Historia itakuza uzalendo au tujikite kupata katiba yakusimamia haki?

Historia itakuza uzalendo au tujikite kupata katiba yakusimamia haki?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Tunakwenda kutafuta uzalendo kwenye historia Leo hii karne ya 21, karne ambayo watu awataki kupoteza muda kusoma vitu visivyo na tija maishani Bali wanawaza kuwaza namna yakufanya ubunifu katika kila ngazi ya maisha.

Je, uzalendo wetu umepotea kwa sababu watu awajui historia au kwa sababu mfumo wa uendeshaji nchi unamakosa? Je, tusome historia ambayo hata watawala wakiisimilia wanajikita kuumbuana namna walivyoimomonyoa nchi kwa kuuza rasilimali zetu na kujilimikizia Mali?

Natamani ajitokeze kiongozi ambaye ataachana hata miradi mikubwa ajikite kwa gharama yoyote kutengeneza mtumo wa utoaji haki nchini ili haki isiwe mikononi mwa kiongozi Bali iwe mikononi mwa sheria.

Juzi nilisikitika kumsikia Waziri mmoja analalamika eti wafanyabiashara walikuwa wanakimbilia mqbaraza Kodi; kwa hiyo Kama watu wanakimbilia kwenye tafsiri ya sheria nayo ni kosa Tanzania? Kwamba wakienda huko kwenye mabaraza nakuwagaza wasimamiz wa kodi ndo tukimbilie kubadili mfumo badala ya kuajiri watu competent? Je tukienda nje mipaka ya nchi tunatumia mfumo wa usuluhishi wa kibiashara au tunatumia taskforce kupata haki?

Huu ni mfano mmoja wa namna ambayo usipokuwa na mfumo wa haki ni vigumu haki kupatikana......watu wanakwepa mfumo wa sheria wanakimbilia kwenye mfumo wa dola

Tujenge mfumo wa sheria tusijifunze historia maana historia inajiandika kila siku na kila mtu anaweza akaisoma kwa wakati wake. Dunia ahiitaji wanahistoria inahitaji watu wenye suluhisho na matatizo ya kila siku.
 
Tunapaswa kujua vitu hivi viwili ni lazima viende kwa pamoja yani History na Katiba vinatakiwa viwe sambamba.

Then tuweke mtaala wa Elimu unaoendana na nchi yetu , mwisho tupendane kati ya sisi kwa sisi.

Hivi vitu ndio vinawafanya wazungu watoboe ( uwezi kukuta mwili wa mzungu umeokotwa msituni) nawaza hawa watu ni sahihi waendelee

Marais wa afrika wakishika nchi wana vitu common katika vichwa vyao

1 . Visasi

2. Kuchota hela ( hapa kila mtu ana mbinu yake lkni kikubwa ni kuiba tu)

3. Kuweka marafiki katika sehemu mbalimbali.
 
umemaliza mama manake sioni hata historia hiyo imewapa uzalendo hao wazee wanaoondoka coz Kama uzalendo wa kujinyima mfano wa Nyerere nani mwingine wa kumfananisha?
 
Beatrice kamugisha!
Vipi Mzee wetu wa Mataga Company Limited, unataka kumtishia nyau kwa sababu anapingana na mawazo ya mfalme wako?

Watanzania tunataka Katiba Mpya! Tunataka Maisha Bora! Hatutaki Somo la Historia! Kama ni suala la Uzalendo, liwekewe tu vifungu vya kutosha kwenye hiyo Katiba Mpya!

Mambo ya kulazimishana kumsoma Mkwawa, Kinjekitile Ngwale usawa huu ni wastage of time and resources.
 
Jitu/bumunda linaingia madarakani kupitia wizi wa kura halafu linataka watu wawe wazalendo!🚶🚶🚶
 
Kamugisha watakutisha kina Magonjwa Mtambuka lakini ukweli ndiyo huo. Watu wanataka tuishi enzi za propaganda za ki communist za uzalendo uchwara, huku haki za wananchi zikiamuliwa na kukaliwa na wanasiasa badala ya sheria.

History inayotakiwa na wanasiasa na wala si history. Ni Ile ya kuwafurahisha wao
 
Vuta bhangi hadharani haya ndio madhara ya kujificha!
Vipi Mzee wetu wa Mataga Company Limited, unataka kumtishia nyau kwa sababu anapingana na mawazo ya mfalme wako?

Watanzania tunataka Katiba Mpya! Tunataka Maisha Bora! Hatutaki Somo la Historia! Kama ni suala la Uzalendo, liwekewe tu vifungu vya kutosha kwenye hiyo Katiba Mpya!

Mambo ya kulazimishana kumsoma Mkwawa, Kinjekitile Ngwale usawa huu ni wastage of time and resources.
 
Back
Top Bottom