Historia fupi ya Oman

Historia fupi ya Oman

Tokyo40

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
2,065
Reaction score
1,925
Zana za watu wa kale (Paleolithic stone tools) zilichimbuliwa katika mapango au majabali, kusini mwa Oman, karibu na Straits of Hormuz, njia muhimu ya bahari kati ya Ghuba ya Oman na Ghuba ya Uajemi.

Hizi zana, zilifanana na zile zilizochimbuliwa Afrika. Zilitumiwa zaidi ya miaka 125,000 iliyopita.

Kuanzia 300 B.C mpaka kuingia kwa dini ya Kiislamu mwaka 700 A.D, Oman ilikuwa chini ya Wairani ( Parthian and Sassanid Dynasty). Oman hapo ilikuwa inajulikana kwa jina la Mazum. Sehemu ya Oman ilikuwa muhimu sana kwa ajili ya biashara na usalama wa "Dynasties" za Wapersia. Wakapata utamaduni wa watu wa Iran na kuwa na jeshi lao pamoja na kutumia njia bora ya kilimo cha umwagiliaji cha Wapersia.

Wakati wa uhai wa Mtume Muhammad (S.A.W), Uislamu ukaenea na kusambaa. Uislamu wa Oman wengi unaitwa " Ibadhi" au "ibadiyya" na siyo wenye siasa kali kama wa Kiwahabi wa Saudi Arabia. Mpaka leo, Oman ni nchi yenye wafuasi wengi wa Ibadhi kuliko nchi yoyote.

Wapersia wa Kishiia wa makabila tofauti waliitawala Oman mpaka 1053 A.D. Baada ya hapo walikuwa chini ya utawala wa "Seljuk Turk Empire" mpaka 1154.

Wazalendo wa Oman wa ukoo wa Kifalme wa Nabhani waliweza kuchukua madaraka 1443. Kuna miaka kati ya 1154 na 1443, walipokonywa madaraka na makabila tofauti ya Wapersia waliposhindwa katika vita.

Mjini Mkuu wa Muscat ikachukuliwa na Wareno mwaka 1515 mpaka 1650. Baadhi ya ardhi ya Oman ilikuwa chini ya "Ottoman Empire" na ukoo wa Kifalme wa Nabhani pia waliweza kutawala baadhi ya sehemu ya Oman vile vile.

Mwaka 1650, ukoo wa Al-Ya'ariba (Yaruba Dynasty) wa asili ya nchi jirani ya Yemen, waliweza kuwashinda nguvu Wareno na kuitawala tena Muscat. Pia, waliweza kuunganisha makabila tofauti ya Oman siyo tu waweze kuwa na umoja na nguvu ya kuwatimua Wareno bali pia kuiwezesha Oman kuwa na uchumi bora kwa kutumia rasilimali ya bahari yao.

Chini ya Imam wa Kwanza wa Yaruba Dynasty, Imam Nasir bin Murshid, Oman ikawa na umoja katika makabila yao na kuwatimua Wareno, Oman.

Alipofariki Nasir, mwaka 1649, Sultan bin Saif, binamu yake, akatumia nguvu yake ya jeshi na kupigana na Wareno kutoka India mpaka Afrika Mashariki.

Hapa ndipo uhusiano wa Oman na Zanzibar ulipoanza.

Zanzibar ikashambuliwa na kuchukuliwa mwaka 1652 na jeshi lake na Mombasa kuchukuliwa mwaka 1696 baada ya kushambuliana na jeshi la Ureno tangu mwaka 1691. Pemba na Kilwa ikachukuliwa mwaka 1699.

Alipofariki Sultan bin Saif mwaka 1679, kukatokea ugomvi Kati ya watoto wake. Mtoto wake Bil'arab bin Sultan akachukua madaraka lakini ndugu yake, Saif bin Sultan hakupendezewa na kulikuwa na ugomvi katika madaraka yake mpaka alipomrithi madaraka kwa njia ya vita , ndugu yake, Bil'arab, mwaka 1692.

