Historia & Shujaa: Dedan Kimathi, Afrika na Uafrika Vol. 1

Historia & Shujaa: Dedan Kimathi, Afrika na Uafrika Vol. 1

anonymousafrica

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
611
Reaction score
640
mashujaa east africa2.jpg

Alizaliwa, akapambana na kuuliwa kikatili, tofauti na wengine, yeye hata nchi yake ilipanga kufutilia mbali historia yake na kumtambua. Marehem akumbukwe kwa mazuri bwana. Hata anapopumzika ajiskie kweli alifanya kitu. Hii ni imani yangu mimi muafrika, kama hyukubali pole sana.

Awamu mbili za utawala wa mwanzo wa Kenya baada ya uhuru, ile ya Mzee Jomo Kenyatta na baadaye wa mrithi wake, Daniel arap Moi, zilikataa kumtambua na kumpa Kimathi heshima ya kuwa mpiganiaji uhuru, zikimuangalia kama gaidi. Ndiomaana nikasema hata baada ya kifo chake walitaka kumpuuza.

Lakini baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na kuingia madarakani kwa Rais Mwai Kibaki hapo mwaka 2006, serikali ilimtangaza Kimathi kuwa ni shujaa wa vita. Na mimi namuunga mkono Kibaki.

Alipofika umri wa miaka 15, alijiunga na shule ya msingi kijijini kwao, Karuna-ini, ambako alijifunza Kiingereza kwa ufasaha na kuitumia lugha hiyo baadaye kuandika mengi kabla na baada ya uasi wa Mau Mau. Alishiriki sana katika mijadala shuleni na alikuwa na kipaji cha kuandika mashairi. Mimi Kuanzia leo nampa jina la Dedan Makengeza.
Alijiunga na jeshi la uingereza lakini alifukuzwa kwa madai ya utovu wa nidham. Na hapo akaenda kwenye ualimu lakini alikosa kazi pia baada ya muda. Akagundua bado waafrika au Kenya haipo huru na kuingia rasmi msituni mwaka 1951 ambapo akajiunga na wapiganaji wa Maumau.

ERCm1GQWAAEEXIe.png
Aliteuliwa kuwa katibu Mkuu wa wapiganaji hao katika tawi la Thomson Fall na kusimamia nidhamu kwa wanajeshi wa maumau. Inasemekana alisimamia viapo kwa wapiganaji hao na hata kutumia vitisho ili wanajeshi hao wakae kwenye mstari imara. Maana kwenye mapambano msaliti mmoja anaweza kusababisha matatizo kwa kikosi kizima. Hivyo Dedan aliwapika wapambanaji kisawasawa.

Mwaka wa 1951 alikamatwa na Wakoloni lakini askari weusi waliokuwa ndani ya kikosi cha usalama walimsaidia kutoroka.

Mwaka 1953, Kimathi akaunda Baraza la Ulinzi kuratibu shughuli za wapiganaji wote wa msituni.

Mwaka 1956, miaka minne tangu kuanza uasi huo, Kimathi alikamatwa katika misitu ya Nyeri na kundi lililoongozwa na Ian Henderson. Kukamatwa kwake kukawa mwisho wa vita vya msituni. Walikata mizizi mti wote ukaanguka lakini mapambano hayo yalikua chachu ya ukombozi na uhuru wa Wakenya.

KIMATHI.jpg

Alihukumiwa kifo na Jaji Mkuu O`Connor huku akiwa kitandani hospitali kuu mjini Nyeri. Alinyongwa mapema asubuhi ya tarehe 18 feb 1957 katika gereza kuu la Kimiti.

Mahala alipozikwa hadi leo hapajulikani.Juhudi nyingi zimefanyika ili kupata kaburi la Dedan. Kuna baadhi ya chapisho zilisema kaburi lake limepatikana lakini taarifa hiyo ilikanushwa.

Kimathi anaangaliwa kama shujaa wa taifa na serikali ya sasa na kuna sanamu maalum la "Mpigania Uhuru Dedan Kimathi" katikati ya jiji la Nairobi, lililozinduliwa tarehe 11 Desemba 2006, katika kumbukumbu ya tarehe aliyouwawa.

“Siongozi magaidi. Ninaongoza Waafrika ambao wanataka serikali yao binafsi na ardhi. Mungu hakukusudia kwamba taifa moja litawaliwe na mwingine milele. “
 
Hapo ndipo utaona ujinga wa mwafrika.
Kenya kwa miaka zaidi ya 40 hawakuweza kuuona na kuutambua mchango wake ktk uhuru wa Kenya.

Marais wote wawili walijiona na kujiita wazalendo,uzalendo ni kutojitambua mchango wa wenzako ktk ukombozi wa taifa?

Hapa Tanzania tuna viongozi wanaojiita wazalendo,na hawathamini mchango na mawazo ya watanzania wengine kwa kisingizio kwamba,wapinzani wao ni mawakala wa MABEBERU.

