Hisa za kampuni ipi zipo sokoni!?

Hisa za kampuni ipi zipo sokoni!?

rodrigaz

Senior Member
Joined
Jan 4, 2015
Posts
185
Reaction score
199
Habarini wanajamvi, ningependa kufahamu ni hisa za kampuni gani ambazo zipo sokoni kwa sasa na zinauzwa!? Binafsi ningependa kununua hisa katika moja ya makampuni hayo!
 
ImageUploadedByJamiiForums1421359811.995143.jpg

Kwa maelezo zaidi Ingia kwenye website ya DSE link chini hapo

http://dse.co.tz/content/listed-companies
 
Mimi nauza hisa za kampuni ya Mwananchi Co. Ltd ni pm tuongee
 
Habarini wanajamvi, ningependa kufahamu ni hisa za kampuni gani ambazo zipo sokoni kwa sasa na zinauzwa!? Binafsi ningependa kununua hisa katika moja ya makampuni hayo!

Nunua hisa za swissport mkuu hutajuta.Achana na hizo za mwananchi/NMG utaingia choo cha kike.Sio kila kampuni iliyopo DSE ni ya kununua hisa zake.Epuka mkombozi bank,Precision air,Kenya airways,Swala na Uchumi supermarket(kwa sasa).
 
Ndugu nachukulia una ujuzi kwenye haya mambo kwa upande wangu nimekua na shahuku sana kuwekeza katika masoko ya kifedha kama la hisa. Ila sijui njia ya kupita kuna kanuni labda inayotumika kufanikisha uwekezaji mzuri. Na vipi kuhusu mifuko kama UTT?
 
Nunua hisa za bank za hapa nchini mfano CRDB,DCB,NMB kwani kufirisika kwake si rahisi, ila kama una pesa za kutosha nunua TBL au TCC na ziko juu sana mfano TBL inafikia 14,ooo/ kwa hisa ndhani itakua imeshapanda kwa sasa. TCC ni 16,000/ kwa hisa moja nadhani nayo itakua imepanda kidogo.
Vilevile unaweza ongezea kwa kampuni nyingine zinachipukia na ni bei rahisi kidogo ukilinganisha na haya makampuni makubwa.
Vilevile unaweza kununua hisa za campuni za cement za Tanga na Dar ambazo nazo zinafanya vizuri
kwa ufupi tmbelea web ya DSE Tanzania kwa maelezo zaidi
 
Back
Top Bottom