Imam Saif bin Sultan aliijenga Oman vizuri. Chini ya utawala wake, aliweza kuwashinda Wareno na kuchukua makoloni yake ya Zanzibar, Pemba, Kilwa na Mombasa. Akafika mpaka Msumbiji na Kongo.

Chini yake, wananchi wengi wa Oman walianza kwenda kuishi Zanzibar.

Aliwateua Magavana mbalimbali katika koloni zake ambao walikuwa chini ya Gavana Muhammed bin Uthman Al-Mazrui wa Mombasa.

Sultan Saif alishindwa kutawala vizuri kwa kuwa Gavana Al-Mazrui alikuwa hamtii Sultani na kuendesha nchi anavyopenda. Mpaka hapo baadae, ukoo wa Al-Mazrui walijaribu kupigana na ukoo wa Sultani wa Oman wakishirikiana na Wareno. Wakashindwa.

Saif bin Sultan alifariki mwaka 1711 akiwa tajiri. Alimiliki meli 28, 1/3 ya mitende yote ya Oman na watumwa 700.

Mtoto wake, Sultan bin Saif II akarithi Usultani. Akafariki mwaka 1718. Kwa kuwa mtoto wake alikuwa mdogo, familia waligombania Usultani kivita wenyewe kwa wenyewe.

Nchi ikarudi nyuma kiuchumi. Mwisho nchi ikajigawanya kati ya uongozi wa Kisultani wa ukoo wa Kisunni wa Ghafiri waliompenda mtoto , Saif bin Sultan, na ukoo wa Ibadi wa Hinawi waliomchagua binamu yake, Bal'arab bin Himyar kuwa Imam (Kiongozi) wao.

Saif alikuwa mjanja na mlevi wa mvinyo wa Shiraz. Akamzidi kete Himyar kwa kuomba jeshi la Persia la Nader Shah.

Shah akamsaidia lakini jeshi lake lilikuwa katili na kuchoma na kuiba mali yote mwaka 1737. Saif akashinda lakini wananchi wakachukizwa na tabia yake ya starehe nyingi na kuomba msaada wa kijeshi kutoka kwa maadui wa kihistoria wa Oman.

Mwaka 1742, akatokea Sultani mwingine, Sultan bin Murshid, kumpinga Saif kutawala. Saif akaomba tena msaada wa Wairani. Aliwaahidi mji wa Sohar kama Ahsante yake.

Waliwasili mwaka uliofuata lakini wakashindwa kuukamata mji wa Murshid wala Sohar. Wakamdanganya kuwa itakuwa rahisi wakiingia ndani ya ngome iliyokuwa inamlinda na wananchi wake Muscat. Akawapa ruhusa kuingia ngome ya Al Jalali na Al Mirani.

Jeshi la Wairani likaiteka ngome na kuwaua watu wote ndani. Katika vita hivi, wakafa Saif na Murshid. Lakini Wairani hawakuweza kuwatawala kwa muda mrefu.

Himyar, Sultani aliyompinga Saif, akawa Sultani wa Oman kabla ya kupingwa na Gavana wa Sohar, mwaka 1744.

Gavana Ahmad bin Said Al-Busaidi akawatimua Wairani mwaka 1747 na kuwa Sultani asiye na mpinzi baada ya Bal'arab bin Himyar kufariki mwaka 1749.

Hapa ndiyo ikawa mwanzo wa utawala wa ukoo wa Said Al-Busaidi.

Ahmad akafariki mwaka 1783. Mtoto wake, Said bin Ahmad akachukuwa madaraka na kutawala mpaka 1786.

Alipofariki mwaka aingia mtoto wake, Hamad bin Said mpaka 1792.

Akafariki na smallpox, mjomba wake, Sultan bin Ahmed akachukuwa madaraka mpaka 1804.

Alipofariki, watoto wawili, Salim na Said bin Sultan wakatawala pamoja. Salim akafariki mapema baada ya kutawala miaka miwili tu na kumwacha Said kutawala mpaka 1856. Ndugu hawa walipinduliwa lakini waliweza kurudi katika uongozi tena.