Kiongozi na mwanaume unamuogopaje beberu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sir Dedan, nilimjua kupitia kitabu cha the trial of Dedan Kimathi... one of the great men during colonial era,hawa watu walikuwa majasiri sasa hivi kidogo tu mtu anashusha silaha, sijui usongi uliwatengeneza na uliotutengeneza sisi ni tofauti?
 
Hahaha Dedan Kimathi, haya maneno kwenye signature yangu nimeyatoa kwenye hicho kitabu kinaitwa Dedan Kimathi....
 
Hivi hapa nyumbani hakuna sehemu ambayo imeandikwa history ya Kinjekitile Ngwale, toka utoto, kukua, Maji Maji na kufa kwake...... Madirector wa filamu/tamthilia wangepata hadithi nzuri sana
 
Angejua huko aliko vizazi alivyovipambania vinalilia kuwa wazungu sijui atajisikiaje. Wakenya wa leo wanaona sifa kuwa kama wazungu.
 
Shukran kwa kunitag jombaa. Field Marshal Dedan Kimathi Waciuri(Kimathi Wa Waciuri) aliwaongoza Mau Mau kivita na kiimani pia, wakiwa pamoja na General Stanley Mathenge Wa Mirugi, General China(Waruhiu Itote), Field Marshal Musa Mwariama na Field Marshal Muthoni Wa Kirima.
C1a32tpDC5dk.jpg
Hii hapa ni moja ya baadhi ya picha zake za mwisho, akiwa hospitalini Nyeri, siku vikosi vya mkoloni vilipomkamata, Oktoba 26, 1956. Walimkamata akiwa na matatizo ya kiafya, baada ya kumpiga risasi, wakampokonya silaha zake zote. Vikosi vya mkoloni navyo vilikuwa vimezingira sehemu yote hiyo walipomfikisha hapo hospitalini, ila bado hawazikutoa pingu hizo hapo kwenye picha. Hata baada ya wao kumhukumu na kumtia kitanzi tarehe 18 Februari 1957, bado walimzika na pingu mikononi, wakiamini kwamba anaweza akafufuka. Yaani aliwaogopesha sana na kuwatesa wakoloni, alikuwa shujaa kweli.
 
Hapo ndipo utaona ujinga wa mwafrika.
Kenya kwa miaka zaidi ya 40 hawakuweza kuuona na kuutambua mchango wake ktk uhuru wa Kenya.

Marais wote wawili walijiona na kujiita wazalendo,uzalendo ni kutojitambua mchango wa wenzako ktk ukombozi wa taifa?

Hapa Tanzania tuna viongozi wanaojiita wazalendo,na hawathamini mchango na mawazo ya watanzania wengine kwa kisingizio kwamba,wapinzani wao ni mawakala wa MABEBERU.

Kiongozi na mwanaume unamuogopaje beberu??

Sent using Jamii Forums mobile app
ukiwafundisha watoto historia... watakuja kuiishi ndiomaana waliogopa kumtambua
 
Hahaha Dedan Kimathi, haya maneno kwenye signature yangu nimeyatoa kwenye hicho kitabu kinaitwa Dedan Kimathi....
The day you understand why your father died: the day you ask yourself whether it was right for him to die so; the day you ask yourself: ......... that day, my son, you'll become a man."
 
Hivi hapa nyumbani hakuna sehemu ambayo imeandikwa history ya Kinjekitile Ngwale, toka utoto, kukua, Maji Maji na kufa kwake...... Madirector wa filamu/tamthilia wangepata hadithi nzuri sana
kupata hizo historia ni mziki...... kila kitu kilifichwa
 
Shukran kwa kunitag jombaa. Field Marshal Dedan Kimathi Waciuri(Kimathi Wa Waciuri) aliwaongoza Mau Mau kivita na kiimani pia, wakiwa pamoja na General Stanley Mathenge Wa Mirugi, General China(Waruhiu Itote), Field Marshal Musa Mwariama na Field Marshal Muthoni Wa Kirima.
C1a32tpDC5dk.jpg
Hii hapa ni moja ya baadhi ya picha zake za mwisho, akiwa hospitalini Nyeri, siku vikosi vya mkoloni vilipomkamata, Oktoba 26, 1956. Walimkamata akiwa na matatizo ya kiafya, baada ya kumpiga risasi, wakampokonya silaha zake zote. Vikosi vya mkoloni navyo vilikuwa vimezingira sehemu yote hiyo walipomfikisha hapo hospitalini, ila bado hawazikutoa pingu hizo hapo kwenye picha. Hata baada ya wao kumhukumu na kumtia kitanzi tarehe 18 Februari 1957, bado walimzika na pingu mikononi, wakiamini kwamba anaweza akafufuka. Yaani aliwaogopesha sana na kuwatesa wakoloni, alikuwa shujaa kweli.
apumzike kwa AMANI
 
Back
Top Bottom