Historia/ Shujaa: Bibi Zura Karumbi, Afrika na Uafrika VOL 1

anonymousafrica

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
611
Reaction score
640
1.jpg

Mchawi mpatie mwanao amlee, kauli ina ukakasi hii. Ndio hatomuua, lakini je akimfundisha uchawi mtoto huyo na kuja kuwa balaa kwenye nyumba yako?. Kuna wachawi wameokoa watu na kupata tuzo. Wenzetu wa kabila Fulani wakikuhisi tu hata kama una macho mekundu wanakuua. Tumepoteza mashujaa wengi sana. Hii sio movie, maana usijedhania nataka kukusimulia hadithi za Merlin kwenye nchi ya Camelot.

Huu ni mkasa wa kweli kuhusu bibi Zura Karuhimbi. Mwanamke aliyeweza kuokoa mamia ya watu katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda 1994

Zura Karuhimbi hakuwa na silaha yeyote ya kujilinda wakati wanaume waliokuwa na silaha walipoizunguka nyumba yake na kumtaka awakabidhi watu aliokuwa amewahifadhi nyumbani mwake.
Umdali.jpg

Mwanamke huyo alikuwa anajulikana kuwa na nguvu za giza.

Hali iliyowafanya kundi hilo la wauaji kuwa na uoga na kumfanya mwanamke huyo mzee kuwaokoa watu zaidi ya 100 kuwa salama wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Vyumba viwili vidogo vilivyopo kijijini Musamo, kwa haraka vilikuwa sehemu salama kwa watusi, Waburundi na hata wazungu watatu walijificha humo wakati wa mauaji ya kimbari.

Makundi ya watu yaliripotiwa kuwa walikuwa wamejificha chini ya kitanda na eneo lingine la siri juu ya paa.

Huku wengine walisema kuwa alikuwa amewachimbia shimo kuwaficha.

_104900807_51d78e04-305b-4019-aee8-8797f89a727e.jpg

Baadhi yao walikuwa watoto ambao walichukuliwa kutoka kwa mama zao waliokufa, alisema hivyo.

Karuhimbi alimwambia mwandishi wa habari wa Rwanda Jean Pierre Bucyensenge katika kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari kuwa ,

“Silaha pekee ya Zura ilikuwa ni kuwatisha wauaji kuwa atawaloga wao pamoja na familia zao, “ bwana Bucyensenge alieleza
ada1f2a7f0f016c6505321479decc22452eac46e.jpg

Maisha yaliendelea huku akiwa ni mwanamke ambaye anaomboleza kupotea kwa mtoto wake katika vurugu hizo na binti yake ilijulikana kuwa aliwekewa sumu akafa.

Pamoja na umaarufu mkubwa alioupata kuwa alikuwa mchawi lakini hakuwa mchawi na wala hakuwahi kuwa mchawi.

IMG-20181213-WA0071.jpg

Mwaka 2006, bibi huyo alitunukiwa tuzo ya kupambana na mauaji ya kimbari na rais wa Rwanda Paul Kagame, Tuzo ambayo alikua analala nayo kitandani siku zote . Tuzo hiyo ilimpa nafasi ya kusimulia namna alivyookoa watu wengine 50 katika miaka ya nyuma. Aliweza kumwokoa kijana wa kitutsi miaka ya 1950. Wahutu waliua watoto wa kiume wa kitutsi, bibi huyu alimsaidia mwanamke mmoja aliyebeba mtoto wa kiume kwa kumfunga shanga kichwani ili wauwaji hao wamdhanie ni motto wa kiume.
IMG-20181213-WA0070.jpg

Na ilimsaidia motto Yule kuokoka kwenye mikono ya wanyamera. Bibi Zura alimfananisha motto Yule na Rais wa Rwanda Paul Kagame. Na kusema, nimemsaidia Kagame ambaye leo hii amenipatia tuzo. Hii ikimaanisha bibi Yule alikua akiamini katika Karma ( wazungu wanasema goes around comes around) kitisho cha uchawi chaokoa mamia nchini Rwanda.

mashujaa east africa6.jpg

kama watakufa basi na mimi pia nitakufa, Hata kama ningejua mtuhumiwa yeyote , nisingeweza kumzuia.”
 
View attachment 1451980
Mchawi mpatie mwanao amlee, kauli ina ukakasi hii. Ndio hatomuua, lakini je akimfundisha uchawi mtoto huyo na kuja kuwa balaa kwenye nyumba yako?. Kuna wachawi wameokoa watu na kupata tuzo. Wenzetu wa kabila Fulani wakikuhisi tu hata kama una macho mekundu wanakuua. Tumepoteza mashujaa wengi sana. Hii sio movie, maana usijedhania nataka kukusimulia hadithi za Merlin kwenye nchi ya Camelot.

