Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Hovyoooooooo. Tunapoongelea uhuru wa nchi tuondoe udini mwanangu vinginevyo hata nyani watatucheka. Hata kama mna ajenda yenu ambayo Mohamed ameshupalia siku zote, approach yenu ni hovyo tu hamtafanikiwa. Sasa kama waislam ndiyo waliopigania uhuru na Nyerere naye alikuwa muislam? UHURU wa Tanzania umepiganiwa na watanzania finish.Biti...
Mimi siku zote huo ndiyo ushauri wangu kwa wasomaji ambao wanaumizwa kwa kuandikwa historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kuona imejaa Waislam.
Huwashauri kutosoma nyuzi zangu.
Haipendezi kwa wao kusoma na kutoa matusi na kejeli.
Liber...Mzee wangu hakuna kitu kinanikwaza kama kuwasakama watu waliotutangulia mbele za haki
Father...Hovyoooooooo. Tunapoongelea uhuru wa nchi tuondoe udini mwanangu vinginevyo hata nyani watatucheka. Hata kama mna ajenda yenu ambayo Mohamed ameshupalia siku zote, approach yenu ni hovyo tu hamtafanikiwa. Sasa kama waislam ndiyo waliopigania uhuru na Nyerere naye alikuwa muislam? UHURU wa Tanzania umepiganiwa na watanzania finish.
Sikumaanisha kuwa umemsakama marehemu yeyote. Nilikuwa nikigusia hasa comment ya yule mdau aliyeweka maneno yasiyo na staha kuhusu Bibi Titi ilhali akijua mhusika alishatangulia mbele ya haki. Niwie radhi Mzee wangu kama comment yangu was ambiguousLiber...
Sijapata kusakama mtu yeyote katika maandiko yangu.
Nina vitabu, research papers na makala za kawaida hapa JF na kwenye magazeti na majarida kadhaa.
Ikiwa umeona nimefanya hivyo popote tafadhali hebu weka huo ushahidi huo hapa.
Kaka una pwenti. Ila simaanishi kusahau umuhimu wa watu katika kupigania uhuru. Ninachotaka kuweka wazi ni kwamba tuwatambue kama watanzania waliopigania uhuru wetu kama watanzania na si kama waislam au wakristo, wapwani au wabara. Kwangu ni kwamba uhuru wa Tanzania ulipiganiwa na watanzania regardless of their religious affiliations. Watanzania wana makabila ila nchi yao haina makabila bali ni taifa. Mchango wako si wa kudharauliwa katika kuandika historia ya Tanzania kama msomi na mtanzania. Shida yangu na maandiko yako ni ule mwelekeo wa udini udini. Sina shaka na usomi wako wala uzalendo wako. Nina shida na bias yako kuelekea uislam. Mfano, siku moja ningependa kusoma historia yako juu ya biashara ya utumwa. Wapo waandishi ambao ni biased watakwambia mzungu ndiye aliyenufaika na utumwa huku mwarabu akionekana agent wa kawaida jambo ambalo ni uongo.Father...
Hapo chini ni jibu kwa mmoja wa wasomaji wangu:
'''...ukisema unataka kuandika historia bila ya kujali dini utakuwa unajitumbukiza katika shida iliyowafika waandishi wa Chuo Cha CCM Kivukoni wa historia ya TANU.
Wao kama wewe walidhani wanaweza kuandika historia ya TANU kwa kukwepa mchango wa Waislam.
Matokeo yake leo tumeyaona baada ya mimi kuandika, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."
Tafuta picha ya Julius Nyerere na Mapadri katika harakati za kupigania uhuru kama utaiona.
Hatuna sababu ya kuuogopa ukweli wa historia ya Vita Vya Maji Maji wala historia ya TANU.
Walionyongwa na Wajerumani wanafahamika majina yao yapo kwenye minara ya kumbukumbu halikadhalika waliounda TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika wanafahamika wamo kwenye nyaraka na kwenye picha.
Picha ya kwanza ni Mnara wa Kumbukumbu ya Maji Maji Kilwa,a picha ya pili kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed, kushoto wa kwanza ni i. Tatu bint Mzee na hUyo katikati ni Julius Kambarage Nyerere akina mama hawa wanamsindikiza Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza ya Nyerere UNO mwaka wa 1955 na picha ya tatu ni Baraza la Wazee wa TANU.
