Historia imeandikwa Tanzania

Historia imeandikwa Tanzania

Billal Saadat

Senior Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
169
Reaction score
358
Haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania benki za Biashara kuweka rekodi faida zaidi ya trilioni 1.16 Tzs kwa Mwaka.

Ndani ya kipindi cha miaka miwili mabadiliko ni makubwa kutoka bilioni 500 kwa Mwaka 2021 hadi Trilioni 1.16 haijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu.

Watu wamepata imani kwenye Biashara kurejesha uwekezaji wa ndani, uwepo wa sera nzuri za Biashara ndiyo kichocheo cha mabadiliko haya.

Miaka mitano nyuma sisi sote ni mashahidi biashara zilifungwa na mabenki yalifilisika. Kilichofanyika Miaka hii miwili ni jambo la pongezi.

Huyu Mama anazidi kutupa suprise nyingi ambazo hatujazizoea.

Tuingie darasani kidogo Serikali huchukua asilimia 30 kama Corporate Tax hapa Serikali itakuwa imekusanya bilioni 348 kama Corporate Tax.

Ipo faida kwenye kutengeneza sera nzuri za kibiashara. Unakusanya bila jasho.

IMG_2585.jpg
 
Ndani ya miaka mitano ijayo kiasi kama hicho cha faida kitaingizwa na Bank moja sio sector nzima. Mazingira rafiki ya biashara ndo kilichohitajika. Subiri shida za Russia na Ukraine zipo mfumuko wa bei urudi chini.
 
Hizi benki zinatangaza kupata faida kubwa lakini cha kushangaza ni pale wanapotoa gawio kiduchu kwa wanahisa wao!😂😂
Ngojea uone NMB na CRDB watakapo declare dividends to their shareholders utashangaa!!😂😂
 
Back
Top Bottom