pepo uliyoaidiwa na dini yako, au utajivika ukauzu kupuuzia habari za dini na mambo ya upako/
Utakumbuka kutaja ID yako ili tukukumbuke nasisi kwa mchango wako, au hutajali utafanya mambo kibinafsi kivyako vyako?/
Je utajutia kupoteza muda wako,,,kwa watu ambao hawajawahi kuweka muda wao kwa ajiri yako??/
Utakufa ukiwa bado unakinyongo na mimi, kwa zile mada nazozipinga hapa jamvini?/
Inamaana hujawahi kufurahishwa na mimi, hata kwa zile post za utani wa vituko mitandaoni?/
Please dont let me down, nami pia ni mtu japo ngozi yangu ni brown/
.............Mwisho.......
Usisahau kuweka na yako
Mvumbo Daby
Da'Vinci
kurlzawa