Huu ni mkasa wa kweli kuhusu bibi Zura Karuhimbi. Mwanamke aliyeweza kuokoa mamia ya watu katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda 1994

Zura Karuhimbi hakuwa na silaha yeyote ya kujilinda wakati wanaume waliokuwa na silaha walipoizunguka nyumba yake na kumtaka awakabidhi watu aliokuwa amewahifadhi nyumbani mwake.

View attachment 1451981
Mwanamke huyo alikuwa anajulikana kuwa na nguvu za giza.

Hali iliyowafanya kundi hilo la wauaji kuwa na uoga na kumfanya mwanamke huyo mzee kuwaokoa watu zaidi ya 100 kuwa salama wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Vyumba viwili vidogo vilivyopo kijijini Musamo, kwa haraka vilikuwa sehemu salama kwa watusi, Waburundi na hata wazungu watatu walijificha humo wakati wa mauaji ya kimbari.

Makundi ya watu yaliripotiwa kuwa walikuwa wamejificha chini ya kitanda na eneo lingine la siri juu ya paa.

Huku wengine walisema kuwa alikuwa amewachimbia shimo kuwaficha.

View attachment 1451982
Baadhi yao walikuwa watoto ambao walichukuliwa kutoka kwa mama zao waliokufa, alisema hivyo.

Karuhimbi alimwambia mwandishi wa habari wa Rwanda Jean Pierre Bucyensenge katika kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari kuwa ,

“Silaha pekee ya Zura ilikuwa ni kuwatisha wauaji kuwa atawaloga wao pamoja na familia zao, “ bwana Bucyensenge alieleza
View attachment 1451983
Maisha yaliendelea huku akiwa ni mwanamke ambaye anaomboleza kupotea kwa mtoto wake katika vurugu hizo na binti yake ilijulikana kuwa aliwekewa sumu akafa.

Pamoja na umaarufu mkubwa alioupata kuwa alikuwa mchawi lakini hakuwa mchawi na wala hakuwahi kuwa mchawi.

View attachment 1451984

Mwaka 2006, bibi huyo alitunukiwa tuzo ya kupambana na mauaji ya kimbari na rais wa Rwanda Paul Kagame, Tuzo ambayo alikua analala nayo kitandani siku zote . Tuzo hiyo ilimpa nafasi ya kusimulia namna alivyookoa watu wengine 50 katika miaka ya nyuma. Aliweza kumwokoa kijana wa kitutsi miaka ya 1950. Wahutu waliua watoto wa kiume wa kitutsi, bibi huyu alimsaidia mwanamke mmoja aliyebeba mtoto wa kiume kwa kumfunga shanga kichwani ili wauwaji hao wamdhanie ni motto wa kiume.
View attachment 1451985
Na ilimsaidia motto Yule kuokoka kwenye mikono ya wanyamera. Bibi Zura alimfananisha motto Yule na Rais wa Rwanda Paul Kagame. Na kusema, nimemsaidia Kagame ambaye leo hii amenipatia tuzo. Hii ikimaanisha bibi Yule alikua akiamini katika Karma ( wazungu wanasema goes around comes around) kitisho cha uchawi chaokoa mamia nchini Rwanda.

View attachment 1451986
kama watakufa basi na mimi pia nitakufa, Hata kama ningejua mtuhumiwa yeyote , nisingeweza kumzuia.”
 
Ina maana kweli bibi hakuwahi kujaribu kumloga mtu live live hadi hao wauaji kuogopa bila ya kuona moto wake
 
Hahahahaaa sisi waafrika banaaa
Hawa Intarahamwe hawakuogopa kwenda kuwakatakata mapanga watu kanisani, ila wameogopa kwenda kuwachomoa kwa bibi aliewatisha kua yeye ni mchawi na wakimletea ujinga atateketeza mpaka panya wote kwenye ukoo wao.
Shkamoo Zito MwamiRuyagwa Kabwe.
 
Mungu hadhuru, lakini mchawi anakumaliza faster
 
Hahahahaaa sisi waafrika banaaa
Hawa Intarahamwe hawakuogopa kwenda kuwakatakata mapanga watu kanisani, ila wameogopa kwenda kuwachomoa kwa bibi aliewatisha kua yeye ni mchawi na wakimletea ujinga atateketeza mpaka panya wote kwenye ukoo wao.
Shkamoo Zito MwamiRuyagwa Kabwe.
HAHAHAHHAAAAA sasa Zitto anahusikaje hapo
 
Back
Top Bottom