Hii ni historia ya wazee wangu na nilipoona historia hii haipo niliamua kutafiti na kuiandika.
Ikiwa wewe hujapendezewa na hili basi na tuwiane radhi wala hapana sababu ya kufokeana na kutukanana.
Ningekuwa na faida gani mimi kwa jamii yangu hapa Dar es Salaam nilikozaliwa na kukua ikiwa ningeacha historia hii yote ipotee?
Ikiwa huipendi usiisome.
Kitabu katika miaka 23 toka kichapwe kwa mara ya kwanza Uingereza mwaka wa 1998 sasa kimechapwa mara nne.''
View attachment 1918611View attachment 1918613View attachment 1918633View attachment 1918628
View attachment 1918612
Liber...Sikumaanisha kuwa umemsakama marehemu yeyote. Nilikuwa nikigusia hasa comment ya yule mdau aliyeweka maneno yasiyo na staha kuhusu Bibi Titi ilhali akijua mhusika alishatangulia mbele ya haki. Niwie radhi Mzee wangu kama comment yangu was ambiguous
Father...Kaka una pwenti. Ila simaanishi kusahau umuhimu wa watu katika kupigania uhuru. Ninachotaka kuweka wazi ni kwamba tuwatambue kama watanzania waliopigania uhuru wetu kama watanzania na si kama waislam au wakristo, wapwani au wabara. Kwangu ni kwamba uhuru wa Tanzania ulipiganiwa na watanzania regardless of their religious affiliations. Watanzania wana makabila ila nchi yao haina makabila bali ni taifa. Mchango wako si wa kudharauliwa katika kuandika historia ya Tanzania kama msomi na mtanzania. Shida yangu na maandiko yako ni ule mwelekeo wa udini udini. Sina shaka na usomi wako wala uzalendo wako. Nina shida na bias yako kuelekea uislam. Mfano, siku moja ningependa kusoma historia yako juu ya biashara ya utumwa. Wapo waandishi ambao ni biased watakwambia mzungu ndiye aliyenufaika na utumwa huku mwarabu akionekana agent wa kawaida jambo ambalo ni uongo.
Nimalizie kwa kukushukuru kwa mchango wako hataa kama sikubaliani na mawazo yako hasa angle yako ya udini na si udini tu bali uislam. Nirejee na kusisitiza kuwa uhuru wa Tanzania ulipiganiwa na watanzania regardless of their religions. Uwe na siku njema kaka.
Mbona wapo wengi kama vile akina Paul Bomani, Mbowe (baba yake Freeman), Lawi Nangwanda Sijaona, mzee Rupia na engine wengi kaka pia bado hujagusia machief kibao mikoani.Father...
Naomba nipatie majina ya hao waliopigania uhuru nje ya haya majina niliyoyaleta mie baada ya kufutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika,
Sheikh Mohammed sisi huwa tanafaidika sana kwa kujifunza mengi kutoka kwako, kwa hivyo hao wasiopenda na waendelee tu na chuki zao.Father...
Hapo chini ni jibu kwa mmoja wa wasomaji wangu:
'''...ukisema unataka kuandika historia bila ya kujali dini utakuwa unajitumbukiza katika shida iliyowafika waandishi wa Chuo Cha CCM Kivukoni wa historia ya TANU.
Wao kama wewe walidhani wanaweza kuandika historia ya TANU kwa kukwepa mchango wa Waislam.
Matokeo yake leo tumeyaona baada ya mimi kuandika, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."
Tafuta picha ya Julius Nyerere na Mapadri katika harakati za kupigania uhuru kama utaiona.
Hatuna sababu ya kuuogopa ukweli wa historia ya Vita Vya Maji Maji wala historia ya TANU.
Kaka una pwenti. Ila simaanishi kusahau umuhimu wa watu katika kupigania uhuru. Ninachotaka kuweka wazi ni kwamba tuwatambue kama watanzania waliopigania uhuru wetu kama watanzania na si kama waislam au wakristo, wapwani au wabara. Kwangu ni kwamba uhuru wa Tanzania ulipiganiwa na watanzania regardless of their religious affiliations. Watanzania wana makabila ila nchi yao haina makabila bali ni taifa. Mchango wako si wa kudharauliwa katika kuandika historia ya Tanzania kama msomi na mtanzania. Shida yangu na maandiko yako ni ule mwelekeo wa udini udini. Sina shaka na usomi wako wala uzalendo wako. Nina shida na bias yako kuelekea uislam. Mfano, siku moja ningependa kusoma historia yako juu ya biashara ya utumwa. Wapo waandishi ambao ni biased watakwambia mzungu ndiye aliyenufaika na utumwa huku mwarabu akionekana agent wa kawaida jambo ambalo ni uongo.
