Hip Hop ya U.S kwa 90% imejaa matusi. Kwani Bongo tunachakujifunza kwao zaidi ya Production?

Hip Hop ya U.S kwa 90% imejaa matusi. Kwani Bongo tunachakujifunza kwao zaidi ya Production?

PHOSGENE

Member
Joined
Mar 12, 2023
Posts
12
Reaction score
7
Mziki wa Hip Hop unafungamanishwa na ugumu yaani u-hardcore, nyimbo nyingi za Hip Hop zinapewa sifa ya kuibadilisha jamii kifikra.

Lakini kwa bahati mbaya sana, wasanii wengi wa mziki wa aina ya Hip Hop hasa hasa kutoka Marekani kwa kila nyimbo wanazoimba basi zinajaa matusi ku.anzia mwanzo hadi mwisho. Wimbo hausongi bila H***s, A****le na matusi mengine mengi.


Kiukweli sielewi hata wanaosema Hip Hop ni mziki bora wanakuwa wanawaza nini. Mtu unasikiliza albamu nzima inasifia Umalaya, Bange na matusi ya nguoni na bado unadahi unapata Elimu?

Kwa bahati mbaya hata hivi vi-subparts vya Hip Hop kama Trap navyo vimebeba ujinga ule ule.

Wanazi wa Hip Hop huwa nyimbo za Hip Hop zinawaelimisha nini wakati zimejaa lugha nzito nzito?
Mifano ya wasanii wa Hip Hop ambao huwa nyimbo zao zimejaa matusi ni kama hawa Lil Wayne, Young Thug, 2Pac Shakur, Ice Cube, Jay-z, Future n.k
 
Nyimbo inaweza kuwa na ujumbe mkubwa sana
Ivo vimaneno like f*ck,a*s huwa ni vinogesho tu mkuu
 
Machaguo yako sio sahihi....
Nenda kawasikilize NAS,B.I.G,NIPSEY,DAX,TOMMY MCDONALD,KODAK,P.DIDDY,MEEK MILL,RICK ROSS,2CHAINZ Halafu uje kuedit hii post yako....
Rick Ross? Yani baada ya kumsikiliza nije kuedit hii post?
 
Hapa mkuu nakubaliana na aliye comment kuwa machaguo yako ndo yamefanya uandike hivyo.

Asilimia kubwa ya hip-hop hasa old school ya nje na ndani ya bongo zina lyrics zenye maana na ujumbe mzuri sana.

Asilimia kubwa ya nyimbo za wasanii kama Jay Z, Nas, Bone Thugs Harmony, 2Pac, nipsey hussle, logic, n.k ni dawa ya magonjwa ya akili.
 
Cursing words kama fvck, as*hole, modhafocka, bitch n.k huwa yanatumika kuelezea hisia za uzito wa anachokiimba. Hayo maneno ukitafsiri kwa kiswahili ni kama, unazingua, fala ww, danga/malaya, kudadeki, makalio ww, n.k
 
Machaguo yako sio sahihi....
Nenda kawasikilize NAS,B.I.G,NIPSEY,DAX,TOMMY MCDONALD,KODAK,P.DIDDY,MEEK MILL,RICK ROSS,2CHAINZ Halafu uje kuedit hii post yako....
mkuu nafurah sana umemuweka meek mill hapo, ingawa nae akivurugwa inakuaga kisanga sana.
 
Kitu pekee cha kuiga kwa rappers wa marekani ni flow style na production, pia marketing strategy zao na userious wao kwenye game
 
Ingia YouTube, search "Joyner Lucas songs". Sikiliza moja baada ya nyingine. Usiache kuichek "i'm not racist" pamoja na "Frozen"

Niko hapa nakusubiri urudi tujadili mada yako.
 
Ndo maana inaitwa muziki wa shetani nadhani umeelewa.

Lengo kuu la hip hop ni kuharibu jamii kwa kupromote:
1. Ushoga,
2. Uzinzi,
3. Ulevi,
4. Vurugu,
5. Ugomvi,
6. Matusi,
7. Starehe, anasa, na maisha bandia.

Huwezi penya kwenye hip-hop industry bila kuuza nafsi yako.
Kuuza nafsi yako kwa shetani kunamaanisha ni kujenga hali ya kushinda-kushinda kati yako na shetani. Shetani anakupa pesa kwa kukufanya kuwa maarufu, yeye ananufaika kwa wewe kuibomoa jamii kupitia nyimbo na video zako ambapo mashabiki zako ndio waumini wataiga kile unachoimba au ulichoshuti.
 
KILA wimbo wa harmonize ni lazima uanze na kupromote kuvuta bhangi.
Lazima usikie sauti ya kukooa bangi, ni the same, hapa ni watoto wadogo wanapromotiwa kuvuta bangi
 
Huwezi penya muziki industry bila kuuza nafsi yako.
USA pana underground wengi sana shida kupenya
 
Back
Top Bottom