Mfano crdb wametangaza hisa zao je nikinunua nafaidikaje nazooo?
CRDB waliuza hisa zao kwa mara ya kwanza miaka kadhaa imepita (IPO)
Na zimekuwa zikiuzwa ktk soko la hisa la Dar es salaam.
Wanachofanya saiv ni kuongeza mtaji tena, hivyo wanauza tena kwa mara ya pili ,lakin safari hii hawauzi kwa watu wote wanauza tu kwa wanahisa ambao tayari wana hisa za CRDB (inaitwa Right issue au Hisa stahili)
So kama unataka hisa za crdb au kampuni yeyete iliyopo ktk soko la hisa la Dar es salaam inabd ununue kupitia madalali (brokers) wa soko hilo ambao ni makampuni 8 yaliyosajiliwa na DSE na kusimamiwa na CMSA (capital market and securities authority)
Faida za kumiliki hisa.
1.Gawio: Kampuni zinafanya biashara, mfn hyo CRDB faida yake itakayo ingiza kwa mwaka,kuna ambayo itagawiwa kwa kila mwanahisa kutokana na hisa anazomiliki
2.Kuongezeka kwa thaman ya uwekezaji : hela utayonunulia leo hisa za CRDB si hela utakayo uza mwakan au hata baada ya miaka mitano tuseme, kwa kadri CRDB itavyozid kufanya vzur katika soko na kuzid kupata faida na kukua kila siku, na hisa zako zitazid kukua kila siku.
Mfano unaweza nunua leo hisa kwa kila kipande kwa sh 300 au 500 lakin baada ya miaka kadhaa ukakuta ile thaman imekuwa maradufu had 5000 au 10000 kwa kila hisa. Kwa kadri kampuni inavyoperform
Angalizo: kampuni inaweza kufanya vibaya pia na kufilisika na ukapoteza pesa zako.
3.Kuwa na haki ya kuhudhuria mikutno na kupiga kura juu ya maamuz ya namna ya kuendesha kampuni.
Kwa mfano huo wa CRDB ni kuwa Utahudhuria mikutano muhim kama ile AGM na kupiga kura au kuamua namna ambavyo kampuni itafanya mambo kadha wa kadhaa kwa mwaka husika.
4.Cheti cha Hisa hutumika kama dhamana ktk mabank na wakopeshaji wengine ktk kuombea mkopo.
5.Hisa zinagawanyika: Tofaut ya uwekezaj wa hisa na uwekezaji wa vitu vingine kama Nyumba au mashamba ni kuwa ukihitaj hela ,kama ni shamba utalazimika kuuza lote au nyumba yote hata kama pesa unayohitaj ni nusu tu ya ile ya investment yako,lakin hisa zinagawika, unaweza uza kias kidogo tu ukapata tu unachohitaj. ukihitaj Tsh million 20 na unanyumba ya million 30 mara nyingi utalazimika kuuza nyumba yote ili upate hyo hela,
Lakin kama ni hisa unazo hizo za million 30 na unahitaji 20M utajiuzia tu hizo hisa za 20M million na ukajibakizia za 10M
6.Uwekezaji wa hisa ni rahis unaweza kuanza na kiwango chochote kile kuanzia Tsh 10,000 had Mabillion.