Hip hop ni America tu anayebisha nani?

Hip hop ni America tu anayebisha nani?

mgonjwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2013
Posts
514
Reaction score
223
Kwa faida yenu wasanii wa hip hop bongo ni na sehemu nyingine Afrika kuna utafiti niliofanya unaonyesha hakuna msanii yoyote wa hip hop ambaye si wa America.

Amewahi ku heat na kua star dunia kama hatoki Amerika achana na hip hop fanya uanze kuimba tu na kama unafanya kwa ajili ya Tanzania pekee yake sawa lakini kuwa star kwa hip hop nje ya nchi yako sahau kabisa.

My take Fid Q, Weusi, Darasa, Roma, na wengine wote mnaofanya hip hop msitegemee kufika level za bwana Almasi a.k.a Diamond kwa hizo hip hop zenu.

Kama una ushahidi wa msanii gani ambaye anafanya hip hop katoka Afrika na kawa star nje ya Africa nitajie hapa.

Nawasilisha comment za matusi zinakaribishwa pia.
 
Attachments

  • 1408460869454.jpg
    1408460869454.jpg
    19.8 KB · Views: 423
Najuwa lengo la thread ni kupromote jina la Diamond ili ujio wa mwana Daresalame usimfunike jumla, labda tuanze kwa wewe kutueleza Diamond anapiga category ipi ya muziki?
 
Sijui ni aina gani ninachofahamu mimi anaimba na mi ni bonge la fans wa alikiba lengo si kumpaisha diamond !! P square, davido we unajua wanafanya aina gani ya music ?? Mi ninachojua wanaimba na ndo maana wapo juu sana !! Alikiba anaimba ndo maana R.kelly aliitwa kufanya colabo na wasanii wengine wote ni waimbaji walikua hamna mwana hip hop pale
 
Al jinn hamna lolote nyie mnaojifanya mnaifahamu hipo hop mnaishia ngarenaro, na unga limited basi !! Hip hop amerika bongo ni kubana pua mwanzo mwisho
 
Sijui ni aina gani ninachofahamu mimi anaimba na mi ni bonge la fans wa alikiba lengo si kumpaisha diamond !! P square, davido we unajua wanafanya aina gani ya music ?? Mi ninachojua wanaimba na ndo maana wapo juu sana !! Alikiba anaimba ndo maana R.kelly aliitwa kufanya colabo na wasanii wengine wote ni waimbaji walikua hamna mwana hip hop pale

Unampata Navio?
 
Nampata sana !! Si mganda yule jamaa kafanyaje kafa ??
 
Hip hop haiuzi-Madee
nawapa pole Tamaduni Music kwa kuamua kujiua huku wanajiona halaf usikute kuna watu kama P the Polymoth mc naye ana ndoto za kuhit internationaly ila Music wa TZ ukiwa na kipaji unakufa masikini ila wababaishaji wengi ndo wanatusua
 
Am out we ndo unamponda alikiba kua hana star look !! Embu njoo hapa unakimbia nini we mr gentleman !! Nitajie mwana hip hop gani ambaye ni star duniani kutoka tanzania
 
Am out we ndo unamponda alikiba kua hana star look !! Embu njoo hapa unakimbia nini we mr gentleman !! Nitajie mwana hip hop gani ambaye ni star duniani kutoka tanzania

Ndugu naona uu mgonjwa sana hadi kumbukumbu zinakutoka.

Umesahau kuwa Knaan yule rapper wa Kisomali alivyoshine sana mwaka 2010.
Ni strategy tu na hakuna kingine.
World entertainment ipo dominated na US na hii ni ktk vitu vyote movie, Music etc .nikimaanisha kuwa no matter msanii au actor anafanya vizuri kiasi gani ktk nchi yake kama hata ingia ktk supply chain ya US hawezi kutoka kimataifa.
 
Last edited by a moderator:
Kwani AY na diamond nani ni star kimataifa?
 
Am out we ndo unamponda alikiba kua hana star look !! Embu njoo hapa unakimbia nini we mr gentleman !! Nitajie mwana hip hop gani ambaye ni star duniani kutoka tanzania

Nitajie msanii yoyote kutoka Tanzania ambae ni star duniani?
 
mgonjwa kwa faida yako, mfano wa Mc's wa Hip Hop waliofanya vyema level za waimbaji kina Davido na Mr, Kinywa au zaidi yao ni;

1. Sarkodie
Huyu ni Hip Hop Mc toka Ghana. Ana tuzo ya BET mwaka 2012. Aliwashinda Ice Price (Hip Hop Mc toka Nigeria), Hip Hop group Camp Mulah toka Kenya, Wizkid n.k. Pia alikuwa nominated BET za 2014.

2. Ice Prince.
Huyu ana tuzo ya BET ya mwaka 2013, Aliwagaragaza 2 Face, Radio N Weasel n.k. Pia alikuwa nominated BET za 2012.
mgonjwa unaposema nje ya America hakuna Hip Hop unamaanisha nini?
NOTE: Hapa nimegusa Bara La Africa Tu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom