Historia gani ni ya kweli

Historia gani ni ya kweli

Huyu mzee ana udini sana anajulikana, watu km hawa ni HATARI SANA
Edward...
Kwako kuwa na historia ambayo hayumo Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi Sharifa bint Mzee na wazalendo wengine waliokuwa mstari wa mbele katika TANU ndiyo kutokuwa mdini?

Unaona sawa tuwe na historia isiyo ya kweli kwa kuogopa propaganda za udini kutoka kwa wale ambao hawakuwapo mstari wa mbele?
 
Edward...
Kwako kuwa na historia ambayo hayumo Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi Sharifa bint Mzee na wazalendo wengine waliokuwa mstari wa mbele katika TANU ndiyo kutokuwa mdini?

Unaona sawa tuwe na historia isiyo ya kweli kwa kuogopa propaganda za udini kutoka kwa wale ambao hawakuwapo mstari wa mbele?
Wewe ni mdini Una udini. Hapo ndio natofautiana na wewe! Na mtu kama wewe ndio kila sehemu mnaweka udini na Kupanda mbegu mbaya ya Udini katika nchi yetu. Kila kitu wewe unaleta Udini tuu. Ninyi mnarudisha nyuma maendeleo kwa ajili ya Udini.
 
Huyu mzee ana udini sana anajulikana, watu km hawa ni HATARI SANA
Hatari unaileta wewe sisi tunao mjua huyu mzee huku ujerumani na uengereza wewe ndo utaonekana juha,inapo tajwa dini ya kiislam tu katika swala basi wenye mikuki mshachomoa kuwarushia,
 
Wewe ni mdini Una udini. Hapo ndio natofautiana na wewe! Na mtu kama wewe ndio kila sehemu mnaweka udini na Kupanda mbegu mbaya ya Udini katika nchi yetu. Kila kitu wewe unaleta Udini tuu. Ninyi mnarudisha nyuma maendeleo kwa ajili ya Udini.
Bwana Edward huijui historia ya uhuru na sababu walioshika serikali wanaiogopa.

Laiti wazee wetu wangekuwa wabaguzi wa dini Nyerere asingekuwa kiongozi wa TAA, TANU na Tanganyika.

Je, unawajua waliompokea Nyerere Dar es Salaam ya miaka ya 1950 na kuishi na yeye kama ndugu yao?

Unajua nyumba aliyoishi Nyerere Dar es Salaam baada ya kuacha kazi ya ualimu Pugu?

Unaijua historia ya Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy na Nyerere na Mama Maria?

Je na ya Ali Msham na Nyerere na Mama Maria?
Je ya Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Nyerere?

Je historia ya Mshume Kiyate, Mwinjuma Mwinyikambi na Max Mbwana na Nyerere?

Bi. Shariffa bint Mzee na Suleiman Masoud Mnonji na Sheikh Yusuf Badi Lindi, Mtwara na Mikindani Waislam wengi wasio na hesabu Tanganyika nzima.

Wapi umesikia wametajwa?
Hawa walimbagua Nyerere kwa kuwa alikuwa Mkatoliki?

Hivi kuandika historia za mashujaa hawa waliofutwa katika historia ya uhuru wetu ndiyo imekuwa ubaguzi wa dini?

Au hujui kama historia hii ilifutwa?
Unawajua waliotishwa na historia hii na bado inawatia hofu hadi leo?

Nini sababu ya uoga huu?

Je uliridhika kuona kuwa historia hii haikuwa inafahamika na leo unachukia kuona mimi nimeiandika na watu wameanza kujua ukweli.

Unajua kuwa wenye madaraka ya kuongoza nchi si Waislam na mgao ni 20:80?

Rais Mkapa alielezwa hali tuliyonayo na akaomba ushahidi na ushahidi akapewa na Prof. Hamza Njozi kupitia kitabu cha mauaji ya Mwembechai.

Kitabu kilipigwa marufuku.

Huu ndiyo udini wenyewe.
Hili ni tatizo na linafahamika.

Wewe ungeridhika kuona Waislam wamehodhi serikali kwa 80%.
Sidhani.

Hii ndiyo mbegu mbaya uliyoitaja ati inapandwa na Waislamu.
Ukipenda naweza nikakusomesha somo hili.

Udini ulianza tu baada ya uhuru mwaka 1961 kwa kuwekwa mikakati ya kufuta historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hii ni mada ya inayojitegemea yenyewe.

Soma historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika si hii iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni mwaka wa 1981

Soma kitabu cha Abdul Sykes na mwandishi ni mie.
Kitabu kinakwenda toleo la tano toka kuchapwa mwaka wa 1998.

Kitabu kimependwa kwa kuwa kina historia ya kweli inayowavutia wasomaji wengi wao ni vijana wa kizazi ambacho hakikuwepo wakati wa kudai uhuru.

Ukweli wote umo humo ndani.

Kitabu hiki ndiyo sababu ya kuandikwa Biography of Julius Nyerere ikidhaniwa kuwa kinaweza kujibu masuala ndani ya kitabu cha Abdul Sykes.

Yapo mengi.
Ikiwa hujui kitu uliza wenye kujua ufahamishwe.

Mimi siandiki kufanya maskhara.
Naandika kuitafutia amani ya kweli nchi yangu.

Naandika ili viongozi wetu wachukue hatua kurekebisha hali hii.

Angalia picha hizo hapo juu.
Ulipatapo kuziona popote.

Ziko nyingi sana na zinajieleza wenyewe.
Je unaona ni sawa kuwa historia hii isifahamike?

Bado unaamini kuwa Waislam ni wabaguzi hata baada ya ushahidi huu?

1660189154044.jpeg
1660189354288.png
1660189484368.jpeg
 
Wewe ni mdini Una udini. Hapo ndio natofautiana na wewe! Na mtu kama wewe ndio kila sehemu mnaweka udini na Kupanda mbegu mbaya ya Udini katika nchi yetu. Kila kitu wewe unaleta Udini tuu. Ninyi mnarudisha nyuma maendeleo kwa ajili ya Udini.
Badala ya kuweka hoja za wazi na ushahidi unakimbilia kwenye udini. Wewe umefilisika kabisa. Akitajwa Julius sawa lakini akitajwa Ali tayari kuna udini! Mtu wa ajabu sana wewe.
 
Onea22,
Hakuna shida ni kitu gani ungetaka nieleze khasa.
mtoa mada ameongea general sana kwamba history ni vitu vya kubuni,,,
baadh ya wadau wameingia kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika,,but history tunaanzia kwenye history yaulimwengu umeanza vp,,tuje kwenye dunia imeanza vp,,tuje kwenye formation of continents,,tuje kwenye early life,,tuje kwenye zama za ma dinosars,,tuje kwa watu wa kale,,zama za mwe,,zama za chuma,,ustaarabu wa mwanzo,,tuje zama za dini kuanza,,tuje zama za wafilosofia na wanasayansi wakubwa,,tuje kwenye slavery,,tuje kwenye ukoloni,,tuje kwenye vita vya dunia,,tuje kwenye harakati za uhuru,,independence,,tuje cold war,,fall of ussr,,ugunduzi wa compyuta,,,tuje ugunduzi wa internet,,tuje september 11 ,,tuje economic criss 2007,,n.k ndio maana nilifupisha kwa kusema be specific history gani waiongelea??
 
Mimi Nina hamu kweli ya kujua ukweli kuwa Mungu alitokea wapi!?chanzo chake Nini!?
 
Back
Top Bottom