Ndugu Nalo neno,Hapo ndipo unapokuja kwenye kiini cha kufanya biashara katika soko la hisa.kumbuka anayeshikilia hisa anafahamu ni thamani gani hisa za swala katika industry ya gesi na mafuta inaweza kufika,kama ana taarifa zinazomfanya aamini kuwa thamani ya swala inaweza kupanda zaidi hadi tuseme 2000tsh kwa hisa basi hatauza hisa zake bali ataendelea kuzishikilia, labda wewe unayezitaka uweke dau la tuseme 2500 kwa hisa. Kwako wewe unayezitaka hizo hisa za swala unatakiwa uwe na taarifa muhimu za kampuni hiyo na mwelekeo wake katika hiyo industry, ukiwa na silka ya ujasiliamali basi nenda soko la hisa weka bei yako ya kununulia hisa za swala kwa mfano 800tsh kwa kila hisa, inawezekana wanaozishikilia wakavutwa na bei yako na kukuuzia kiasi walichonacho,kwa maana hiyo basi kadili watu wanavyoshindana kuweka madau bei yake inazidi kupanda.Vinginevyo wale wanaozishikilia wanaweza kuamua kupanga bei hata zaidi ya hiyo iliyoko DSE.nafikiri nimekujibu.