Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kuna mrembo mmoja nilitokea kumpenda, na katika harakati ikapelekea tukapata mtoto naye.
Nilimpenda kutokana na muonekano wake, achilia mbali ni mtu anayependa sana mambo ya urembo urembo.
Pia ni mtu mwenye tabia ya kujisifia sifia, na kuniona mimi kama mtu mwenye bahati kwa kuwa naye.
Kuna kauli moja huwa anapenda kuongea, ambayo huwa inaniumiza sana, ''unajua mimi ni mzuri, inabidi ujivunie unapokuwa na mimi na unihudumie kwa wakati pale ninapohitaji matumizi.''
Nimejaribu kumvumilia kwa muda mrefu, ila bahati nzuri tunaishi mikoa tofauti; kwa hiyo mara nyingi kuonana lazima mmoja aweze kusafiri.
Baada ya kujifungua alinenepa sana, nami nikavutiwa zaidi na muonekano wake kwa sababu mimi huwa napenda warembo wenye miili mikubwa na mvuto.
Kwa upande wake ile hali haikumvutia, akaamua kutumia njia mbali mbali aweze kupungua, na kuwa na mwili mdogo ambao kwangu ulikuwa haunivutii.
Hivi karibuni alikuja kunitembelea, baada ya kuona mwili wake ulivyopungua, hisia zikapotea kabisa; ata tulivyolala sikumfanya chochote, kwa sababu amekua ni wabaridi joto hakuna tena.
Nikamuuliza kwa nini unajipunguza, akasema anataka asizeeke mapema na anataka aendelee kuonekana binti.
Nikamshauri aurudishe ule mwili wake ili hisia pia ziweze kurudi, kwa sababu kwa sasa gari imegoma kuwaka.
Ingawa hakupendezwa na kilichotokea, lakini ndio hivyo hakuna namna.