Said bin Sultan ni kiungo mzuri na Zanzibar.

Alianzisha uhusiano wa Kirafiki na Marekani. Mwaka 1837, akaichukua Mombasa kutoka kwa Wareno. Akahama kabisa Zanzibar kutoka Oman mwaka 1840.

Alipofariki mwaka 1856, watoto wake wawili waligombania Usultani.

Serikali ya Uiingereza ikawasuluhisha na maamuzi yalifanywa na kila mtoto akapewa Usultani.

Thuwaini bin Said Al-Said akawa Sultani wa Muscat na Oman. Huyu hajafika Zanzibar.

Oman ilikuwa inajulikana Kama "Muscat and Oman". Jina lilibadilishwa baadae na Sultan Qaboos miaka ya 70 na kuitwa " Sultanate of Oman ".

Ndugu yake, Majid bin Said, akawa Sultan wa Zanzibar (Sultanate of Zanzibar).

Kila mwaka Majid alifanya makubaliano ya kumlipa Thuwaini fedha kusaidia uchumi wa Oman.

Biashara za meli za Bahari Hindi zimeitajirisha Zanzibar.
Wahindi, Wachina na wahamiaji kutoka Oman waliokimbia hali ngumu ya maisha wameijenga Zanzibar.

Oman iliimiliki Dar es Salaam, Mombasa, Kilwa, Pemba, Zanzibar na ardhi iliyokuwa chini ya Wareno huko India na Msumbiji. Hawakuweka jeshi wala serikali nje ya Zanzibar. Magavana wa Sultani walijichotea mali na kuongoza kama koloni lao binafsi. Walijuwa kuwa uongozi wa Masultani uko mbali yao na Sultani walikuwa hawasafiri mara kwa mara, kuogopa kupinduliwa.

Ndio maana ikawa rahisi kuwatoa uongozi, Afrika ilivyoanza kugawanywa katika mkutano wa Berlin wa 1884.
Uiingereza na Ujerumani wakajigawania ardhi yote nje ya Oman.

Oman yenyewe ikawa chini ya hifadhi ya Uiingereza (British protectorate) mwaka 1891.

Hali ya kisiasa ikazidi kuchafuka Oman. Uiingereza ikaingilia tena na kumsaidia kifedha na kijeshi kibaka wao, Turki ibn Said Al - Busaid kuwa Sultani.

Walimpinduwa Azzan ibn Qais, aliyochukuwa madaraka Oman baada ya kufariki Thuwain mwaka 1866.
Mtoto wa Thuwain , Salim, alivuliwa madaraka na Azzan mwaka 1868.

Azzan akafariki katika vita na Turki. Mjomba wa Salim, Turki, akawa Sultani mwaka 1871 mpaka 1888 alipofariki.

Salim alikufa India mwaka 1876 akiwa mfungwa wa nyumbani wa Uiingereza.
Uiingereza hawakumwanini kuwa hajamuua baba yake kuchukuwa madaraka.

Turki alipofariki, Mtoto wake Faisal bin Turki akachukuwa madaraka mwaka 1888 mpaka 1913.

Faisal na mwanawe Taimur bin Faisal, walishindwa kutawala vizuri kwa kuwa Imam wa vijijini walikuwa na nguvu ya kuongoza vijiji vyao bila ya kuheshimu uongozi wa Sultani.

Uingereza ulipenda uongozi wa aina hii ili Oman isiwe na nguvu ya kumfukuza. Aliingilia tena na kufanya mkataba baina ya imam wengi na Sultani ili wasimpindue au kushambulia Muscat. Na Sultani atawaachia wajiongoze lakini waheshimu na kukubali kuwa Sultani ni Mkuu wa nchi. (Treaty of Assib).

Uiingereza iliingilia Kati siasa za Oman mpaka mwaka 1951 ilipowapa uhuru wao wa kujiamulia mambo yao.

