Lugha iliyotumika katika kujibu swali la kushuka kwa hisa, inafanya mtu wa kawaida kuwa mwoga sana wa kununua HISA. Sababu unajiuliza maswali kama 2nd quarter ilikuwa na faida zaidi ya 1st quarter inakuwaje HISA zishuke thamani sababu tu zimeingia sokoni?
Au better yet, ikiwa kampuni imesha amua HISA 500 ndio zitakuwa kwa wale ambao ni wanunua HISA si inatakiwa ziendelee kupanda/kushuka tokana na kupanda/kushuka kwa thamani ya kampuni yenyewe?
Samahani, ni mchanga kabisa katika sekta hii, na hivi nimepata mtu wa kunielewesha naona nibanane nawewe unipe darasa.
CC: Wakuu
TUKUTUKU,
Bulesi,
burden,
Madewa,
Prisoner 46664,
KIBANGA Ampiga Mkoloni na wengine wengi mnaweza mkawa msaada kwa mada hii kama hamtajali. Tunaomba darasa.
Salaam
AshaDii,...hope all is well...
Nitachangia kidogo...
Kwanza kabisa, huku nikiheshimu jibu la mkuu
TUKUTUKU hapo,,ningependa pia kusema kuwa hisa, zikiwa kama sehemu ya umiliki wa kampuni, soko lake ni kama la bidhaa nyingine yeyote..mtu atakubaliana na mimi kuwa kuna sababu zaidi ya moja inayoweza kupelekea kupanda au kushuka kwa bei ya bidhaa fulani sokoni wakati fulani. Inaweza kuwa ni sababu ya kupungua/kufurika kwa bidhaa husika sokoni, kuwepo kwa bidhaa shindani bora zaidi, hisia ya wateja kuhusu kukosekana kwa bidhaa hiyo hapo baadaye na hivyo kutaka kununua kiasi kikubwa leo na kadhalika....
Primarily, alichokisema
TUKUTUKU kwamba bei ya hisa sokoni inakuwa determined solely na
demand vs supply ya hisa at a time ni kweli kabisa. Lakini je, ni nini kinachopelekea mtu kutaka kuuza au kununua hizo hisa na hivyo kuathiri kiasi hicho cha demand/supply ya hisa sokoni at a time? Sababu ni nyingi..mfano:
1) Current company profits - Kuna watu wanaodhani kuwa kampuni ikipata faida kubwa mwaka huu kuliko uliopita basi itakuwa inafanya vizuri na hivyo wanaamua kuwa sehemu ya wamiliki na hivyo kutaka kununua hisa zake. Hata hivyo faida ya sasa ya kampuni inaweza isiwe kipimo tosha cha uzuri au ubaya wa kampuni. Mfano, kwenye hii case ya CRDB, inawezekana faida yake kubwa imetokana na vyanzo visivyoweza kujirudia mwakani (one - off transactions) kama kuuzwa kwa baadhi ya assets zake n.k..mwekezaji anapoona kuwa kampuni imeshindwa kutengeneza faida kwenye ile biashara yake kuu, basi ataona kuwa uwezo wa kampuni kutengeneza faida utakuwa mdogo pia huko miaka ya mbele na hivyo kutaka kuuza hisa zake.
2) Company prospects/Investment plans (Mipango endelevu) - Kampuni inaweza kutengeneza faida nzuri leo, lakini kwa kulinganisha mipango mikakati yake ya muda mrefu, faida yake haitaongezeka kwa kasi kama ile ya washindani wake wa karibu. Kwa matarajio ya kupata faida zaidi baadaye, mwekezaji anaweza kuamua kuuza hisa zake na kununua za kampuni nyingine yenye mipango yenye faida zaidi huko mbeleni.
3) Decline in company's market share - Wawekezaji siku zote hutaka kuweka pesa zao pale ambapo wanahisi zitakuwa na faida kubwa zaidi. Kampuni inaweza kuwa imepata faida leo, lakini ukubwa/umahiri wake kwenye soko lake la bidhaa ukawa unapungua taratibu. Hivyo wawekezaji wataona uwezekano wa kutengeneza faida zaidi ikiwa watawekeza kwenye hiyo kampuni nyingine inayoonyesha ukuaji wa soko lake la bidhaa ingawa hapa walipowekeza sasa kumepatikana faida pia.
