HISTORIA: Alichofanyiwa Zelensky Ikulu ya Marekani, Muingereza, Mfaransa na Israeli walifanyiwa mwaka 1956

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Mfalme Suleimani aliwahi kusema hakuna jipya chini ya jua.

Jana limetokea jambo ambalo limeshangaza dunia kidogo, lakini ukweli ni kwamba kama wewe ni msomi wa historia utafahamu kwamba fedheha za waziwazi na namna ile zimewahi kufanywa na Raisi wa Marekani General Dwight Eisenhower mwaka 1956 baada ya mataifa rafiki kabisa kuingilia maslahi ya Marekani.

Inaanza na raisi wa Misri, Gamal Abdel Nasser ambaye sera zake zilikuwa ni hatari kwa maslahi ya wakubwa wa dunia hii. Hapa Afrika aliingilia maslahi ya Mfaransa kwa kudhamini waasi nchini Algeria, kule Mashariki ya Kati aliingialia nchi za kiarabu kama Jordan ambako alishawishi na kuratibu maandamano wanajeshi wa Uingereza wafukuzwe kwenye majeshi ya nchi hiyo (Arabization Program), na alikuwa ndiyo nchi kinara wa kushawishi Arab League wapambane na Wazayuni wa Israeli.

Mwaka 1956 akaenda mbali kabisa na kuamua kutaifisha mfereji wa Suez, (Suez Canal), ambao ulijengwa mwaka 1859 na hisa zake kumilikiwa na Muingereza na Mfaransa. Mfereji huu ndiyo unapitisha manowari zote za kibiashara kutoka Asia kwenda Ulaya. Bwana Nasser akaamua kuufanya uwe mali ya ummah. Jambo ambalo likawakera wakubwa wa dunia ambao waliamini kama Misri ikiendelea hivi, basi muda siyo mrefu maslahi yao yatahatarishwa.

Anthony Eden, Waziri Mkuu wa Uingereza, Rene Coty, Raisi wa Ufaransa, na David Ben Gurion, Waziri Mkuu wa Israel, walifanya kikao cha siri kabisa na kuunda umoja wa kijeshi kuvamia Misri ili kumtoa Nasser. Waliamini hakuwezi kuwa na madhara makubwa sana kwasababu hata Marekani iliwahi kugombana na Nasser baada ya kuwashikilia Wasovieti kwenye ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Aswan (The Aswan High Dam).

Masikini, hawa viongozi walichanga karata zao vibaya. Marekani alikuwa na malengo marefu na Misri kama ambavyo alikuwa na malengo na Israel. Kuitumia Misri kusambaza ushawishi wake kiuchumi na kutowafanya waarabu wasifungamane na upande wa wakomunisti.

Baada ya uvamizi, Raisi wa Marekani, General Eisenhower, alipiga mkwara mzito kwelikweli na kusema kama vita hiyo haitaisha mara moja, basi Marekani angeuvuruga kabisa uchumi wa Uingereza ambao yeye ndiyo alikuwa anaushikilia tokea mwaka 1945 baada ya vita ya dunia. Alitishia kuuza deni lote la Uingereza ambalo analimiliki kupitia Hati-Fungani (Sovereign Bonds), jambo ambalo lingeifanya London ambayo ilikuwa bado ni kitovu cha biashara ya fedha (Financial Markets Capital) kwa wakati huo, pamoja na Pound Sterling ambayo bado ilikuwa na mzunguko mkubwa mno kuanguka kabisa.

Mambo yakawa mabaya zaidi baada ya kiongozi wa Wasovieti, Nikita Khruschev kuunga mkono kauli ya General Eisenhower na kutishia kulipua Uingereza na Israel kwa makombora mazito ya kinyuklia endapo hawatasitisha uvamizi huo mara moja. Mkwara huu Marekani hakuonesha kukerwa nao kabisa ilhali yeye ndiye alikuwa mlinzi mkuu wa Ulaya dhidi ya Ukomunisti wa Kisovieti.

