mtoto mpole
JF-Expert Member
- Mar 22, 2010
- 678
- 148
Faida ya hisa ni nini?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mfano crdb wametangaza hisa zao je nikinunua nafaidikaje nazooo?
Shukran kwa wadau wote, mwanzisha mada/hoja, wachangia hoja na kuuliza kwa niaba ya wengne
Naomba kufahamu masuala yafuatayo:
Moja, mfano, ikitokea mwenye hisa amefariki, je hisa zake zitarithiwa na mtoto/ndugu yake?
Pili, ukishamiliki hisa ktk kampun fulan, je inakuwa moja kwa moja mpk mwisho wa maisha yako au mpk pale unapoamua kujitoa?
Mwisho, je kampun ikifilisika na kufa, je wanahisa wanafidiwa vp na wkt kampun ipo hoi kiuchumi?
Naomba kuwasilisha wadau
Mkuu
Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni.
Mtaji wa kampuni huwa unagawanywa katika vipande au visehemu vilivyo sawa, na hivyo visehemu ndo vinavyoitwa hisa.
Mfano:- wewe na rafiki zako watatu mkiamua kuchanga Tsh 2M kila mtu ili muanzishe biashara ya duka, ina maana jumla ya mtaji wenu itakuwa ni Tsh 6M
Kwa lugha nyingine itakuwa ni sawa na kusema kila mtu anamiliki asilimia 25% ya kampuni.
Sasa inaweza fika kipindi mmoja wenu anataka kujitoa, au kuna mtu mwingine anataka kuingia, mtafanyaje fanyaje ili aingie au atoke bila kuharibu hesabu zilizopo za mtaji wenu?
Ndo hapo ambapo wataalam walikuja na hii dhana ya Hisa kwamba, Mtaji ule wenu jumla yake yaan Tsh 6M zinagawanywa ktk vipande vilivyo sawa, lets say vipandw vya 6000 vilivyo sawa ambapo kwa mfano wetu huo kila kipande kitakuwa na thaman ya Tsh 1000.
sasa hapo utagundua kuwa kila mmoja wenu ktk wale watatu akogawanya hela alotoa ile 2M kwa thaman ya kila kipande (Hisa) itakuwa sawa na kusema kila mtu anamiliki hisa 2000.
na ndo hapo inapokuja kuwa rahis kumuuzia yeyote yule sababu unakuwa unajua unamiliki nini, na kina thaman gan? Unaweza tu kuamua kuniuzia hisa zako 500 we ukabakiwa na 1500 na maisha yakaendelea bila kuvuruga mahesabu ya kampuni.
Hizo issue ni kama kamali so kuna kula na kupuswa.. so take care. Design kama una bet niko na 8m nahitaji kuziweka mahali zinizalishie hata kwa one year lakini sio kwenye hisa...any idea nipeleke wapi?
niko na 8m nahitaji kuziweka mahali zinizalishie hata kwa one year lakini sio kwenye hisa...any idea nipeleke wapi?