Nimalizie kwa kukushukuru kwa mchango wako hata kama sikubaliani na mawazo yako hasa angle yako ya udini na si udini tu bali uislam. Nirejee na kusisitiza kuwa uhuru wa Tanzania ulipiganiwa na watanzania regardless of their religions. Uwe na siku njema kaka.
Salaam kwa yule anaejiita Floribert, amsikize kwa vizuri mchango wa hao asiowapenda kwenye uhuru wa tanganyika na hata ruanda urundi.WAISLAMU walijitoa sana ktk kutafuta uhuru kwakweli.
Father...Mbona wapo wengi kama vile akina Paul Bomani, Mbowe (baba yake Freeman), Lawi Nangwanda Sijaona, mzee Rupia na engine wengi kaka pia bado hujagusia machief kibao mikoani.
Kaka Mohamed, shukrani kwa mawazo yako na ufafanuzi wenye mengi ya maana ingawa sikubaliani nawe kuwa wewe ndiye unayeijua historia husika peke yako. Haya mambo ni intersubjective. Hivyo, kila mtu anachukua kile kimfaacho kama ambavyo umekuwa ukifanya. Ulichochukua wewe ni kupigia chapuo waislam kana kwamba wakristo hawakushiriki kudai uhuru. Nadhani ninachokuzidi ni ile hali ya kutambua kuwa waliopigania uhuru wa Tanganyika ni watanganyika na si waislam wala wakristo hata kama walikuwa na dini zao. Lengo lilikuwa ni kupigania uhuru na si dini. Pia, nadhani walijua kuwa dini ndicho chanzo kikubwa cha ukoloni kama utakumbuka namna wamissionari waliosaidia ukoloni kuenea Afrika. Hata hivyo, sikulaumu sana hasa ikizingatiwa kama alivyowahi kusema Wilson Churchill kuwa mara nyingi historia huandikwa na washindi. Hivyo, kuandika watakavyo badala ya inavyotakiwa. Unachofanya kwa wasio waislam ni sawa na kile Allies waliifanyia Ujerumani chini ya dhana ya reschstat ambapo katika kesi hii naweza kusema islamic reschstat. Kwa taifa kama letu ambalo Mwalimu Nyerere alilijengea misingi ya kijamaa yenye kukuza usawa na kupambana na udini, ujimbo, ukanda, ukabili na mabaya mengine, huwezi kufanikiwa hata kama vijana wetu wengi hawajui historia ya taifa lao. Watahoji tu kwa namna yoyote. Ukiondoa wewe siku zote kujionyesha kama msomi anayetetea udini, sina ugomvi nawe kifalsafa. Ugomvi wangu nawe ni kutaka tukubaliane na hii sumu ya udini unayoipenyeza kwenye historia ya Tanzania. Kama utaamua kuongelea misikiti na namna ilivyojengwa, kuchangiwa na vitu kama hivyo, angle yako barabara kaka yangu. Ila hili la historia ya ukombozi wa Tanganyika kuwa ya kiislam halina tija kwa tulio wengi ambao kwetu dini ni asasi za kikoloni sawa na serikali za kikoloni. Chini ya cultural imperialism, dini zinapaswa kupigwa vita na kutengwa na mambo yetu ya msingi. Leo sitaki nijikite kwenye hili hasa nikizingatia wengi watakwazika, itoshe kusema kuwa kuna haja ya kuanza kuzitaka dini zitulipe fidia kwa uharibifu wa mila zetu na kutuibia hata utambulisho kwa kutupachika majina machafu ya kizungu na kiarabu. Kwa leo naishia hapa kaka yangu Mohamed Said ambaye identity yako inakuonyesha kama mwarabu kuliko mswahili wa kawaida. Kila la heri.Father...
Nakuwekea hapo chini historia ya Paul Bomani kama nilivyokutananae katika Nyaraka za Sykes:
''Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo UNO kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine UNO.
Nia ya safari ya pili baada ya Kirilo ilikuwa kuisisitizia UNO kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini wake na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao.
Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Saadan Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hii.
Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi chini ya John Rupia aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.
Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua.
Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja kamati ya Abdu Kandoro ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga.
Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea kamati hii ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote.
Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.
(Report ya Lake Province Kwa Kifupi Iliyotolewa na Bwana Abbas K. Sykes, Nyaraka za Sykes).
Hayo hapo chini ni kutoka kwa Salum Mpunga na Yusuf Chembera waasisi wa TANU Lindi:
Ilikuwa kupitia juhudi zake binafsi Suleiman Masudi Mnonji ndipo TAA iliasisiwa Lindi ijapokuwa ilichelewa.
Mnonji alijitolea nyumba yake katika mtaa wa Makonde kama ofisi ya chama.
Mnonji kwa kutambua umuhimu wa kuwa na uongozi ulioelimika vizuri, alimleta Lindi Nangwanda Lawi Sijaona kutoka Nachingwea aje aishauri TAA jinsi ya kufanya mambo kwa utaalamu.
Wakati huo mjini Lindi kulikuwa na chama cha wafanyakazi bandarini Dockworkersí Union chini ya uongozi wa Mussa Athumani Lukundu, chama ambacho kwa kiasi chake kilianzisha vuguvugu la siasa za vyama vya wafanyakazi.
Machifu walichelewa sana kuiunga mkono TANU ukitoa wachache kama Mwami Theresa Ntare.
Chief Kidaha Makwaia wa Siha na Mangi Abdiel Shangali walikuwa wajumbe wa Legico kwa hiyo ilikuwa vigumu sana kwao kuunga mkono harakati za TANU.
Mwaka 1955 Abdulwahid na Dossa walialikwa na Chifu Adam Sapi kwenda Kalenga kwenye sherehe za kukabidhiwa fuvu la Chifu Mkwawa aliyejiua katika vita vya Wahehe na Wajerumani.
Chifu Adam Sapi Mkwawa aliingizwa kisirisiri ndani ya TANU na Dossa Aziz hivyo kuwa mmoja wa machifu wa wachache sana waliounga mkono TANU.
(Kwa maelezo ya Machifu waliounga mkono TANU angalia Sauti ya TANU No. 22 ya tarehe 28 Februari, 1958).
Father...
Unahitaji kujifunza historia ya Tanganyika kwa utulivu ili uwe katika hali ya kuweza kufanya mjadala.
Nikikusoma nakuona kuwa unadhani unajua lakini ukweli ni kuwa kama wengi walivyo mnakuja hapa kwa ghadhabu kupambana hakuna moja mlijualo katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Dah....alipata muda atumwagie ya Hamza pia 🤭Yakhee, tuletee historia fupi ya Sheikh Osama na katibu wake Sheikh Dr Ayman al-Zawahiri.
Asanta.
FaKaka Mohamed, shukrani kwa mawazo yako na ufafanuzi wenye mengi ya maana ingawa sikubaliani nawe kuwa wewe ndiye unayeijua historia husika peke yako. Haya mambo ni intersubjective. Hivyo, kila mtu anachukua kile kimfaacho kama ambavyo umekuwa ukifanya. Ulichochukua wewe ni kupigia chapuo waislam kana kwamba wakristo hawakushiriki kudai uhuru. Nadhani ninachokuzidi ni ile hali ya kutambua kuwa waliopigania uhuru wa Tanganyika ni watanganyika na si waislam wala wakristo hata kama walikuwa na dini zao. Lengo lilikuwa ni kupigania uhuru na si dini. Pia, nadhani walijua kuwa dini ndicho chanzo kikubwa cha ukoloni kama utakumbuka namna wamissionari waliosaidia ukoloni kuenea Afrika. Hata hivyo, sikulaumu sana hasa ikizingatiwa kama alivyowahi kusema Wilson Churchill kuwa mara nyingi historia huandikwa na washindi. Hivyo, kuandika watakavyo badala ya inavyotakiwa. Unachofanya kwa wasio waislam ni sawa na kile Allies waliifanyia Ujerumani chini ya dhana ya reschstat ambapo katika kesi hii naweza kusema