4) Temporary buyers/sellers - Masoko ya hisa duniani kote siku hizi yametawaliwa na watu wanaotaka kununua hisa na kukaa nazo kwa muda mfupi tu mpaka hapo bei itakapopanda kidogo ili wauze wapate faida, halafu wanunue nyingine na kuuza tena kwa mtindo huo huo. Hii inaweza kuwa kweli kwa case ya CRDB pia. Kwamba hawa wawekezaji waliopeleka sokoni walikuwa wanasubiria kampuni itangaze gawio la faida kwa mwaka (dividends), wachukue faida yao halafu wauze hisa zao na kupeleka sehemu nyingine. Utashangaa kuwa kuna watu huwa wanawekeza ada za shule za watoto wao kwenye hisa na wakati wa kulipa ada ukifika inabidi tu wauze ili walipe ada..no matter what!
5) Wawekezaji kulipa mikopo - hii hutokea mara nyingi wakati kampuni nzuri ikiingiza hisa zake sokoni kwa mara ya kwanza. Wawekezaji huweza kuchukua mikopo benki, kununua hisa na kukaa nazo, na kuziuza pindi bei inapopanda sokoni (au wakati wowote muda wa kurejesha mikopo hiyo benki unapofika, bila kujali bei ya hisa sokoni wakati huo!)
6) Speculative buyers (wanunuzi watabiri) - Hawa ndio wameshamiri kwenye masoko ya hisa duniani kote, na ndio chanzo kikuu cha financial crisis iliyoikumba Marekani miaka ya juzi. Ni kwamba badala ya watu kununua hisa za kampuni kwa sababu ya uwezo wake wa uzalishaji wa sasa hivi, ununuzi wa hisa unakuwa umeegemea zaidi kwenye yatakayotokea kwenye kampuni miaka hata 20 au 100 ijayo. Kunakuwa na watu wapiga debe, wanaochimba (au kupika) habari za mipango ya kampuni (au ya serikali, itakayoneemesha mapato ya kampuni) hata miaka 10 huko inayokuja. Kwa hivyo basi watu hawa kwa maneno yao wanaishia kusababisha bei ya hisa kuongezeka ama kupungua...
kwa hivyo kwa kujibu swali lako dada Ashadii, kutokana na kuwepo hasa hasa kwa wanunuzi/wauzaji wa hisa wa category namba sita (6) hapo juu, mara nyingi bei ya hisa sokoni haiendani moja kwa moja na ubora wa kampuni kwenye kuzalisha fedha kwa sasa. Kifupi kuna mambo meengi tu yanayoweza kufanya prospective investors wakaongeza ama kupunguza imani yao kwa kampuni fulani. Ndiyo maana unaweza kuona wakati mtu kama Steve Jobs alipokuwa anakaribia kujiuzulu kama Apple CEO ilibidi kufanyike marketing campaign ya kutosha ku-restore investor confidence na kuwadhihirishia watu kuwa kampuni itaendelea kuwa kwenye mikono salama, itaendelea kupata faida, na hivyo watu hawana haja ya kuuza hisa zao kwa hofu ya kupata hasara huko mbeleni.
In a nutshell, the best way to buy or sell shares is to just act like a smart layman, huhitaji technicalities nyiingi kuhusu sijui faida ama hasara ya kampuni leo, earnings per share, etc...angalia mifano ya maswali anayotakiwa kujiuliza layman hapa:
(a) Twiga/Simba Cement zinazalisha cement? Je cement itaendelea kuwa bidhaa inayohitajika na watu wengi? Je demand yake ni kubwa? Je bidhaa za kampuni zina ushindani mkubwa sokoni? Je kampuni ina uongozi mzuri? kama majibu ni ndiyo badi nunua hisa..lakini mwaka 2014 ukishasikia Dangote Cement imeanza kuzalisha cement kule mtwara kwa kiwango kinachotosheleza demand ya Afrika Mashariki yote,,,you should know it is a sign that Twiga's share of the cement market is about to decline and..may be, may be you need to sell your shares!
(b) Hisa za Precision Air...ilikuwa ni sahihi kabisa kwa watu kununua hisa za Precision Air wakati ambapo kampuni ilikuwa inaoperate kama monopoly, bila mshindani. Hii ni kwa sababu lazima kampuni ingetengeneza pesa tu, iwe isiwe (walau ikiwa na uongozi makini kidogo). Lakini je, baada ya kuja kwa fast jet, Precision ina uwezo wa kuendelea kutengeneza pesa?Je ina uwezo/mipango gani ya kupambana na hii bei ndogo ya mshindani wake ilhali wote tunajua wateja wanavyopenda kulipa gharama ndogo kuliko kubwa?..haya ni maamuzi ambayo yanaweza kufanywa na a smart layman...trust me,hayo ni muhimu kuliko expert advice...