Uiingereza ikasaidia kuvunja uongozi wa Kiimamu na kumfanya Sultani kuwa na uongozi wa nguvu baada ya kugunduwa mafuta. Ilikuwa vigumu na ghali kufanya biashara na viongozi wengi.

Hii pia ikapunguza vita vya mara kwa mara vya kumpindua Sultani asiyependwa na imamu fulani.

Sultan Said bin Taimur alichukuwa nchi ikiwa na madeni mwaka 1932. Baba yake, Faisal , alijiuzulu.

Said akaja kupinduliwa na Mtoto wake, Sultan Qaboos mwaka 1970. Alisaidiwa na Uiingereza na mjomba wake.

Said hajaweza kuongoza nchi vizuri. Saudi Arabia ,Misri na Yemen walikuwa wanasapoti Imamu waliofukuzwa na Said. Pia walitaka Uiingereza iondoke Oman.

China waliwasapoti kundi linalotaka kumpindua na kumaliza uongozi wa Kisultani. Kulikuwa na jaribio la kumuua mwaka 1966. Akawa anajifungia na kuto sema na mtu, hata mwanae.

Said akakataza kuvuta sigara, kuvaa miwani, kuongea na wenzako zaidi ya dakika 15. Mtoto wake aliwekwa jela ya nyumbani. Alikuwa "paranoid".

Aliwauzia Pakistan, koloni lake la mwisho , Gwadar, kwa dola milioni moja mwaka 1958.

Sultan Qaboos akampindua na kumpa ukimbizi wa nguvu, London. Akafariki huko mwaka 1972.

Sultan Qaboos akaweza kuleta amani na umoja tena. Akaibadilisha jina na kuiita "Sultanate of Oman".

Uchumi wa petroli ukaleta maendeleo, elimu bora na hali nzuri ya maisha.

Vita na baadhi ya wananchi wake wa Dhofar vikaisha kwa msaada wa nchi rafiki. Walipigana miaka 14 ili wajitenge na Oman. Walihisi kunyanyaswa na kubaguliwa kama jamii tofauti na Waomani.

Ukoo wa Ahmed bin Said Al-Busaidi unaendelea kuitawala Oman mpaka leo.

Kizazi cha 14 cha ukoo huu ni Sultan Qaboos bin Said Al- Said.

Leo, Oman ni nchi safi, ya amani na utajiri wa mafuta.

Wananchi wake bado hawana demokrasia kamili.

Hamna kura ya kuchagua uongozi.

Oman ni "Absolute Monarchy".

Sultani Qaboos, ana miaka 76, mgonjwa na hana mtoto.

Chanzo:

en.m.wikipedia.org

Historytoday.com

Realhistoryww.com

Omansultanate.com

Zanzibar.cc/chronology.htm
 
Domo aregeto sensei Tuukyo juu yon.
Asante sana mwalimu Tokyo40
 
Domo aregeto sensei Tuukyo juu yon.
Asante sana mwalimu Tokyo40

Dou Itashemashte.

Mkuu mgogoone, Mimi ni mwanafunzi wa historia bado.

Karibu kunifunza hapa.
 
Hivi Oman wamegundua nini cha kuvutia au ndo wanasemaga wamefanikiwa kugundua mkeka tu???
 
Ficha aibu yako,sio lazima uchangie kila kitu.
wewe ndo unajivua nguo unajifanya "mr. know it" kumbe kichwani bogus kumejaa mimavi, kwanza sitaki kujibizana na wewe tafuta level yako me sio mtu wa umbea, period.
 
Hivi Oman wamegundua nini cha kuvutia au ndo wanasemaga wamefanikiwa kugundua mkeka tu???

Oman ni tajiri wa mafuta.

Uongozi wao wameutumia utajiri huu vizuri. Kila raia anapata elimu bora na nyumba za bei nafuu. Watoto wanasomeshwa duniani kote bure, kama wamehitimu vizuri.

Nchi safi na ina amani.

What more can you ask?
 
wewe ndo unajivua nguo unajifanya "mr. know it" kumbe kichwani bogus kumejaa mimavi, kwanza sitaki kujibizana na wewe tafuta level yako me sio mtu wa umbea, period.