islamic reschstat. Kwa taifa kama letu ambalo Mwalimu Nyerere alilijengea misingi ya kijamaa yenye kukuza usawa na kupambana na udini, ujimbo, ukanda, ukabili na mabaya mengine, huwezi kufanikiwa hata kama vijana wetu wengi hawajui historia ya taifa lao. Watahoji tu kwa namna yoyote. Ukiondoa wewe siku zote kujionyesha kama msomi anayetetea udini, sina ugomvi nawe kifalsafa. Ugomvi wangu nawe ni kutaka tukubaliane na hii sumu ya udini unayoipenyeza kwenye historia ya Tanzania. Kama utaamua kuongelea misikiti na namna ilivyojengwa, kuchangiwa na vitu kama hivyo, angle yako barabara kaka yangu. Ila hili la historia ya ukombozi wa Tanganyika kuwa ya kiislam halina tija kwa tulio wengi ambao kwetu dini ni asasi za kikoloni sawa na serikali za kikoloni. Chini ya cultural imperialism, dini zinapaswa kupigwa vita na kutengwa na mambo yetu ya msingi. Leo sitaki nijikite kwenye hili hasa nikizingatia wengi watakwazika, itoshe kusema kuwa kuna haja ya kuanza kuzitaka dini zitulipe fidia kwa uharibifu wa mila zetu na kutuibia hata utambulisho kwa kutupachika majina machafu ya kizungu na kiarabu. Kwa leo naishia hapa kaka yangu Mohamed Said ambaye identity yako inakuonyesha kama mwarabu kuliko mswahili wa kawaida. Kila la heri.
Father...Kaka Mohamed, shukrani kwa mawazo yako na ufafanuzi wenye mengi ya maana ingawa sikubaliani nawe kuwa wewe ndiye unayeijua historia husika peke yako. Haya mambo ni intersubjective. Hivyo, kila mtu anachukua kile kimfaacho kama ambavyo umekuwa ukifanya. Ulichochukua wewe ni kupigia chapuo waislam kana kwamba wakristo hawakushiriki kudai uhuru. Nadhani ninachokuzidi ni ile hali ya kutambua kuwa waliopigania uhuru wa Tanganyika ni watanganyika na si waislam wala wakristo hata kama walikuwa na dini zao. Lengo lilikuwa ni kupigania uhuru na si dini. Pia, nadhani walijua kuwa dini ndicho chanzo kikubwa cha ukoloni kama utakumbuka namna wamissionari waliosaidia ukoloni kuenea Afrika. Hata hivyo, sikulaumu sana hasa ikizingatiwa kama alivyowahi kusema Wilson Churchill kuwa mara nyingi historia huandikwa na washindi. Hivyo, kuandika watakavyo badala ya inavyotakiwa. Unachofanya kwa wasio waislam ni sawa na kile Allies waliifanyia Ujerumani chini ya dhana ya reschstat ambapo katika kesi hii naweza kusema islamic reschstat. Kwa taifa kama letu ambalo Mwalimu Nyerere alilijengea misingi ya kijamaa yenye kukuza usawa na kupambana na udini, ujimbo, ukanda, ukabili na mabaya mengine, huwezi kufanikiwa hata kama vijana wetu wengi hawajui historia ya taifa lao. Watahoji tu kwa namna yoyote. Ukiondoa wewe siku zote kujionyesha kama msomi anayetetea udini, sina ugomvi nawe kifalsafa. Ugomvi wangu nawe ni kutaka tukubaliane na hii sumu ya udini unayoipenyeza kwenye historia ya Tanzania. Kama utaamua kuongelea misikiti na namna ilivyojengwa, kuchangiwa na vitu kama hivyo, angle yako barabara kaka yangu. Ila hili la historia ya ukombozi wa Tanganyika kuwa ya kiislam halina tija kwa tulio wengi ambao kwetu dini ni asasi za kikoloni sawa na serikali za kikoloni. Chini ya cultural imperialism, dini zinapaswa kupigwa vita na kutengwa na mambo yetu ya msingi. Leo sitaki nijikite kwenye hili hasa nikizingatia wengi watakwazika, itoshe kusema kuwa kuna haja ya kuanza kuzitaka dini zitulipe fidia kwa uharibifu wa mila zetu na kutuibia hata utambulisho kwa kutupachika majina machafu ya kizungu na kiarabu. Kwa leo naishia hapa kaka yangu Mohamed Said ambaye identity yako inakuonyesha kama mwarabu kuliko mswahili wa kawaida. Kila la heri.
