kilio
Member
- Jan 24, 2014
- 29
- 36
Kwa dunia ya leo ya ulimwengu wa kidigitali, ni lazima somo la hisabati lipewe kipaumbele kwakuwa ni msingi wa program nyingi za teknolojia ya kisasa. Mifumo mingi ya kidigitali tutanyotumia leo katika shughuli mbalimbali ina chembechembe za hisabati katika utengenezaji wake na utumiaji wake. Kwa mfano katika ulimwengu wa sayansi ya data “Data science”, shughuli kubwa ya kuchakata data lazima muhusika awe na msingi mzuri wa somo la hisabati ili kuchakata data hizo na kupata kilichopo kutokana na data “Actionable insight from the data and creating data visualization”. Kiukweli kuna juhudi zimefanfyika katika sayansi ya data kuhakikisha inatumika hapa nchini Tanzania. Sayansi ya data kwa sasa inatumika katika sekta mbalimbali. Miradi mingi inayofadhiliwa na serikali za nje kama Marekani na nchi za ulaya zinasisitiza matumizi ya data ili kupata usahihi wa taarifa na kujua ukubwa wa tatizo au eneo lililolengwa kufanyiwa mradi. Sayansi ya data imewekewa kipaumbele katika sekta kama ya Afya, Kilimo, katika shughuli za Uhandisi, au Uhandishi wa habari “Data Journalism”. Pia katika mashirika binafsi kunaongezeko kubwa wa nafasi za kazi zinazomuhitaji mtu mwenye uzoefu na maarifa katika eneo la sayansi ya data. Nimeshuhudia benki kubwa za Tanzania; CRDB na NMB zinatangaza nafasi za mtu mwenye uwezo katika sayansi ya data. Haya ni mafanikio makubwa, siyo tu kwenye mashirika ya misaada, pia katika makampuni kuna uwekezaji mkubwa katika sayansi ya data.
Tukija katika teknolojia inayozungumzwa kwasasa na inayopewa kipaumbele ya Akili Bandia (Artificial intelligence), hisabati ina mchango mkubwa katika utengenezaji na inavvyotumika. Akili bandia inatazamiwa katika kubadilsha utendeji katika sekta mbalimbali, na ili kuweza kuandika “Alogarithms” zenye uhusiano na program za Akili Bandia.unahitajika kuwa na ujuzi wa mada fulani ambazo msingi wake unapatikana katika somo la hisabati. Utengenezaji wa program za akili bandia zinazotumika kwa mfano kutengenezea video,audio au picha. Pi Utengenezaji wa hizo programu kwasehemu kubwa unahitaji mtu mwenye uelewa wa mahesabu ili kutengeneza kitu kilicho bora.
Nakumbushia, katika sekta ya elimu, Ufaulu mzuri wa Somo la Hisabati katika elimu ya Tanzania inamuwezesha mtoto kuwa na uwanja mpana wa kuchagua masomo katika uchaguzi wa masomo. Wakati ufaulu wa somo kama historia halina uwanja mpana wa kumwezesha mtoto kuchagua. Ufaulu wa somo la hisabati linamwezesha mtoto kusoma “combinations” za masomo ya Arts, au masomo ya Biashara au masomo ya Sayansi. Ukija katika ngazi ya chuo, Maarifa yanayotokana na somo la hisabati unamwezesha mtu kuwa na uwanja mpana katika kuchagua kozi ya kusomea.Ufaulu mzuri unamwezesha mtu kusomea kozi mbalimali katika elimu ya juu katika ngazii ya cheti, stashahada au Shahada. Ukiwa na ufaulu wa somo la hisabati unaweza ukasoma kozi za biashara, za sayansi ya kijamii”Social science” au “Natural science”;Kozi yenye mahusihano na uhandisi, kozi za afya, kozi zenye mahusiano na Fizikia, Kemia na biolojia.
Kwa bahati mbaya somo la hisabati linaongoza kwa ufaulu duni/mbovu kutoka ngazi ya shule ya msingi mpaka shule ya sekondari. Watoto wengi wamekuwa wakilichukia somo la hisabati, wengine wanasema ni somo gumu sana. Na wengine wanajiuliza hesabu wanazosoma darasani ziwasaidia nini katika maisha yao kila siku na maisha yao ya baadae. Kwa upande wao wanasema,hawaoni kama maisha yao ya kila siku hayahusian na hisabati wanazosoma darasani. Kwanin walipende somo hilo, Ukilinganisha na masomo kama ya jografia au uraia (CIVICS) matumizi yake yanaonekana kila siku katika maisha yao. Kiukweli katika hizo ngazi za elimu (shule ya msingi na sekondari), watoto kwa asilimia kubwa wanajifunza hasa kukotoa mahesabu. Watoto wanafundishwa njia mbalimbali za kukotoa mahesabu. Na watoto wenye msingi mzuri wanakuwa na ujasiri wa kukokotoa na kupata alama nzuri. Lazima tufikiri Zaidi ya kuwafundisha watoto kukokotoa mahesabu. Watoto wanataka kujua Hesabu wanazosoma zina msaada gani katika maisha yao ya baadae, na wasihishie kwenye kukokotoa tu.
"Nini Kifanyike kuwawezesha watoto walipende somo la hisabati kuanzia ngazi ya chini mpaka uko waendapo katika elimu ya juu"

- Watoto wafundishwe kwa mifano halisi “Application” za hizo mada wanazofundishwa katika somo la hisabati.
Ili kuwahamasisha (Motivate) watoto walipende somo la hisabati ni lazima waelezwe matumizi ya mada wanazosoma katika mazingira yetu ya kila siku. Kila mada ya somo la hisabati ina matumizi katika mazingira yetu. Kwahiyo, Somo la hisabati lazima lifundushwe katika njia ya matumizi ili watoto waanze kuijenga taswira ya kesho yao. Kwa mfano nikiwa nasoma kidato cha tatu tulijifunza mada ya” statistics”, niliishia kukotoa” Mean, Mode, Standard deviation,” na kuchora grafu na chati.Sikujua ni wapi nitatumia maarifa haya katika mada ya Statistics. Lakini baada ya kuendelea na elimu yangu ya juu. Nilijifunza matumizi ya” statistics” katika mazingira yetu ya kila siku. Je ingekuwaje nisingeendelea na masomo yangu ya elimu ya juu. Niingekuwa mmoja wa wahanga wanaosema hisabati inatusaidia nin katika maisha yetu ya kila siku.
Mfano Kuna mada kama “Probability”, watoto huishia kukotoa Probability ni kubwa kuliko sifuri na ni ndogo kuliko moja. Lakini probability ina mchango mkubwa katika “Digital electronics”, “Cybersecurity”,”Digital Communication”, kwa wataalamu wa jografia wanatumia katika “Remote sensing technology”. Kwahiyo watoto wangepata mwanga kujua wapi wahelekee.
Mada kama “Matrix” ina mchango mkubwa katika elimu ya kanzu data “database”. Mada kama “calculus and integration” zinatumika katika elimu ya ufund au uhandisii. Kama mtoto akifundishwa ili uweze kuwa engineer lazima uwe vizuri katika mada hii. Inaweza kumsaidia mtoto kukazana kufanya vizuri
Hitimisho: Watoto wanatakiwa waandaliwe mapema ili waje kupambana katika dunia ya ushindani. Tusisubiri mpaka wafike katika elimu ya juu ndiyo wasome matumizi ya hizo mada walizosoma katika somo la hisabati. Tutapunguza wimbi la watoto wanaolichukia hili somo la hisabati katika ngazi za chini.
Upvote
1