Let's all be civil.
 
Sultan Qaboos anamiaka 76 na Hana Mtoto .....kwahiyo hakuna mrithi tena baada yake na huu ndo mwisho wa koo hyo kutawala Oman
 
Umeruka ruka sana

Napenda utufunue kwenye yafuatayo :

1. Chanzo cha wao kutawala East Africa. Tuliambiwa kulikuwa na watoto wawili wa sultan mmoja aliambiwa akatafute mali na partners nchi za arabuni na mwingine alikuja down south ndio wa down south anakutafuta nchi za East Africa kuna Neema ndio uamuzi ukawa kuwa wajitwike East Africa and Zanzibar in particular. Naomba ufafanuzi

2. Kuna story kuwa current ruling elites ni wa Zanzibari je kuna ukweli kwenye hili? Tuliambiwa kuwa baada ya mapinduzi Zanzibar waliokenda Oman walikuwa bado hawako Civilized ndio wa kapewa fursa mbali mbali na ndio walimilikishana Oman hapo ilipo is this true?

3. Niliskikia kuwa watu we using wengi wako maeneo ya salala na ndio waliojazana jeshini etc. Mbona hatuwaskii wala kuwaona kwenye utawala ???

4. Naomba wasitumie wa nephew wake Qabus anayeitwa Said Haytham tafadhali

5. Naomba utueleze kwa nini Oman haija invest sana Zanzibar ambayo wana cultural linkages kuliko nchi yoyote ile ya GCC??


6. Hebu tupate historia ya wale wahindi akina Khimijis ambao wako close sana na ruling elites wa Oman

7. Inasemekana kuwa aliyekuwa balozi wa Oman toka 2012 alirejeshwa nyumbani na Magufuli kwa makosa makubwa sana je kuna ukweli wowote au bas tuuu story za mitaani?
 
Sultan Qaboos anamiaka 76 na Hana Mtoto .....kwahiyo hakuna mrithi tena baada yake na huu ndo mwisho wa koo hyo kutawala Oman

Kuna watoto wa Mjomba. Inasemekana wameandaliwa tayari.

The Sultan himself told Foreign Affairs magazine in 1997: “I have already written down two names, in descending order, and put them in sealed envelopes in two different regions.”

chanzo: middleeasteye.com

... The successor to Qaboos would appear to be the children of his late uncle, Sheikh Tariq bin Taimur Al Said, Oman's first prime minister before the sultan took over the position himself (and his former father-in-law).

Oman watchers believe the top contenders to succeed Qaboos are three of Tariq's sons:

1. Assad bin Tariq Al Said, the personal representative of the Sultan.

2. Shihab bin Tariq, a retired naval commander.

3. Haytham bin Tariq, the Minister of Heritage and National Culture.

First Deputy Prime Minister Fahd bin Mahmud al-Said, a distant cousin of the Sultan, and Taimur bin Assad, the son of Assad bin Tariq, are also mentioned as potential candidates.

The problem is that none of the above seem to have the necessary capacities to rule Oman, since Sultan Qaboos, differently from the other Persian Gulf countries, has relied more on the business elite than on family members, who have been excluded from key positions, to secure his power over the country.

Chanzo:

en.m.wikipedia.org
 
Umeruka ruka sana

Napenda utufunue kwenye yafuatayo :

1. Chanzo cha wao kutawala East Africa. Tuliambiwa kulikuwa na watoto wawili wa sultan mmoja aliambiwa akatafute mali na partners nchi za arabuni na mwingine alikuja down south ndio wa down south anakutafuta nchi za East Africa kuna Neema ndio uamuzi ukawa kuwa wajitwike East Africa and Zanzibar in particular. Naomba ufafanuzi

2. Kuna story kuwa current ruling elites ni wa Zanzibari je kuna ukweli kwenye hili? Tuliambiwa kuwa baada ya mapinduzi Zanzibar waliokenda Oman walikuwa bado hawako Civilized ndio wa kapewa fursa mbali mbali na ndio walimilikishana Oman hapo ilipo is this true?

