Hisabati na Tarakimu

Hisabati na Tarakimu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Hisabati na Tarakimu
Msamiati wa hesabu/hisabati unaangazia: majina mbalimbali ya tarakimu/nambari; kuandika tarakimu kwa herufi.maneno; tarakimu za kiarabu; akisami (fractions) na asilimia (percentages).
Tumekuandalia:
  1. Nambari za Kimsingi (0-9) Kiswahili na Kiarabu
  2. Kumi na (11-19) Kiswahili na Kiarabu
  3. Makumi/Ukumi (10-90)
  4. Akisami (fractions)
  5. Mifano Kadhaa
NAMBARI ZA KIMSINGI
Haya ni majina ya tarakimu mbalimbali zinapoandikwa kwa herufi (badala ya nambari) yenye asili ya Kiswahili/Kibantu na pia yale yenye asili ya Kiarabu. Pia, tumeongezea majina ya makumi mbalimbali (10-90)
TARAKIMUKISWAHILIKIARABU
0sufurisufuri
1mojawahed
2mbilithenini
3tatuthelatha
4nnearoba
5tanohamsa
6sitasita
7sabasaba
8nanethemania
9tisatisa
KUMI NA
Majina ya ya tarakimu kutoka (11-19) kwa Kiswahili na kwa Kiarabu.
10+KISWAHILIKIARABU
11kumi na mojaedatashara
12kumi na mbilithenashara
13kumi na tatuthelathashara
14kumi na nnearobatashara
15kumi na tanohamsatashara
16kumi na sitasitatashara
17kumi na sabasabatashara
18kumi na nanethemantashara
19kumi na tisatisatashara
MAKUMI
Kuandika tarakimu mbalimbali katika hali ya ukumi. (11-99).
*10JINAMFANO
#KISWAHILIKIARABU
10kumi12kumi na mbilithenashara
20ishirini27ishirini na sabasaba wa ishirini
30thelathini32thelathini na mbilithenini wa thelathini
40arobaini42arobaini na mbilithenini wa arobaini
50hamsini52hamsini na mbilithenini wa hamsini
60sitini61sitini na mojawahed wa sitini
70sabini76sabini na sitasita wa sabini
80themanini89themanini na tisatisa wa themanini
90tisini93tisini na tatuthelatha wa tisini
AKISAMI
Akisami hutumiwa kuonyesha sehemu ya kitu kizima. Kwa mfano, ukigawa kilo moja kwa visehemu vinne vinavyotoshana, kila kisehemu kitakuwa na uzani wa robo kilo ( sehemu ya nne au moja kwa nne ) ya kilo.
1/#JINAMFANO
1/2nusu1/2nusumoja kwa mbili
1/3thuluthi2/3thuluthi mbilimbili kwa tatu
1/4robo2/4robo mbilimbili kwa nne
1/5humusi3/5humusi tatutatu kwa tano
1/6sudusi4/6sudusi nnenne kwa sita
1/7subui6/7subui sitasita kwa saba
1/8thumuni7/8thumuni sabasaba kwa nane
1/9tusui3/9tusui tatutatu kwa tisa
1/10ushuri6/10ushuri sitasita kwa kumi
1/100asilimia72/100asilimia sabini na mbilisabini na mbili kwa mia moja
MIFANO ZAIDI
  1. Andika nambari zifuatazo kwa maneno/herufi:
    1. 3 ⇒ tatu
    2. 952 ⇒ mia tisa hamsini na mbili
    3. 680 ⇒ mia sita themanini
    4. 4521903 ⇒ milioni nne, na mia tano ishirini na moja elfu, na mia tisa na tatu
    5. 556100016 ⇒ mia tano hamsini na sita milioni, na mia moja elfu, na kumi na sita
  2. Andika tarakimu zifuatazo kwa nambari
    1. sufuri ⇒ 0
    2. mia tatu ishirini na mbili ⇒ 322
    3. sabini na tatu elfu, na mia nane hamsini na tano ⇒ 73855
    4. mia tano sabini na nane elfu, na mia tatu hamsini na tisa ⇒ 578359
    5. mia sita tisini na sita milioni, na mia tisa tisini na nane elfu, na mia saba ishirini na tatu ⇒ 696998723
  3. Andika akisami zifuatazo kwa maneno
    1. 240/295 ⇒ mia mbili arobaini kwa mia mbili tisini na tano
    2. 41/45 ⇒ arobaini na moja kwa arobaini na tano
    3. 26/51 ⇒ ishirini na sita kwa hamsini na moja
    4. 59/74 ⇒ hamsini na tisa kwa sabini na nne
    5. 1/3 ⇒ thuluthi
 
Back
Top Bottom