Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Wakuu salam kwenu,
Tumeshuhudia kwenye Uchaguzi wa 2015 JF ilivyopigwa na kitu kizito kwenye suala la mtandao na hivyo kuzuia wananchi kupata taarifa.
Tulishuhudia hilo pia kwenye uchaguzi wa 2020 jinsi mtandao ulivyochezewa na 'jini' ikawa changamoto kupata taarifa na wale ambao biashara zao zilikuwa zinategemea mtandao waliathirika pakubwa. Club House mpaka leo haipatikani na wakiulizwa wanasema wao hawajazuia, kwa mara nyingine 'jini' amefanya kazi yake.
Tulishuhudia kwenye maandamano Kenya ili kuvuruga Gen Z, X ikafanyiwa mambo ikawa changamoto kuipata kwa kawaida.
Lakini pia tumeshuhudia nchi mbalimbali kuzima mtandao wakati wa uchaguzi kwa visingizio mbalimbali, tujifunze kutokana na historia, tusiwe wa vipofu wa kurudia makosa yale yale.
Tunaona jinsi mtandao unasumbua unasumbua sasa hivi na hakuna neno lolote kutoka kwenye mamlaka husika, naona maandalizi yameanza mapema kuangalia njia nzuri ya kuzuia baadhi ya sehemu huku mambo mengine yakiwa yanaenda kiasi kwamba wakija kuulizwa kwanini huku hakupatikani waje waseme hakuna tatizo, shida itakuwa kwenu sisi hatujafanya lolote si unaona kwengine mambo sawa?
Msisubiri hadi mambo yanashindwa kabisa ndio tuanza kudownload VPN, hata kuingia kwenye app/play store itakuwa tabu ubaki unalalamika tu shughuli zako zimekwama.
Matatizo ya kidigitali yanahitaji suluhu za kidigitali huu ndio muda wa kuhakikisha una VPN kwa simu yako, shughuli zako ziende vizuri huku ukipata taarifa kama kawaida.
Mapendekezo ya VPN nzuri ya kudownload kutoka kwa wadau👇👇👇

Tafuta hii playstore, haina matangazo ya ovyo ovyo na inafanya kazi vizuri - 1.1.1.1 WARP