3. Niliskikia kuwa watu we using wengi wako maeneo ya salala na ndio waliojazana jeshini etc. Mbona hatuwaskii wala kuwaona kwenye utawala ???

4. Naomba wasitumie wa nephew wake Qabus anayeitwa Said Haytham tafadhali

5. Naomba utueleze kwa nini Oman haija invest sana Zanzibar ambayo wana cultural linkages kuliko nchi yoyote ile ya GCC??


6. Hebu tupate historia ya wale wahindi akina Khimijis ambao wako close sana na ruling elites wa Oman

7. Inasemekana kuwa aliyekuwa balozi wa Oman toka 2012 alirejeshwa nyumbani na Magufuli kwa makosa makubwa sana je kuna ukweli wowote au bas tuuu story za mitaani?

1. Uliambiwa na nani? Ingekuwa vizuri zaidi Kama ungekuja na chanzo chako.
Katika vyanzo vyote nilivyovisoma katika vitabu na katika mtandao, watoto wawili wa Sultan waligombania Usultani.

Uiingereza, akawaamulia Usultani ugawanywe. Mmoja kaenda Oman, mwingine kaja Zanzibar.

Nimeweka majina yao.

Kama kuna sababu nyingine, sijazisoma bado. Kama unazo, naomba utuwekee chanzo chake.

2. Hiyo ni hadithi za vijiweni. Waliorudi Oman wameanza maisha tena kama mgeni mhamiaji yoyote. There is no free lunch. Ukisoma unapata kazi nzuri.

3. Chanzo chako?
Sultan Qaboos aliweza kuwashinda kijeshi Dhofar Liberation Front baada ya kusaidiwa na Jordan, Iran na Uiingereza. Baada ya hapo, watu wa Salalah wakapewa maisha mema zaidi ili wasipigane tena na Sultan au kuomba wajitenge. Leo Salalah ni shwari.

Sina info kuhusu mambo ya kijeshi lakini Najuwa kuwa Uiingereza ni rafiki mkubwa wa Sultan Qaboos na wanajeshi wengi wa Uiingereza wapo jeshini kwake kulinda amani na kusaidia asipinduliwe.

Nanukuu program ya Sultan Qaboos baada ya kumpindua baba'ke na kujaribu kumaliza vita:

His "five point plan" involved:

A general amnesty to all those of his subjects who had opposed his father;

An end to the archaic status of Dhofar as the Sultan's private fief and its formal incorporation into The Sultanate of Oman as the "southern province";

Effective military opposition to rebels who did not accept the offer of amnesty;

A vigorous nationwide programme of development;

Diplomatic initiatives with the aims of having Oman recognised as a genuine Arab state with its own legal form of government, and isolating the PDRY from receiving support from other Arab states.

Within hours of the coup, British Special Air Service (SAS) soldiers were flown into the country to further bolster the counterinsurgency campaign.

Chanzo: revolvy.com

4. Sijakuelewa.

5. Una chanzo gani cha kuonyesha Oman hawawekezi Zanzibar?
Na hamna sheria inayolazimisha nchi iwekeze simply kwa kuwa na cultural link.

Najuwa kuwa Salim Ahmed Salim, alivyokuwa Waziri wa Ulinzi, Oman ilimpa Jeep 50 au 100 kama zawadi ya JWTZ alipomtembelea.

Na ukiona nchi inafungua Ubalozi nchini kwako miaka hii, ujue wana uhusiano mzuri wa biashara.

6. Sina info hiyo. Ila biashara yote duniani unatakiwa uwe na contact. The higher up the better. Hujasikia kuhusu connection za AIPAC wa Israel, Washington, DC?

7. Sina info. Tatizo, Tanzania , kila kitu ni Siri ya serikali. Ndiyo maana mitaani tunabaki na story za kutunga.
Mpaka leo, kwa mfano, hatujui mishahara ya Rais na serikali yake.