Jambo hili liliwakera na kuwashangaza watu wa Ulaya hasahasa Waziri Mkuu wa Ujerumani, Conrad Adeneur ambaye alikosoa wazi kwa kusema haitakiwi Marekani aungane na Wasovieti, maana yeye ni mwenzao na anatakiwa kuwahakikishia ulinzi, hasahasa dhidi ya vitisho vya shambulio ya kinyuklia.

Kuonesha hasira zaidi nchi za Ulaya zikaamua kutengeneza Umoja wa Ulaya (EU) mwaka 1957, uliofahamika kama European Economic Community ili kuanza kujitegemea na hata kuwa na jeshi lake, jambo ambalo lilifanikiwa nusu maana waliishia tu kuwa na umoja wa kibiashara bila kuwa na jeshi. Mfaransa akaamua na yeye kutafuta silaha zake na kinyuklia na hichi kinyongo kilikuja kupelekea ajitoe NATO siku za mbeleni.

Songombingo hili lilikuwa ni kubwa mno hadi kupelekea waziri mkuu wa Uingereza, Anthony Eden kujiudhuru kwasababu alilidanganya bunge na kupelekea usalama wa nchi kuhatarishwa.

Israel na kutaka kuweka ULTIMATUMS kwa Marekani ili aweze kutoa vikosi vya Misri hasa Sinai Peninsula, vilikutana na ukuta mzito, mwishowe walikubali kuwa wa kwanza kabisa kuondoa vikosi vyao maana kama wangeendelea kushupaza shingo yangewakuta.

Magazeti na Vyombo vya habari duniani kote hasahasa Ufaransa na Uingereza vilishangazwa na hizi kauli za Marekani dhidi yao. Wao walichukulia Marekani kama Mkubwa wao, lakini aliamua kuwadhalilisha viongozi wa nchi zao kwa kuwakemea na kuwatishia hadharani kama watoto wadogo.

UNO (United Nations Organization) nayo ilitishia kuiwekea Uingereza vikwazo vikali endapo ingerusha hata mabomu machache ambayo yangedhuru watu. Jambo hili halikuwahi kutokea, maana Uingereza ni mwanachama wa kudumu wa UNSC na ana kura ya VETO, lakini alitishiwa na UN hadi akaogopa.

===========================================

Mambo ni mengi sana, muda mchache
 
Naam mkuu asante kwa hii kumbukizi nimeshiba maarifa

Naomba kuuliza ---- Ni kitu kipi kitakacho mfika zelensky endapo atakaidi maagizo ya USA ??
Zelensky kazi yake imeisha very soon atakuwa replaced na kuwekwa Prefect mwingine pale Ukraine. Akishupaza shingo watamuua kama ambavyo baada ya kutumikia maslahi ya Marekani waliuawa viongozi kama Sadam, Mobutu na Savimbi
 
Wazi
 
wote ulaya na USA wana bosi mmoja, ni kama soviet union vs the West, au communism vs capitalism wote wana bosi mmoja, aliyeanzisha na kufund evil communism ni Wealthy capitalistic western bankers …
 
Hapo ndio watu wanatakiwa wajue kua kuna wahuni fulani wameigawa hii dunia pande 2 ili wapate kuitawala kwa urahisi.
Ni sawa tu na bifu lililopo baina ya CocaCola na Pepsi unaweza ukahisi ni maadui wasiopendana kumbe ni michezo tu tunachezewa.
 
Naam mkuu asante kwa hii kumbukizi nimeshiba maarifa

Naomba kuuliza ---- Ni kitu kipi kitakacho mfika zelensky endapo atakaidi maagizo ya USA ??
Leo wakongwe wawili mmeonekana hadharani.
Mkuu Malcolm Lumumba na Mkuu Hearly.
KARIBUNI
 
Sifahamu lolote mkuu, mimi nimeweka hii kumbukizi tu.
Hapana toa tathmini bana acha utani.
Je USA wataondoa majeshi na vifaa vyao Ulaya ili zelensky akomeshwe na Urusi?
Je Ulaya peke Yao wanaweza kumkingia kifua zelensky dhidi ya mighty Russia?
 