Kaka asante japo naona kama unapindisha ukweli. Sina ugomvi na uhakika na usahihi wa maandiko na namna ulivyoandika historia husika. Kubali yaishe kuwa angle ya udini ndiyo inayokutia kasoro. Hata hivyo vyuo siku moja vikipata watu kama sisi kuhoji––na hii ndiyo raha ya taaluma–––vitakuita tena ima ueleze au kukaribisha maoni tofauti. Nilipokuita hovyooo, nilimaanisha kabla hatujaanza kujibizana. Kitu cha hovyo tu nikionacho ni kutetea udini badala ya utaifa. Sina zaidi ya hapa na wala siombi msamaha kwa kupigania utaifa nikijitenga na udini na ukabila ambavyo vimekwamisha nchi nyingi barani Afrika.Fa
Father...
Mimi lazima niheshimu fikra za wengine na naamini huo ndiyo uungwana.
Nimesoma historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Kilichonishangaza, kunishtua na kunisikitisha ni kuona kuwa historia hiyo imewaacha wazalendo waliojitolea kwa hali na mali kuutafuta uhuru.
Kilichonifanya nijue kuwa historia imekosewa ni kuwa waasisi wa harakati za uhuru ni wazee wangu kwa hiyo naijua.
Bahati mbaya historia hiyo iliyokuwa inasomeshwa kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu hawa wazee wangu wote hawamo.
Nilichofanya nilikaa kitako nikaiandika historia hiyo.
Kitabu changu sasa kinakwenda mwaka wa 24 na kimechapwa mara 4 kwa kuwa kimependwa sana.
Sasa ikiwa kuna mtu hapendezewi na historia hii ni bahati mbaya sana kwake.
Ikiwa kuna mtu anaona historia hii niliyoandika mimi si historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika mlango uko wazi na aandike.
Kitabu changu kipo na kinasomeshwa vyuo vingi Ulaya na Marekani vinavyosomesha historia ya Afrika.
Inawezekana wewe hujui lakini kitabu changu kimebadili historia nzima ya uhuru wa Tanganyika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
TV na Radio Stations hazikauki mlangoni pangu kuja kunihoji pamoja na TBC kuhusu historia hii achilia mbali wanafunzi wa vyuo vikuu ndani na nje ya Tanzania.
Hivi karibuni tu nimepokea watafiti kutoka CCM Dodoma.
Kilele ni pale nilipoalikwa kuzungumza Northwestern University Evanston Chicago, Illinois, Marekani.
Mimi nitake nini zaidi?
Kubishana na wewe hapa JF?
Labda nikukumbushe ikiwa umepitiwa.
Huko nyuma umeniita, "hovyoooo."
Lakini sasa naona lugha imebadilika.
Wenzako wengi huanza hivyo na humalizikia hivi.
Abdulwahid Kleist Sykes kadi yake ya TANU ni no. 3, no. 2 ni Ally Kleist Sykes na no. 1 ni Julius Kambarage Nyerere.
Baba yao hawa ndugu watatu ndiyo katibu muasisi wa African Association mwaka wa 1929.
Abbas Kleist Sykes kadi yake ni no. 7.
Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa katika TAA Political Subcommitee kamati iliyokuja kuunda TANU.
Sheikh Suleiman Takadir alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.
Unawajua waliojitahidi kuifuta historia hii?
Mimi nawajua kwa majina.
Kabla kunisoma wewe uliijua historia hii?
Vipi leo atokee mtu anisahihishe katika kitu yeye hakijui wala hana ujuzi nacho?
Father...Kaka asante japo naona kama unapindisha ukweli. Sina ugomvi na uhakika na usahihi wa maandiko na namna ulivyoandika historia husika. Kubali yaishe kuwa angle ya udini ndiyo inayokutia kasoro. Hata hivyo vyuo siku moja vikipata watu kama sisi kuhoji––na hii ndiyo raha ya taaluma–––vitakuita tena ima ueleze au kukaribisha maoni tofauti. Nilipokuita hovyooo, nilimaanisha kabla hatujaanza kujibizana. Kitu cha hovyo tu nikionacho ni kutetea udini badala ya utaifa. Sina zaidi ya hapa na wala siombi msamaha kwa kupigania utaifa nikijitenga na udini na ukabila ambavyo vimekwamisha nchi nyingi barani Afrika.
Shukrani na kila la heri
Father of All