Hisa za Kampuni ya kuchimba gas (Swala Tanzania)

hizo hisa huwa wanatangaza au hadhalani au wanautaratibu upi
 
Kwa kawaida utaratibu wa kuuza hisa za makampuni kwa mara ya kwanza(IPO) hutangazwa kwenye vyombo vya habari,mara zote hutoa muda wa mauzo ambao huwa ni mwezi mmoja hivi. Wakiishafunga mauzo ya awali kila aliyenunua hizo hisa anakuwa na umiliki wa sehemu ya hiyo kampuni kulingana na hisa alizolipia.Kiwango gani mtu ananunua inategemea na mtu binafsi, ni kwa kiasi gani yuko tayari kama mjasiliamali kuwekeza pesa yake pamoja na athali za kukosa ambozo zipo wakati wote katika biashara yoyote ile. Baada ya mauzo ya awali hisa za hiyo kampuni hu-orodheshwa katika soko la hisa,na hapa ndipo aliyewekeza ana uhuru wa kuendelea kuzishikilia hizo hisa kwa kungoja gawio au kuziuza kwa faida. Chukulia mfano wa swala: Hisa moja iliuzwa kwa shs 500... Kama uliamua kununua hisa 10000 maana yake(shs 500*10000=shs5000000)
Hivi sasa ziko sokoni kwa bei kati ya shs 600-700...tuchukulie kuwa unaweza kupata mnunuzi kwa sh 650@ maana
utatengeneza(shs 650*10000=shs6500000) hapa una faida ya shs 1500000 katika kipindi cha mwezi mmoja na hii
ina maana kuwa uwekezaji wako umetengeneza faida ya 30% ambayo unaweza kuiacha ikiwe ukingoje gawio tena au kuchukua pesa yako na kuachana na swala ili kuwekeza kwingine.Nafikiri Maluyaga Ikohi mtakuwa mmeelewa.
 
hiyo hisa nikinunua mimi ninafaidika vipi mdau

unakuwa mmiliki wa kampuni. kila mwisho wa mwaka ambapo kampuni hutangaza faida, na wewe utamegewa sehemu ya faida (gawio) kama mmiliki kulingana na kiasi cha hisa ulizo nazo. fikiria, kwa mfano una hisa 100 na kisha kampuni ikatangaza kiasi cha gawio kwa kila hisa ni TZS 15, kwa hiyo utapata faida ya TZS 15 x hisa 100 = TZS 1500.

faida nyingine ni pale thamani ya kampuni inapopanda. hapo unaeza ukaamua kuuza hisa zako (kama kuna wanunuzi). tuseme umenunua hisa 1000 kwa TZS 500 kila moja (chukulia mfano wa SWALA sasa) halafu baadae hisa zikapanda bei mpaka TZS 2000 kila moja; unaeza ukaamua kuuza hisa zote au sehemu yake. utapata faida. kuna watu wanacheza na masoko ya hisa kwa mtindo huo, hasa nchi zilizoendelea.

lakini wewe kama mmiliki wa kampuni, kampuni ikipata hasara na wewe utapata hasara. kwa hiyo kampuni ikitangaza hasara hutopata gawio, ila bei ya hisa kweye soko itayumba kwa kuwa watu hawatoiamini kampuni. utaendelea kumiliki hisa zisizo na faida, na hata ukiuza utakuwa na hasara tu. chukulia mfano wa NICOL na Precision Air. Pitia pia kwenye tovuti ya Dar es Salaam Stock Exchange uone makampuni yanayofanya vizuri na vibaya kwenye soko ndipo uamue utanunua wapi. na pia fuatilia biashara za hizo kampuni ili ujue kama zina faida.

natumaini nimejaribu kujibu swali lako.
 
they way I see Tanzania, sidhani kama kuwekeza kwenye his a kunalipa sana. may be kama una capital kubwa. but kama capital yako ni ndogo heri uwekeze kwenye mobile banking.
ni mawazo tu jaman.
 
mm naomba unisaidie namna ya kununua hisa na nini faida yake kwangu yaani kwa ufupi mambo yahusuyo hisa nami niweze kujiunga nao au ninunue hizo hisa
 
Unatakiwa kufutatilia mwenendo wa makampuni yote yaliyosajiliwa na DSE.

-Kila kampuni lina 'minimum shares' ambazo wateja wake watatakiwa kununua...mf. Kampuni ya sigara, TCC wanaweza kuuza kuanzia hisa mia moja '100 shares' nakuendelea, which means unaweza kununua hisa 100--- kutokana na uwezo wako.

