Mbona wapo wengi kama vile akina Paul Bomani, Mbowe (baba yake Freeman), Lawi Nangwanda Sijaona, mzee Rupia na engine wengi kaka pia bado hujagusia machief kibao mikoani.
Father...
Nakuwekea hapo chini historia ya
Paul Bomani kama nilivyokutananae katika Nyaraka za Sykes:
''Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo UNO kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine UNO.
Nia ya safari ya pili baada ya Kirilo ilikuwa kuisisitizia UNO kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini wake na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao.
Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Saadan Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hii.
Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi chini ya
John Rupia aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.
Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua.
Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja kamati ya Abdu Kandoro ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga.
Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa,
Paul Bomani aliipokea kamati hii ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote.
Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.''
(
Report ya Lake Province Kwa Kifupi Iliyotolewa na Bwana Abbas K. Sykes, Nyaraka za Sykes).
Hayo hapo chini ni kutoka kwa Salum Mpunga na Yusuf Chembera waasisi wa TANU Lindi:
''Ilikuwa kupitia juhudi zake binafsi Suleiman Masudi Mnonji ndipo TAA iliasisiwa Lindi ijapokuwa ilichelewa.
Mnonji alijitolea nyumba yake katika mtaa wa Makonde kama ofisi ya chama.
Mnonji kwa kutambua umuhimu wa kuwa na uongozi ulioelimika vizuri, alimleta Lindi
Nangwanda Lawi Sijaona kutoka Nachingwea aje aishauri TAA jinsi ya kufanya mambo kwa utaalamu.
Wakati huo mjini Lindi kulikuwa na chama cha wafanyakazi bandarini Dockworkersí Union chini ya uongozi wa Mussa Athumani Lukundu, chama ambacho kwa kiasi chake kilianzisha vuguvugu la siasa za vyama vya wafanyakazi.''
Machifu walichelewa sana kuiunga mkono TANU ukitoa wachache kama Mwami Theresa Ntare.
Chief Kidaha Makwaia wa Siha na Mangi Abdiel Shangali walikuwa wajumbe wa Legico kwa hiyo ilikuwa vigumu sana kwao kuunga mkono harakati za TANU.
Mwaka 1955 Abdulwahid na Dossa walialikwa na Chifu Adam Sapi kwenda Kalenga kwenye sherehe za kukabidhiwa fuvu la Chifu Mkwawa aliyejiua katika vita vya Wahehe na Wajerumani.
Chifu Adam Sapi Mkwawa aliingizwa kisirisiri ndani ya TANU na Dossa Aziz hivyo kuwa mmoja wa machifu wa wachache sana waliounga mkono TANU.
(Kwa maelezo ya Machifu waliounga mkono TANU angalia Sauti ya TANU No. 22 ya tarehe 28 Februari, 1958).
Father...
Unahitaji kujifunza historia ya Tanganyika kwa utulivu ili uwe katika hali ya kuweza kufanya mjadala.
Nikikusoma nakuona kuwa unadhani unajua lakini ukweli ni kuwa kama wengi walivyo mnakuja hapa kwa ghadhabu kupambana hakuna moja mlijualo katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.