Historia Pekee ya Pemba na Wapemba

Che...
Cheo kikubwa nilichopata kushika ni mkutubi (Librarian) wa darasa shule ya msingi.

Unaniwazia kuwa Rais wa Tanzania?
 
Che...
Cheo kikubwa nilichopata kushika ni mkutubi (Librarian) wa darasa shule ya msingi.

Unaniwazia kuwa Rais wa Tanzania?
Una haki ya kuwa na cheo chochote hapa Tanzania.
Librarians ni watu wenye akili nyingi sana kwakuwa wanasoma vitabu muda wote.

Kama huwezi kuwa Raisi kwa sababu ya Umri.
Basi mjibie Mwanao yaani Mtoto wako.

Kama mtoto wako akibahatika kuwa Raisi wa Tanzania utamshauri nini kuhusu hayo maswali yangu.
Ayajibu namna gani ?

Watu wanataka kukusikia ukijibu hayo maswali na sio mimi tu.

Wanataka kwa Hekima yako na umri wako unasemaje kuhusu nilivyo kuuliza ?
 
Historia hii inatisha sana.

Ikawaje Tanzania kupambania uhuru wa Afrika ilihali wananchi wake wapo dhalilili kiasi hiki?

Mzee,
Nasubiria kusoma zaidi hii historia. Kuna mengi sana tumedanganywa mashuleni.

Nchi inahitaji kutubu
 
Mzee Mohamed Said huwa namkubali sana kwa uandishi na simulizi zake. Anabusara sana!
 
Ipo hivi mzee akiwa rais maudhui ya nyuz zake ndo itakua vpaumbele vyake, dully saiks atakua waziri wa michezo na sanaa, bunge litahamia ukumbi wa anatoglo, wazee wake wote wataingizwa kwny mitaala ya shule wajulikane kisawasawa, historia ya taifa itaeditiwa pakubwa kwa mlengo wake, wazee wa barza kunywa gahawa free nch nzma,kariakoo itakua kama dubai
 
Lugoda,
Unafanya kejeli katika jambo ambalo halistahili kuchezwa shere.

Historia ya uhuru wa Tanganyika sasa ni nyingine si ile iliyokuwa sawa na mchuzi uliotiwa maji ya baridi.

Historia hii ya wazee wangu ipo katika Cambridge Journal of African History toka 1998 na imo katika Dictionary of African Biography toka 2011.

Maprofesa wa historia vyuo vingi duniani wanaposomesha historia ya Mwalimu Nyerere rejea muhimu ni kitabu cha Abdul Sykes na rejea hizo mbili nilizokutajia hapo juu.

Ndani ya Cambridge Journal of African History wanafunzi wanawasoma John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan waliofanya pitio la kitabu changu.

Katika Dictionary of African Biography wanafunzi wanamsoma Dr. Kwegyir Aggrey na Kleist Sykes.

Sababu ya rejea hii ni kuwa ilikuwa Dr. Aggrey ndiye aliyempa Sykes wazo la kuunda African Association alipokuja Tanganyika 1924.

Kleist aliunda African Association 1929 na katika kuona faida ya jumuia akaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 na taasisi zote hizi zilitoa mchango mkubwa katika kuundwa kwa TANU 1954 na kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Mkuu kabla hujaondoka Pemba tujuze pia asili au chimbuko la Rashfold wa Manchester United,, yule wakwetu kabisa,, tusiache asili ipotee
 
Mkuu kabla hujaondoka Pemba tujuze pia asili au chimbuko la Rashfold wa Manchester United,, yule wakwetu kabisa,, tusiache asili ipotee
He is of paternal Jamaican descent, and maternal Kittitian descent, with his grandmother being born on the West Indies island of Saint Kitts
 

Rais wa Kenya William Ruto amewapa uraia watu wa jamii ya Wapemba wasio na utaifa, ambao walitambuliwa rasmi tu kati ya makabila ya nchi hiyo mnamo Februari.

Uraia utawapa kundi hilo “kitambulisho na utambuzi wanaostahili” na kuruhusu jamii kupata huduma za umma, Rais Ruto alisema.

"Hii, kwa hakika, inamaliza hali ya watu wa Pemba kutokuwa na utaifa na kutengwa ambao umedumu kwa takriban miaka 100," alisema wakati wa hafla ya Ijumaa.

Jamii ya Wapemba inakadiriwa kuwa takriban 7,000 kwa idadi na wamejikita katika maeneo ya pwani ya Kenya ya Kwale, Kilifi, Mombasa na Lamu.

Rais alitoa vitambulisho, vyeti vya umiliki wa ardhi, vyeti vya kuzaliwa na hati za kusafiria katika hafla iliyoashiria kukamilika kwa mchakato wa usajili wa wanajamii wote.

Hatua hiyo hatimaye inawawezesha Wapemba kupata huduma kamili za umma kama shule, huduma za afya, hifadhi ya jamii na haki ya kufanya kazi ambayo wamekuwa wakinyimwa kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…