Nimejitahidi kukujibu kwa uwezo wangu.
 
Shukran sana mkuuu. Natumai as time goes by tutaendelea kupata nasaha zako

Kuhusu investments in Zanzibar nilidhani kutokana na shared values na Oman WA Omani wangekuwa wanafanya miradi mikubwa ya investments in Zanzibar kama vile free port,airport nk. Either way shukran
 
Shukran sana mkuuu. Natumai as time goes by tutaendelea kupata nasaha zako

Kuhusu investments in Zanzibar nilidhani kutokana na shared values na Oman WA Omani wangekuwa wanafanya miradi mikubwa ya investments in Zanzibar kama vile free port,airport nk. Either way shukran
Watawala wa Magogoni na Dodoma ndio wanaozuia Oman kuinufisha Zanzibar kwa kupandikiza chuki eti waarabu na Sultan wanataka kurudi kuinyakuwa Zanzibar na wakati huo huo kujinufaisha wao kwa kubadilisha the status kwa kuvutia hizo investments kwa upande wa Tanganyika na mfano mzuri ni Mradi wa EPZ ya Bandari ya Bagamoyo. Oman inawekeza 50%
 
Shukran sana mkuuu. Natumai as time goes by tutaendelea kupata nasaha zako

Kuhusu investments in Zanzibar nilidhani kutokana na shared values na Oman WA Omani wangekuwa wanafanya miradi mikubwa ya investments in Zanzibar kama vile free port,airport nk. Either way shukran


My pleasure.

Kila nchi inafanya biashara kutokana na mahitaji yao na self-interest.

Natural business partners wa Oman ni GCC market, watumiaji wake wa mafuta EU, USA na Wahindi across the Straits of Hormuz.

Pia, kuwekeza kunahitaji hali nzuri ya kisiasa. Zanzibar is not stable, CCM hataki kukubali kushindwa.
 
Utawala wa Sultan Zanzibar ulifanikiwa kuleta maendeleo makubwa kijamii na kiuchumi.
 
Watawala wa Magogoni na Dodoma ndio wanaozuia Oman kuinufisha Zanzibar kwa kupandikiza chuki eti waarabu na Sultan wanataka kurudi kuinyakuwa Zanzibar na wakati huo huo kujinufaisha wao kwa kubadilisha the status kwa kuvutia hizo investments kwa upande wa Tanganyika na mfano mzuri ni Mradi wa EPZ ya Bandari ya Bagamoyo. Oman inawekeza 50%

Hizo ni Propaganda zao.

Sawa sawa na sababu Nyerere Apologists wanazotoa kuhusu uchumi mbovu chini yake (vita vya Kagera). Bahati nzuri wikileaks wameonyesha anaomba msaada tangu 1974, kabla ya vita.

Biashara kubwa haziji mpaka hali ya siasa itulie na kura za wananchi wa Zanzibar ziheshimike.

Siyo kila mfanyabiashara ana uwezo wa kwenda London na Geneve kutafuta Arbitrator akidhulumiwa.
 
Dou Itashemashte.

Mkuu mgogoone, Mimi ni mwanafunzi wa historia bado.

Karibu kunifunza hapa.

Soo desnee sensei Tookyu.
Mkuu hongera sana Na shukrani kubwa Kwa kutufungua macho.Watashiwa skoshi nihongo waa karimasu.Katika mizunguko yangu nilikuwa sehemu za Kansai (Osaka,Kobe Na Kyoto)
Kijapani Changu kinanipiga chenga.
Hongera sana Mkuu nakutakia kila la kheri Na masomo.
 
Soo desnee sensei Tookyu.
Mkuu hongera sana Na shukrani kubwa Kwa kutufungua macho.Watashiwa skoshi nihongo waa karimasu.Katika mizunguko yangu nilikuwa sehemu za Kansai (Osaka,Kobe Na Kyoto)
Kijapani Changu kinanipiga chenga.
Hongera sana Mkuu nakutakia kila la kheri Na masomo.

Domo. Anata mo.
 
Back
Top Bottom