-Kila kampuni lina bei za hisa zake kutokana na reputation au jinsi linavyofanya biashara. Kwa mf. hisa moja ya TCC yaweza kuuzwa kwa sh. 2500, kama unataka kununua hisa mia moja then unatakiwa kuzidisha mara 2500 (2500*100 =250,000), hivyo basi kwa hisa mia moja utatakiwa kuwa na sh. 250, 000 ili kumiliki sehemu ya kampuni.

-Unachotakiwa kufanya ni kufuatilia mwenendo wa kampuni yako kila siku ili kujua je bei ya hisa imeongezeka au imepungua, unaeza kuuza hisa zako mda wowote kama ukiona inakupa faida. Mf. kama ulinunua hisa moja kwa sh. 2500 then umeona bei kidogo imepanda hadi sh. 2700 unaweza kuuza hisa zako kwa faida ya sh. 200 kwa kila hisa (2700*100 =270,000). Kwa hiyo utapata faida ya sh. 20, 000. "The more shares you own, the more profit you make".

-Kama hutaki kuuza hisa zako, utasubiri kwa kipindi kilichowekwa na kampuni kwa ajili ya kugawana faida ''dividends'', mara nyingi ni miezi mitatu au miezi sita.
-Wengi wanasema ni vizuri kununua hisa za makampuni yanayouza kwa viwango vya chini coz utanunua hisa nyingi kwa bei ya chini kidogo. kwa mf. kama Swala Gas wanauza hisa moja kwa sh. 500 unaweza kununua hisa mia tano (500) kwa sh. 250,000, tofauti na kununua hisa za TCC ambazo kwa hiyo tsh. 250,000 utapata hisa moa moja tu. Labda wataalam watujuze kitaalam zaidi.
Bestito ladyfurahia twende kununua hisa.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru kwa kunifahamisha na kunielezea kiundani zaidi maana nilikuwa sijui bestito umenifumbua macho oky acha niwekeze hela na niangalie ni kampuni gani naweza nunua ihizo hisa kwa mwaka huu maana nimeona kama hiyo inalipa zaidi asante rafiki kwa kunielewesha suala hilio kweli jf ni zaidi ya kuchat hata mambo mazuri tunayapata hapa asante nitakuutalifu lini twende bestito kama uko dar
 
Kwa nini asinunue za Swala?

Jamaa hata exploration hawajafanya wamefanya kitu kinachoitwa seisemic ambayo hii does not prove kuwa kuna kitu chini,fautalia company inaitwa petrobas utajua zaidi
 
Jamaa hata exploration hawajafanya wamefanya kitu kinachoitwa seisemic ambayo hii does not prove kuwa kuna kitu chini,fautalia company inaitwa petrobas utajua zaidi

Umeongea point nzuri mkuu, lakini hembu mueleweshe ili ajue kwa undani. Kuna kampuni moja sikumbuki kama ni DAHACO, watu walilia miaka ya mwanzoni mwa 2000.
 
Usijali nipo nimejaa tele.
Wekeza afu utaona matunda yake..
 
asante ngoja nijaribu ushauri wako maana naona ni mzuri sana
itabidi nipunguze kununua nguo niwekeze huko yaelekea kuna amavuno mazuri asante sana my dia
Usijali nipo nimejaa tele.
Wekeza afu utaona matunda yake..
 
Umeongea point nzuri mkuu, lakini hembu mueleweshe ili ajue kwa undani. Kuna kampuni moja sikumbuki kama ni DAHACO, watu walilia miaka ya mwanzoni mwa 2000.

Sio dahaco, ni nicol. Dahaco ilibadili jina ikaitwa swissport na ni moja ya makampuni yanayofanya vizuri dse
 
they way I see Tanzania, sidhani kama kuwekeza kwenye his a kunalipa sana. may be kama una capital kubwa. but kama capital yako ni ndogo heri uwekeze kwenye mobile banking.
ni mawazo tu jaman.

Mobile banking! How mkuu?
 
mm naomba unisaidie namna ya kununua hisa na nini faida yake kwangu yaani kwa ufupi mambo yahusuyo hisa nami niweze kujiunga nao au ninunue hizo hisa

Unanunua kupitia ma broker....unakuwa kama unaweka order ikitokea mtu anauza hisa ktk kutoka kampuni utakayo wewe e.g. Swala basi wanunua kwaniaba yako.
 
Kwanini mkuu?

Siwezi andika hapa yote kwani it need more explanation to understand but believe me swala energy will never make on this,cost ya kukodi drill ship per day ni 1.2Milion USD ambapo hii ni kwa ajili ya exploration but swala hawajafanya hii kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…