Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
Kama wewe ni mfuatiliaji wa historia na msomaji mzuri matukio ya kisiasa duniani na mabadiliko ya kidemokrasia katika nchi mbali mbali na hata kwenye ukombozi, utakubaliana na mimi mabadiliko ya demokrasia na katiba katika nchi hizo yaliambatana na maumivu makali ya viongozi wa vyama vyama vya upinzani likiwemo la kufungwa jela kwa kesi za kutengeneza.
Ilitokea kwa kina mzee Kenyatta, Raila Odinga wa Kenya, Mzee Mandela, kina Hakainde Hichilema wa Zambia na wengine.
Ukiona taifa limefikia sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wanafungwa jela kwa sababu ambazo ni za kubambikizia, ujue mabadiliko ya kidemokrasia katika eneo hilo hayako mbali. Hii ni kawaida kabisa ni kwa mujibu wa historia zilizopita na ndicho kitakachotokea kwa Tanzania. Kama tutabishana humu basi muda utaongea.
Kesi ya Freeman Mbowe kwa jinsi ushahidi unavyoendelea kwanza haiendani na matukio ya kigaidi, Unaona kabisa ni kama kuna kitu kinachongwa au kinatafutwa ili tu aende jela.
Hakuna ugaidi unaofadhiliwa kwa shilingi laki 6, ugaidi ni neno kubwa sana na linatisha. Huwezi kufananisha na kesi ya Mbowe ambayo unaona kabisa mashadi w upande wa mashtaka anahangaika.
Kuna uwezekano kabisa muda si mrefu CHADEMA wakaja kua sehemu ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania au kikaongoza kabisa nchi. Hii ni baada ya Wananchi kua na awareness .