Zelensky kazi yake imeisha very soon atakuwa replaced na kuwekwa Prefect mwingine pale Ukraine. Akishupaza shingo watamuua kama ambavyo baada ya kutumikia maslahi ya Marekani waliuawa viongozi kama Sadam, Mobutu na Savimbi
Huyu Zelensky ana bahati sana hawezi kuuliwa na CIA kwa sababu itajulikana wazi wao ndio wamemla kichwa.
Isipokua kitakachofanyiaka ni kupigwa Presha Kali ili aitishe uchaguzi,na hapo ndio mwisho wake kama Rais utakua umefika.
Kwenye uchaguzi Zelensky hatoboi.
Hasa ukizingatia fitina za USA.
 
Urusi mikwara wameanza kitambo sana ..
Palikua na battle za kijasusi sana hapo Berlin, urusi walikua na mtu wao ndani ya society ya kijasusi ya uingereza, walikua wanavuna tu info za USA na uingereza
 
Mfalme Suleimani aliwahi kusema hakuna jipya chini ya jua.

Jana limetokea jambo ambalo limeshangaza dunia kidogo, lakini ukweli ni kwamba kama wewe ni msomi wa historia utafahamu kwamba fedheha za waziwazi na namna ile zimewahi kufanywa na Raisi wa Marekani General Dwight Eisenhower mwaka 1956 baada ya mataifa rafiki kabisa kuingilia maslahi ya Marekani.

Inaanza na raisi wa Misri, Gamal Abdel Nasser ambaye sera zake zilikuwa ni hatari kwa maslahi ya wakubwa wa dunia hii. Hapa Afrika aliingilia maslahi ya Mfaransa kwa kudhamini waasi nchini Algeria, kule Mashariki ya Kati aliingialia nchi za kiarabu kama Jordan ambako alishawishi na kuratibu maandamano wanajeshi wa Uingereza wafukuzwe kwenye majeshi ya nchi hiyo (Arabization Program), na alikuwa ndiyo nchi kinara wa kushawishi Arab League wapambane na Wazayuni wa Israeli.

Mwaka 1956 akaenda mbali kabisa na kuamua kutaifisha mfereji wa Suez, (Suez Canal), ambao ulijengwa mwaka 1859 na hisa zake kumilikiwa na Muingereza na Mfaransa. Mfereji huu ndiyo unapitisha manowari zote za kibiashara kutoka Asia kwenda Ulaya. Bwana Nasser akaamua kuufanya uwe mali ya ummah. Jambo ambalo likawakera wakubwa wa dunia ambao waliamini kama Misri ikiendelea hivi, basi muda siyo mrefu maslahi yao yatahatarishwa.

Anthony Eden, Waziri Mkuu wa Uingereza, Rene Coty, Raisi wa Ufaransa, na David Ben Gurion, Waziri Mkuu wa Israel, walifanya kikao cha siri kabisa na kuunda umoja wa kijeshi kuvamia Misri ili kumtoa Nasser. Waliamini hakuwezi kuwa na madhara makubwa sana kwasababu hata Marekani iliwahi kugombana na Nasser baada ya kuwashikilia Wasovieti kwenye ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Aswan (The Aswan High Dam).

Masikini, hawa viongozi walichanga karata zao vibaya. Marekani alikuwa na malengo marefu na Misri kama ambavyo alikuwa na malengo na Israel. Kuitumia Misri kusambaza ushawishi wake kiuchumi na kutowafanya waarabu wasifungamane na upande wa wakomunisti.

