Dar,enzi ya mjerumani.
Railway station hapo.
Mpanda farasi/punda anaelekea Gerezani
Hilo jengo ndio lile linaangaliana na central police. Huyo mpanda farasi anaelekea kule kwenye keep left ya kurasini au kule kwenye njia ya kwenda ofisi za TiGo na majani ya chai.
Dar enzi ya mjerumani
Sanamu la Bismark,ilikuwa kwenye botanical gardens, mwingereza akaiondoa na ile ya Wissmann pale askari monument, ya Wissmann ilirejeshwa Ujerumani. Kulikuwa na nyingine ya Bismark Tanga mjini.
Kariakoo hiyo enzi hizo. Huu ndiyo mtaa unaoingia Sokoni Kariakoo Shimoni. Huu ni mtaa wa Nyamwezi naona upande wa kushoto kuna mkunguni kwa kina marehemu Bwiru Kasembe na huu unakwenda mpaka Uhuru au Kichwele,Ukiangalia vizuri hiyo mishale miwili pembeni, inakuonyesha kingo za kuta za pembeni ambapo hapo magari ya mizigo yalikua yakipita na kushuka chini Shimoni kwa ajili ya kushusha ama kupakia bidhaa. Aliyepita maeneo hayo atakubaliana nami.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.