mkuu zakumi,
si kweli kuwa kutafakari kwa kina hakufundishiki. kusingekuwapo na masomo haya ya critical thinking, au logic katika falsafa. kuna namna mtu anajengwa kujihoji, kuhoji na kutafakari kauli, matendo, mambo, vitu kwa kina na umakini.
kutafakari kwa kina kunafundishwa na wapo wataalam katika fani hizo. na critical thinking kama masomo mengine yanaweza yakarahisishwa katika level ya primary na kuendelea kuboreshwa kwa kadri madarasa yanavyopanda juu.
kuhusu suala la pili la wafrika kujenga shule lakini haitupi manufaa si kwamba shule tulizonazo hazitusadii kabisa ila haziboreshwi kukidhi mahitaji yetu, na bado zinatujenga kuwa tegemezi kwa maaana ya kuajiriwa na sio kuelimika kwa asilimia 100. mf engineering ya kibongo ni kufanya maintainance sio kutengeneza vitu vipya, sasa kama tunajengwa kufanya maintanance je sio bado tunatayarishwa kupokea vya kutoka majuu ili sisi tuje kuvitengeneza vinapoharibika.
hawa wanaotengeneza mitaala wakitengenezewa mitaala bila kuingalalia mara mbilimbili ndio tunaishia hapa tulipo, wazungu hawapendi kabisa sisi tufunguke kiakili wanajua tukifanya hivyo habari kwao itakuwa imekwisha maana ujinge wetu kwao ni utajiri. ni jukumu letu kuetengeneza mitaala inayotufaa na kutusaidia kuwa na maendeleo.