Baada ya uvamizi, Raisi wa Marekani, General Eisenhower, alipiga mkwara mzito kwelikweli na kusema kama vita hiyo haitaisha mara moja, basi Marekani angeuvuruga kabisa uchumi wa Uingereza ambao yeye ndiyo alikuwa anaushikilia tokea mwaka 1945 baada ya vita ya dunia. Alitishia kuuza deni lote la Uingereza ambalo analimiliki kupitia Hati-Fungani (Sovereign Bonds), jambo ambalo lingeifanya London ambayo ilikuwa bado ni kitovu cha biashara ya fedha (Financial Market) kwa wakati huo, pamoja na Pound Sterling ambayo bado ilikuwa na mzunguko mkubwa mno kuanguka kabisa.

Mambo yakawa mabaya zaidi baada ya kiongozi wa Wasovieti, Nikita Khruschev kuunga mkono kauli ya General Eisenhower na kutishia kulipua Uingereza na Israel kwa makombora mazito ya kinyuklia endapo hawatasitisha uvamizi huo mara moja. Mkwara huu Marekani hakuonesha kukerwa nao kabisa maana ndiye alikuwa mlinzi mkuu wa Ulaya dhidi ya Ukomunisti wa Kisovieti.

Jambo hili liliwakera na kuwashangaza watu wa Ulaya hasahasa Waziri Mkuu wa Ujerumani, Conrad Adeneur ambaye alikosoa wazi kwa kusema haitakiwi Marekani aungane na Wasovieti, maana yeye ni mwenzao na anatakiwa kuwahakikishia ulinzi, hasahasa dhidi ya vitisho vya shambulio ya kinyuklia.

Kuonesha hasira zaidi nchi za Ulaya zikaamua kutengeneza Umoja wa Ulaya (EU) mwaka 1957, uliofahamika kama European Economic Community ili kuanza kujitegemea na hata kuwa na jeshi lake, jambo ambalo lilifanikiwa nusu maana waliishia tu kuwa na umoja wa kibiashara bila kuwa na jeshi. Mfaransa akaamua na yeye kutafuta silaha zake na kinyuklia na hichi kinyongo kilikuja kupelekea ajitoe NATO siku za mbeleni.

Songombingo hili lilikuwa ni kubwa mno hadi kupelekea waziri mkuu wa Uingereza, Anthony Eden kujiudhuru kwasababu alilidanganya bunge na kupelekea usalama wa nchi kuhatarishwa.

Israel na kutaka kuweka ULTIMATUMS kwa Marekani ili aweze kutoa vikosi vya Misri hasa Sinai Peninsula, vilikutana na ukuta mzito, mwishiwe walikubali kuwa wa kwanza kabisa kuondoa vikosi vyao maana kama wangeendelea kushupaza shingo yangewakuta.

Magazeti na Vyombo vya habari duniani kote hasahasa Ufaransa na Uingereza vilishangazwa na hizi kauli za Marekani dhidi yao. Wao walichukulia Marekani kama Mkubwa wao, lakini aliamua kuwadhalilisha viongozi wa nchi zao kwa kuwakemea na kuwatishia hadharani kama watoto wadogo.

UNO (United Nations Organization) ilitishia kuiwekea Uingereza vikwazo vikali endapo ingerusha hata mabomu machache ambayo yangedhuru watu. Jambo hili halikuwahi kutokea, maana Uingereza ni mwanachama wa kudumu wa UNSC na ana kura ya VETO, lakini alitishiwa na UN hadi akaogopa.

===========================================

Mambo ni mengi sana, muda mchache
uko vizuri mno eneo hili mkuu
 
Huyu jamaa alikuwa na mwezi mchanga.

Siku moja anatoa hotuba akasema hivi:
"Berlin is a testicle of the West. If a want the West to scream I just squeeze on Berlin"
Urusi huwa inapata viongozi chakaramu balaa 😄😄
 
“Gagarin flew into space, but didn't see any god there."

Hapa anatoa hotuba baada ya mwanasayansi wa kwanza wa kisovieti, Yuri Gargarin kufanikiwa kwenda nje ya anga za mbali. Sasa anawaambia warusi kwamba hakuna Mungu.
 
Back
Top Bottom